Wanaume mnaokaa mijini muwe mnakumbuka na kwenu mlikotoka

Mwagitho

Senior Member
Oct 11, 2013
111
38
Yamewatokea wengi na yatatutokea wengi. Mjini ulikuwa unajulikana kama tupatupa, Unaheshimika kutokana na maisha mazuri unayoishi, nyumba nzuri gari zuri, siku ukifa au ukifiwa siri zako zote zinajianika kweupe kuringa kwako kote nyumbani kwenu ulishindwa hata kujenga kibanda ona leo unaumbuka hata jeneza lako zuri walilokuchongea rafiki zako linashindwa kuingia ndani ya kajibanda ka wazazi wako, inabidi watu wabomoe mlango jeneza lipate kupita au jeneza linawekwa inje, huku mkeo analia kwa aibu atawaaimbia nini mashogaa zake leo mmeumbuka. Jamaani tukumbuke tulikotoka ipo siku tutaludi kama sio leo kesho,kama sio kwa raha basi kwa shida.
 
Ni kweli unavyosema mkuu..... !!!
Ila umenichekesha eti mkeo analia kwa aibu,umenikumbusha inshu ya bajeti
 
mh...ingawa umetumia maneno makavu shukrani,
nadhani wamekusikia
 
Plz usimseme Dr.Mvungi yaani ni majanga kijijini ndio maana hamkuona picha za home kwake zaidi ya zile za kanisani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom