Wanaume, mnaogopa kua na mwanamke mwenye maendeleo kuliko wewe?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume, mnaogopa kua na mwanamke mwenye maendeleo kuliko wewe??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by tatiana., Mar 20, 2011.

 1. t

  tatiana. Member

  #1
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kwa nini wanaume wanaogopa mwanamke mwenye uwezo??? yaweza hata isiwe sana, labda kama wake au kampita kidogo tu.. tatizo nini Jamani??
   
 2. J

  Jef Member

  #2
  Mar 20, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sio wanaume wote duniani,tena tatizo hilo ni kubwa huku afrika,hili linatokana na umajnuni wa wanawake wa kiafrika wanapokuwa na uwezo kuliko mwanaume,pia ni sababu za kisaikolojia wanawake wengi huku afrika humtegememea mwanaume sasa na yeye akipata hutaka kulipa kisasi hukataa utumwa ndio maana wanaume huwaogopa!
   
 3. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Niliwahi kuangalia show moja ya Dr. Phil, alikuwa anajadili hili suala, na kulikuwa na wanawake ambao walikuwa wamefanikiwa sana, lakini hakuna mwanaume ambaye aliwa-approach...nao walikuwa wanauliza why??

  Jibu alilotoa Dr. Phil ni kwamba, historically mwanaume amekuwa ni 'bread earner"kwa familia yake na anajiskia vizuri if he can provide for his wife/partner/family. Sasa inapotokea anakutana na mwanamke ambaye amejitosheleza kila la kitu na labda kumzidi (mfano, kazi nzuri, gari, nyumba etc), sasa ile nafasi ya kuwa bread earner inapungua, na yeye hiyo satisfaction anaikosa, kwa hiyo wengi wanaona ni bora ampate ambaye hajamzidi materially....

  Ngoja tusubiri wao wanasemaje...
   
 4. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  mi nafkiri ni suala la kila mtu kutambua his or her roles na rensopibilty kwa mwenzake na majukumu kutokana na mila na utamadyuni wenu hata kama mwanamke ni superior akifanya majukumu yake kama mke sioni tatizo, wengi wanawakwepa coz wanawake wengi ni malimbukeni na wakiwa juu wanaleta makuzi na dharau. kama mimi mke wangu ana kipato kikubwa kuliko mimi lkn bado hata kufanya vitu lazima aniconsult hata ka ni hela yake na hili limenifanya na mimi niwe muwazi kwa income yangu na nnavyotumia na lazima tujadiliane ktk matumizi
   
 5. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kuna matatizo makubwa ya kiutamaduni juu ya the head of the family, so wanaume wengi hudhani kuwa maana yake kubwa ni kuwa bread winner wa family na mke anakuwa receiver na mtu anayesubiri maelekezo ya nini cha kufanya na wapi pa kwenda. Idea ya mke kuwa out na kutengeneza fedha bado haijaingia vizuri kwa wanaume wengi so wanadhani kuwa wanawake wenye fedha hawatawaliki katika familia au kuongozeka!
  The problem of superiority for men linachangia wanaume kutafuta wanawake ambao hawakusoma! But I think as days go mambo yanabadilika kidogo na watu watatafuta tafsiri halisi ya kichwa cha nyumba ambayo haiongozwi na nguvu ya pesa bali ability ya Ubaba katika familia.
   
 6. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mada nzuri hii, acha nijipange nitarudi.
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 160
  Uoga tu wa bure sioni tatizo kwanza siku ni haki sawa kwa wote tunatoka asubuhi wote tunarudi jioni, kila mtu na gari yake ha ha wanaume msinishambulie nawatetea wala hamuogopi chochote
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,489
  Likes Received: 81,786
  Trophy Points: 280
  Ni kweli wanaume wengi wanapenda kuwa wao ndiyo mwenye income kubwa ndani ya nyumba kuliko mkewe, lakini miaka hii ya karibuni Wanawake wengi sana katika nchi nyingi duniani wametapa elimu za juu sana ambazo miaka ya nyuma ilikuwa ni nadra sana kufikia elimu ya juu kiasi hicho. Hivyo wengi wao wana vipato vikubwa kuliko hata waume zao na hii trend ya akina mama kuwa na vipato vikubwa kuliko waume zao itaendelea kwa miaka mingi na katika nchi nyingi duniani. Hii inatokana na ushahidi wa kutosha unauonyesha kwamba akina mama wamekaza buti sana katika kutafuta elimu ya juu na hata katika nchi za magharibi nyingi ambapo miaka ya nyuma % ya population kubwa katika vyuo vikuu vya nchi hizo ilikuwa ni wanaume, miaka ya karibuni kibao kimegeuka na Wanawake kuanza kuwa wengi zaidi kuliko Wanaume.
   
 9. s

  sirgeorge Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii inatokana na historia ya huko nyuma ingawaje siku hizi hali hii inapotea. Kwa hili mimi ninaweza kulitazama katika sehemu mbili;
  Kwanza, kwa tamaduni zetu (hasa Tz), mara nyingi sisi wanaume huwa tunaamini kuwa mwanamke mwenye uwezo mkubwa wa kipesa/maendeleo kukuzidi ni vigumu kumcontrol (kwa maana ya kwamba yeye mwanamke ndo atakuwa kichwa cha familia), na mbali na hilo pia wanaume wengi uamini kuwa wanawake wenye pesa huwa wana viburi ambavyo vinavyotokana na hizo pesa/maendeleo. Ukija kwa jamii inayotuzunguka, watu wakishaelewa kuwa mke anamzidi uwezo mume, hata mume akiwa anaendesha gari ambayo labda alinunua yeye watu watesema huyo jamaa anatesa na gari la mkewe (au pesa za mkewe) bila kujua undani halisi wa suala hilo. Kwa vyovyote vile hali haipendezi.
  Kwa upande wa pili hali sasa imebadilika, kuna vijana/wanaume hawaogopi tena hali hiyo kwani wanaelewa kuwa ni njia mojawapo ya kutokea kimaisha kama mke ana uwezo zaidi. Na anaona hilo ni fahari kuwa na mtu wa aina hiyo ni rahisi kumtoa kimaisha.
  Huo ndio mtazamo wangu.
  Nawasilisha.
   
 10. s

  sirgeorge Member

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye nyekundu, kuna watu walivamiwa na majambazi. Mke kamwamsha mumewe kuna wezi wameingia ndani, mume akajibu mke wangu haki sawa kwa wote, mke akagoma kamwambia wewe ndo mwanaume humu ndani kapambane na wanaume wenzako. So dena, haki sawa isiwe tu kutoka asubuhi wote na kurudi jioni kila mtu na gari yake, bali pia kwenye issue za kupambana na wezi, kuchimba makaburi na mengineyo.
   
 11. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Wengi wanaogopa kutawaliwa mke akiwa na uwezo sana
   
 12. BABA JUICE

  BABA JUICE JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 428
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  for now am real broke i wish to have a woman who is loaded.....i dont care if a woman is rich nikivutiwa nae tu nadondoka, tatizo hawa wanawake matajiri they are not attractive thus why, too much time looking for money and they forget to wear make up.:tongue:
   
 13. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mh,who told u?labda wajaruo,wanawake wenye pesa wapo weng wazur
   
Loading...