Wanaume Mungu anawaona! Nipo kwenye ndoa miaka 2 na nina mtoto, nimegundua mume ana-cheat

miss charming

JF-Expert Member
Dec 3, 2016
910
895
Habari za mida wana MMU,

Jamani hapa nimechanganyikiwa sielewi, nipo kwenye ndoa miaka 2 na nina mtoto mmoja wa mwaka na ndani ya huo muda wote sijawahi kuhisi mume wangu kunicheat japo kuna wakati huwa anachelewa kurudi ananiambia ni mambo ya kazi tunasort yanaisha.

Sasa majuzi nimekuta nilishika simu yake ndogo, nikakuta sms anamwambia mwanamke amemiss mapenzi anayompa, anajuta kwanini hakumjua mapema, anampenda sana na mambo kama hayo, toka majuzi mpaka muda huu sijamwambia ila yeye amashaanza kujistukia yaan amekuwa mpole ghafla anajikanyaga kanyaga tu.

Nimekuja humu najua kuna wake na waume za watu ma-legend ambao wameshapitia hii adha mnipe ushauri what to do maana nimechanganyikiwa nikikumbuka hizo sms kichwa kinapata moto.

Nawaza hata nimuache asee maana upendo wenyewe hakuna tena.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
23,196
47,155
Koleza mapenzi mama mpe yote, uno liwe feni, utoe na sauti ya ufufuo wa wafu, jicho liwe kama la kiramba sukari.

Mpende mmeo tulia ndoani ukitoka huko tuliopo nje ya mchezo tunamikwara kushinda huyo malaika.
 
RReigns

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
17,650
32,539
Ukiondoa hilo ana kasoro nyingine? Je, hakuonyeshi mapenzi ya kweli?

Nafikiri stik kwenye mambo ya maana zaidi, mambo yake ukiweza muachie mwanyewe. Kikubwa anawajibika ipasavyo kukupenda na kukutunza wewe na familia kiujumla.

Unaweza kumuacha huyo ukakutana na makubwa zaidi unyanyasaji wa kijinsia etc.

Tena ukiweza ongeza mapenzi maradufu yaani usionyeshe changes zozote kuwa umejua. najuua ni ngumu embu jaribu unaweza pata matokeo chanya. Wee play part yako tu.

Siku zote binadamu hukwepa hatari, unakuwa mtu wa ajabu kuifuata na kuitafuta shari vinginevyo uwe na sababu ya msingi.
 
Gray wolf

Member
May 7, 2022
18
18
Ni vizuri ukawa mvumili kwan mesej si kigezo tosha chakusaliti ndoa.

Jarib kujipa muda wakuchk zaid, kwan nyakat zingine wanaume huamua kuwapitisha wanawake ktk moto japo waponao ndan ya ndoa.

Jipe angalau miez 3 had sita huwa ukifuatilia mawasiliano hayo kwa siri kubwa kwan akibaini anaweza kugeuza mzik kwako tofaut nauvyofikri.
 
Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Apr 2, 2017
7,871
17,691
Dhambi ya usaliti haina cha kuvumilia, muuleze atambue afahamu kuwa umefahamu anavyo vifanya. Ingefaa ungetunza na ushahidi hii itakusaidia kunapokua na maamuzi ya pande mbili upate cha kusemea.

Usifuge ujinga, fikiria ingekua upande wake yeye angevumilia
 
Suzana Alfred

Member
Oct 3, 2021
88
115
Habari za mida wana MMU, jamani hapa nimechanganyikiwa sielewi, nipo kwenye ndoa miaka 2 na nina mtoto mmoja wa mwaka na ndani ya huo muda wote sijawahi kuhisi mume wangu kunicheat japo kuna wakati huwa anachelewa kurudi ananiambia ni mambo ya kazi tunasort yanaisha. Sasa majuzi nimekuta nilishika simu yake ndogo, nikakuta sms anamwambia mwanamke amemiss mapenzi anayompa, anajuta kwann hakumjua mapema, anampenda sana na mambo kama hayo, toka majuzi mpaka muda huu sijamwambia ila yeye amashaanza kujistukia yaan amekuwa mpole gafra anajikanyaga kanyaga tu .. nimekuja humu najua kuna wake na waume za watu malegend ambao wameshapitia hii hadha mnipe ushauri what to do maana nimechanganyikiwa nikikumbuka hizo sms kichwa kinapata moto.. nawaza hata nimuache asee maana upendo wenyewe hakuna tena.
Dada ebu rudia tena eti unawaza umuache?
Yaani umuache mume??! Kwa dunia hii umuache mume!! Anahudumia familia kabisa au? Tatizo ndo hilo la kuchepuka tu ndo uache mume?

Ebu mwambie kaeni chini huenda kweli kuna sehem humfinyii vizuri.
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
3,466
3,719
Habari za mida wana MMU, jamani hapa nimechanganyikiwa sielewi, nipo kwenye ndoa miaka 2 na nina mtoto mmoja wa mwaka na ndani ya huo muda wote sijawahi kuhisi mume wangu kunicheat japo kuna wakati huwa anachelewa kurudi ananiambia ni mambo ya kazi tunasort yanaisha. Sasa majuzi nimekuta nilishika simu yake ndogo, nikakuta sms anamwambia mwanamke amemiss mapenzi anayompa, anajuta kwann hakumjua mapema, anampenda sana na mambo kama hayo, toka majuzi mpaka muda huu sijamwambia ila yeye amashaanza kujistukia yaan amekuwa mpole gafra anajikanyaga kanyaga tu .. nimekuja humu najua kuna wake na waume za watu malegend ambao wameshapitia hii hadha mnipe ushauri what to do maana nimechanganyikiwa nikikumbuka hizo sms kichwa kinapata moto.. nawaza hata nimuache asee maana upendo wenyewe hakuna tena.
Mhn! kwanza jikubali kuwa wewe ndio mke unayepentwa na kutambulika hizo zingine huwa ni swaga zetu tulipie kwa upungufu huduma. kingine elewa hakuna mwanamme wa tanzania aliyemkamilifu wote tunachepuka sema tunatofautiana degree ya uchepukaji kwa hiyo tokea sasa kubali lazima mumeo atachit lakini hii isiwe sababu ya wewe kushindwa kuidhibiti hali hiyo! tumia vizuri macho yako kwake na uombe MUNGU kibali kwa ajili ya mume wako aweze kukukubali na kukupenda.
vinginevyo ndoa ni kuvumiliana zaidi kuliko kupendana.
ndoa
doa
oa
a
 
Mama pretty

JF-Expert Member
May 1, 2020
1,298
2,309
Koleza mapenzi mama mpe yote,uno liwe feni,utoe na sauti ya ufufuo wa wafu,jicho liwe kama la kiramba sukari.

Mpende mmeo tulia ndoani ukitoka huko tuliopo nje ya mchezo tunamikwara kushinda huyo malaika.
Haya asante
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

38 Reactions
Reply
Top Bottom