Wanaume mtuvumilie tu kwakuwa tunaogopa matusi yenu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Tunacheza upatu, vikoba, vibubu ni kwa kujikwamua kiuchumi. Kuna mengine tunashindwa kuwaambia maana mkikasirika hamchagui maneno.

Unatumiwa ujumbe nyumbani nyumba inavuja, paa limechoka. Hawana msaada mwingine wanakutegemea wewe. Ukimshirikisha mumeo katika hili, wee usipompigia pasi shati lake utasikia, “shukran huna juzi tu niwebadilisha paa kwenye nyumba ya baba yako”.

Tumeamua, katika ile 5,000 ya mboga unayoacha tunakata 3,000 inaingia kwenye kibubu na inaunganishwa na upatu J’mosi. Hii 2,000 inatosha fungu la dagaa kavu na bamia. Ukirudi unakuta roast ya dagaa na juice ya maembe.

Mnafanya mengi lakini hatuwaambii kwakuwa wengine makoo yenu yako wazi mno.
 
Ni kama sijaelewa vizuri,!!! Ushakata 3000 imeenda kwenye kibubu, imebaki 2000, ambayo umenunua fungu la dagaa na bamia,

Hiyo rost dagaa na juisi ya embe jion inakuja kwa bajeti ipi Tena? Hiyo hiyo 2000?
Au ndo kuna mpemba pembeni anakuwa anasherehesha show?
 
Mkuu sio dagaa wa kopo,ni wale wa fungu 500
 
Mi ndo maana nasemaga ndoa nyingi ni heri hata zisingekuwepo. Mwanaume unapambania familia, huku nyuma mwanamke anafanya yake.
ndio maana ya uanaume na kuwa mume, sasa unataka nani apambanie familia?
 
ndio maana ya uanaume na kuwa mume, sasa unataka nani apambanie familia?
Hujaelewa point. Point sio kupambana/kutopambana. Point ni kuwa reward ya mapambano ndio sio. Hiyo inaweza kuathiri morale ya mpambanaji
 
Hujaelewa point. Point sio kupambana/kutopambana. Point ni kuwa reward ya mapambano ndio sio. Hiyo inaweza kuathiri morale ya mpambanaji
Reward ya pambano ni ndoa kudumu. Ukishajua unachopata kwa mwanaume kinakufaa iwe kwa hali au mali unamheshimu sana baba fulani.
 
hiyo 2000 inayobaki naomba itoshe samaki kama nilivyokuomba mke wangu

ukipika mboga za majani basi ujue kunibembeleza nile nione kama nakula samaki.

Kuna kitu kimoja sky

Unapoficha pesa kwa nia njema/kuweka akiba hakikisha mumeo hafahamu mpk lengo lako litimie

ila akifahamu/nikifahamu katika fekenyua fekenyua nakutana na kibobo kina hela ndani kipo juu ya kabati

asee sky hizo hela itakubidi unipe maelezo ya kutosha ulikua unaziweka kwa lengo gani,kama ni zuri?

kwann unifiche? Kwenye ndoa tuondoe siri siri jamani tutazivunja hizi ndoa kwa mambo madogo,Pesa hizi et?!
 
Back
Top Bottom