WANAUME NA MFUMO WA MAISHA, tusaidieni ma Doctor wa JF. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WANAUME NA MFUMO WA MAISHA, tusaidieni ma Doctor wa JF.

Discussion in 'JF Doctor' started by Going Concern, Feb 29, 2012.

 1. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  it's morning again, ngoja nikaoge, we mwanaume usioge maji ya moto, wanaume wakioga maji ya moto sio vizuri, inaua mbegu za kiume, utashindwa pata mtoto ....naenda kazi bila kuoga nisije kosa mtoto.

  oky, ngoja niwashe gari niende ofisini... ok lakini usipende kuendesha gari sana, kwani linaleta joto sehemu za siri, sio vizuri kwa wanaume, jaman, mi naenda tu, ofisini mbali....

  kabla sijaingia ofisini, ngoja nipite hapa nipigie chai ata na chapati mbili, stooop, acha kabisa, chai si nzuri kwa wanaume,,, ok basi nipe chapati kavu, usipende vitu vya mafuta sana sio vizuri kiafya ata mfumo wa uzazi pia... basi acha naenda ofisini


  kaka mida ya lunch, twenzetu, aya makazi yapo tu... Dada mi nipe ugali na nyama, unga wa sembe sio mzuri kiafya, usipende kutumia, kama ni dona sana, ata iyo nyama nyekundu sio nzuri kabisa acha ndugu yangu.. kaka mi narudi ofisini we kula tu. sina mtoto ata mmoja

  bora mida ya kazi imeisha, ngoja nipite hapa kwenye kikao cha harusi then niende nyumbani kwa wife.... kaka unakunywa nini? nipatie Serengeti ya moto, kaka bia ndo mbaya zaidi acha, inaua nguvu za kiume na mfumo wa uzazi, basi nipe soda, soda ndo kabisaaaaa, acha! jamani mi naenda nyumbani nimechoka sana

  vipi wife leo umepika nini? ata sijapika ndo nafika toka ofisini, nimechukua chips kuku. usiguse ndugu yangu, tena chips ukiweza usiguse kabisa... mi nalala ma wife we kula tu..

  jaman, tuishe vipi sie watoto wa kiume? tusaidieni ma doctors ..
   
 2. D

  Dotowangu JF-Expert Member

  #2
  Feb 29, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  kaka usipeangalia utakufa kwa kwashakoo eti unaogopa kupata kupoteza nguvu... Kama vip hamia kijijini uwe unjisevia maboga, togwa, na makande.
   
 3. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #3
  Feb 29, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mkuu kwa uzalishaji wa mbegu unategemea sana na joto na hilo joto linatakiwa liwe la chini yaani utoe 2 degree centigrade kwenye joto la mwili wako 36.5-37.3 likiwa juu ya hilo ulilotoa likawa juu basi uzalishaji wa mbegu utapungua .umejaribu kutoa sababu za kupungua kwa mbegu hapo juu kama zitaongeza joto basi uwezekano huo upo.lakini kwenye chai hapana haiwezi sababisha kupungua kwa mbegu, kwenye pombe yaani serengeti hapo ni big true, lakini siyo ugumba na maanisha uzalishaji wa mbegu unapungua. NITARUDI
   
 4. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #4
  Feb 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Fisi alichanika msamba nja panda kwa kutaka kuhudhuria karamu pande zote!
   
 5. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 934
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  classic .......thanx ndugu.
   
 6. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama bado ni kijana, basi puyanga na vyote ulivyo jizuia. Production ya mbegu ina rejuvinate haraka sana. Labda kama uko above 50.

  Babu yangu hakujikataza cho chote ujanani mwake isipokuwa pombe. Lakini kwa wake zake wawili alizaa watiti 18. Mmoja wao ni baba yangu. Sasa ukitaka kuchunguza saaaaana science za kisasa, utajikuta unajizuia kila kitu lakin na mtoto usipate.
   
 7. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa vipingamizi vyote hvo wanaume tunashida, kwa maeneo kama iringa, mbeya huku usipooga maji moto asubuh unaeza ukaganda bafuni mkuu, na kuhusu chai duuh sidhani kama inatatizo labda kwenye serengeti nayo ukiinywa kupita kiasi. Mkuu hata chipsi ni msala lakini ugali we kula tu bwana mixer manyama na mamboga ya kijani, kwenye suala la usafiri yaweza kuwa na ukweli, lakini mimi babayanga amekuwa driver kabla ya uzao wangu na mpaka sasa anadrive na tupo wanae wa4 nikiwa ndo kifungua mimba so nadhani endesha tu gari yako uwah kazini,
   
 8. ram

  ram JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 6,203
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Duh, nimmecheka sana, kila kitu hutakiwi kutumia? si utapata utapiamlo mkuu
  Ngoja wanaume wenzio waje, watakusaidia

   
 9. la Jeneral

  la Jeneral JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  fanya vyooote ila mazoezi,mda wa kupumzika,kula vizuri,maji mengi ya kunywaaa hapo mbeguuuuu kibao mpaka zitakuwasha teh teh
   
Loading...