Wanaume mnapaswa kuwa na akili.

The Donchop

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
294
376
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Mimi ni mwanamke mtu mzima (wengi uwa wanachanganyikiwa na hii jina wakidhani ni mwanaume.) Nilikua na mpenzi wangu toka october 2014 na mpaka sasa.

Kwenye mapenzi kuna raha na karaha. Mwanzo tulipendana sana kiasi cha mwenzangu kutambulika kwenye ukoo wa mwenzangu pasipo sisi wenyewe kutambulishana rasmi. Pengine ni kwa sababu wakwe watarajiwa ni majirani na pia tunakutana sana kwenye shughuli za kijamii.

Mwaka 2016, tuligombana na mwenzangu. Lakini kila mmoja akiwa bado ana mapenzi na mwenzie. Lakini kila nilipojaribu kusimamia kisolvu tatizo mwenzangu ndiye aliyeleta shida. Leo siwezi kuingia kwa undani juu ya ugomvi sababu si muhimu kwa mada hii ila ni ugomvi wa kawaida sana ambao mnaweza kuelewana na maisha yakaendelea.

Mwenzangu akaamua kusikiliza watu wa nje waliompa ushauri kuwa ni bora aachane na mimi. Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuachwa na ninaempenda. Nililia. Niliomba msamaha pasipo kujua kosa. Nilihangaika sana.

Mwenzangu hakujali wala kunionea huruma. Ndio kwanza akaendelea kunituhumu hadi kwa sifa za uongo. Akaenda mbali zaidi na kusema hawezi kurudi labda amdate mama yake. Kitu cha mwisho kabisa, aliamua kunichafulia kwa ndugu zake wote na akanisingizia mambo mengi mabaya.

Sasa amerudi anaomba msamaha sana. Anataka tuoane na tusahau yote ya nyuma. Nikamwambia kwa jinsi ulivyonichafua, utawalaumu ndugu zako kuweka vipingamizi vya kila aina? Imetosha mimi nilipogombana na wewe, kesho siwezi kugombana na ndugu zako ambao tayari wameonyesha chuki kwa mambo yako ya uongo nami sipo comfortable kama mwanzo.

Kuna la kujifunza mwana jf. Unapogombana na mpenzi wako hata kama kweli ni mbaya, jifunze kumhifadhia madhaifu yake moyoni mwako. Ni utoto na ujinga sana kupeleka madhaifu ya mwenzako na kuongeza juu ili kumchafua. Wanasema mchimba kaburi anaingia mwenyewe. Sasa nimetulia na mambo yangu, mwenzangu anahangaika hajui wapi pa kushika.

Usiku mwema.
 
Unapogombana na mpenzi wako hata kama kweli ni mbaya, jifunze kumhifadhia madhaifu yake moyoni mwako. Ni utoto na ujinga sana kupeleka madhaifu ya mwenzako na kuongeza juu ili kumchafua. Wanasema mchimba kaburi anaingia mwenyewe. Sasa nimetulia na mambo yangu, mwenzangu anahangaika hajui wapi pa kushika.
Usiku mwema.
word
 
Pole sana mwaya.

Tuliza nafsi yako mwaya we muache ahangaike. Mana anajifanya ameshasahau aliyokufanyia. Akili kichwani mumy mana wanaume wana kila mbinu.

Na endapo utamkubalia jiandae kwa maumivu mengine aisee.
 
pole sana..hakika alifanya ujinga wa hali ya juu..ameshajifunza but itakuwa ni ngumu sana wewe kuolewa nae coz bdugu zake tayari wamejenga picha mbaya juu yako kwa aliyowaambia..
angalau basi asingeongea mabaya ya uongo juu yako kqa ndugu zake mmgeweza yamaliza na kurudiana.
but its too late..au kama anaweza mwambie awaite ndugu zake wote awaambie ukweli mpaka waelewe.japo ai rahisi..

mwamaume mpumbavu
 
Wanawake apa ndo ua siwaelewi,... Kama yeye ulitaka akusamee inashindikan lipi wew kumsamehe yaishe kama ulimpenda,... Uu. Uzi wa kipuuzi
 
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Mimi ni mwanamke mtu mzima (wengi uwa wanachanganyikiwa na hii jina wakidhani ni mwanaume.) Nilikua na mpenzi wangu toka october 2014 na mpaka sasa.
Kwenye mapenzi kuna raha na karaha. Mwanzo tulipendana sana kiasi cha mwenzangu kutambulika kwenye ukoo wa mwenzangu pasipo sisi wenyewe kutambulishana rasmi. Pengine ni kwa sababu wakwe watarajiwa ni majirani na pia tunakutana sana kwenye shughuli za kijamii.
Mwaka 2016, tuligombana na mwenzangu. Lakini kila mmoja akiwa bado ana mapenzi na mwenzie. Lakini kila nilipojaribu kusimamia kisolvu tatizo mwenzangu ndiye aliyeleta shida. Leo siwezi kuingia kwa undani juu ya ugomvi sababu si muhimu kwa mada hii ila ni ugomvi wa kawaida sana ambao mnaweza kuelewana na maisha yakaendelea.
Mwenzangu akaamua kusikiliza watu wa nje waliompa ushauri kuwa ni bora aachane na mimi.
Ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuachwa na ninaempenda. Nililia. Niliomba msamaha pasipo kujua kosa. Nilihangaika sana.
Mwenzangu hakujali wala kunionea huruma. Ndio kwanza akaendelea kunituhumu hadi kwa sifa za uongo. Akaenda mbali zaidi na kusema hawezi kurudi labda amdate mama yake.
Kitu cha mwisho kabisa, aliamua kunichafulia kwa ndugu zake wote na akanisingizia mambo mengi mabaya.
Sasa amerudi anaomba msamaha sana. Anataka tuoane na tusahau yote ya nyuma. Nikamwambia kwa jinsi ulivyonichafua, utawalaumu ndugu zako kuweka vipingamizi vya kila aina? Imetosha mimi nilipogombana na wewe, kesho siwezi kugombana na ndugu zako ambao tayari wameonyesha chuki kwa mambo yako ya uongo nami sipo comfortable kama mwanzo.
Kuna la kujifunza mwana jf. Unapogombana na mpenzi wako hata kama kweli ni mbaya, jifunze kumhifadhia madhaifu yake moyoni mwako. Ni utoto na ujinga sana kupeleka madhaifu ya mwenzako na kuongeza juu ili kumchafua. Wanasema mchimba kaburi anaingia mwenyewe. Sasa nimetulia na mambo yangu, mwenzangu anahangaika hajui wapi pa kushika.
Usiku mwema.

OOh thank you Ma'am,
kumbe ulikuwa unatupatia funzo kupita mkasa wa kweli.
pole kwa maswahibu yaliowahi kukupata pi.
 
Kachovya kwa wengine, na kukuta ladha ya Mchuzi ni hile hile, anajaribu kukulaghai kurudia Mchuzi wa kwenye Bakuli alilo lisogeza kwa Mguu....!!

Hakutumia BUSARA huyo mtu wako...!!

Anyway....unaweza kumsamehe tu...kwani kosa hilo kwa sasa limezoeleka...linafanywa na watu wengi kwa sasa...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio maana kunyamaza nihekima,ukiwa na hasira unaeza nena kwakuhis unamkomoa MTU,lakini hasira itaisha maneno yatabaki na mwenye hekima hupimwa kipindi cha hasira namna anavoweza kuhandle situation,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muuh mwanamke mtu mzima halafu una mpenzi!
Watu wazima wana waume na wake banah
Fanya kumsamehe
Mfunge ndoa muondokane ktk upenzi
Heshma nzuri ya watu wakubwa ni kuishi katika ndoa na sio ktk zinaaa
ASANTE KWA KUTUKUMBUSHA MAANA USHAURI WA
VIJIWENU NDO HUTUHATIBU
 
Back
Top Bottom