Wanaume mkiachana na wake zenu mnaachana na watoto wenu pia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanaume mkiachana na wake zenu mnaachana na watoto wenu pia?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Annina, Nov 23, 2009.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Katika vitu vinavyonisikitisha ni pamoja na hii tabia ya wanaume wanapokosana na kufikia kutengana na wake zao mara nyingi wamekuwa wakijikuta wametengana na watoto wao pia! Sina hakika ni kutokana na hasira au huwa ni jitihada za kumkomoa huyu mwanamke ambae awali alijulikana kwa majina mazuri kama honey, sweetie nk.

  Nimeshuhudia matukio mengi ya akina mama kulea watoto waliotokana na ndoa zao zilizovunjika bila msaada wa waume zao, mara nyingi akina mama hawa huwa na kipato kidogo ukilinganisha na waliokuwa waume zao ambao wameenda kuanzisha familia mpya! Kweli sielewi logic ya kuacha mke na kukataa kuwatunza na kuwapenda watoto wako...sielewi ni nini?
   
 2. JAMIETZN

  JAMIETZN Member

  #2
  Nov 23, 2009
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unauhakika ?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Ni yale ya " ukipenda boga shurti upende na ua lake"
  huenda ulikichukia inakuwa hivyohivyo...


  2
   
 4. T

  Tongue blister JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 19, 2009
  Messages: 361
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nadhani inategemea mapenzi kati ya wawili hao yaliyaanza je, Inapofikia mahala pa kuachana inamaana itakuwa mmeshindwana kinyumba.
  Hili hujenga chuki kati ya baba mzazi wa watoto na mama mzazi .
  Kwahiyo hapa nafikiri baba kuwatelekeza watoto wake ni kujaribu kumkomoa mama kitu ambacho ni hatari kabisa kwa watoto walio wazaa.

  Wanaume wa kitanzania tumekuwa na tabia mbaya sana hasa inapofikia katika maswala ya kinyumba yenye kujumuisha watoto .Wapo baadhi ya wanaume huwakimbia wapenziwao pale wapatapo ujauzito pasipo kupangilia. Mpenzi ni wako au Mtoto ni wako ya nini kumkimbia..!
   
 5. Mae

  Mae Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo sasa anapotokea baba wa kambo akawapenda watoto na mama yao na kuanza kuwatunza na kuwakuwajali ndio utajua kuwa hao watoto wana baba mzazi. Janaume litakuja kila siku kujidai "nimewamic wanangu, nataka kuwatoa watoto out, blah blah blah". Wanaume wengine wanafanya hivyo makusudi kukomoa wanawake, wanasahau wewe ukisema wa nini wenzio anasema nitawapa lini?
   
 6. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mama anapokomolewa watoto nao pia wanaumia sana,but keep in mind watoto wanakuwa hawana kosa,sasa kwa nini wapate adhabu kwa ugomvi ambao hauwahusu?
   
 7. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nimesema nimeshuhudia matukio mengi ya namna hii, wewe hujawahi kuona?
   
 8. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi sikubaliani na tabia hii, ila wakati mwingine utakuta wamama wengine huwa wananganania watoto,kwa sababu zao binafsi, labda kwa uchungu na mapenzi kwa wototo wake, au ili aweze kuhudumiwa kiuchumi etc....
  Sasa hapa ukikutana na mwanaume ambaye hajali, anawasahau wote,mama na watoto, anahamishia nguvu zote kwa small house kaazi kwelikweli...
  Lakini by the way, baba hana uhakika asilimia 100 kwamba hao ni watoto wake teh teh..
   
 9. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  ....... Watu mnapotaka kuachana hebu fikirieni watoto kwanza, maana wazazi wanapotengana hata na watoto wanakosa mwelekeo mzuri kimaisha.

  Hawa watoto watakosa elimu bora maana ndio hivyo watu mmeachana, baba hatoi matumizi kwa watoto na mama naye utakuta hana kipato cha maana, hivyo mnaawacha watoto dillema na kuwapotezea dira ya maisha.
  Watoto kulelewa na wazazi wote wawili inaleta raha na kuimarisha msingi wa mtoto.

  Vile vile serikali yetu ingekuwa na sheria kali inayomlinda mtoto, kwamba baba na mama wakiachana basi huyu mzazi baba inabidi atoe child support kwa kila mtoto, hiyo child support mzazi anakatwa moja kwa moja kutoka kwenye mapato yake.Hivyo atake asitake lazima pesa imtoke kutoka kwenye mshahara wake.
   
 10. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  wanawake wengi hupenda kubaki na watoto wao, lakini pia sheria ya nchi inasema hivyo mama abaki na mwanaye mpaka miaka saba.
   
 11. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii tabia ipo sana na inanitia hasira sana. Ni irresponsibility ya hali ya juu na inaathiri sana watoto. huwa nasikia kulia kila nikiona watoto wanavyorandaranda mitaani na kuomba pesa as if hakuna mwanaume aliyekuwa responsible kwa wao kuwa hapa duniani. inaumiza kwa kweli.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  mbona ni swala ambalo liko waza kabisa halina haja ya kuuliza ..kama wewe hujawahi kushuhudia basi fanya uchunguzi
   
 13. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #13
  Nov 24, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  na mbaya zaidi ni pale atakapokutana na mwanamke mwanauchumi mwenye uwezo wa kummmiliki ipasavyo
  Inakuwa nipotezee kabisa
   
 14. bht

  bht JF-Expert Member

  #14
  Nov 24, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  hata baada ya miaka saba, do I real want my baby to go and be raised na mke wa mtalaka wangu?

  nina uhakika gani atapata malezi bora na yanayostahili??
   
 15. bht

  bht JF-Expert Member

  #15
  Nov 24, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  weee unabisha sasa? jirani yangu mumewe alitopea kwa janmke la kiswahili akavunja ndoa , sasa mama hawezi kumpeleke shulebinti yake ( inatia uchungu)
  tulijaribu ku-negotiate matunzo ya mtoto baba akawa kichwa ngumu sasa tumemsogeza kw apilato aamue mwenyewe!!!

  kwa nini watoto wateseke kwa makosa ya wazazi? so unfair
   
 16. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #16
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa unabishana na Pilato?? Labda huyo baba asiamue tu kumchukua!!
   
 17. bht

  bht JF-Expert Member

  #17
  Nov 24, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  ntamu-incapacitate huyo baba ili nibaki na mwanangu
   
 18. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #18
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ....Si kweli. Wanawake wengi wanapogombana na waume zao hukimbilia kubeba watoto wakiamini mwanaume lazima atapeleka pesa ya matumizi ya watoto na yeye anakulapo humo humo. Mwanaume asipopeleka pesa ya matumizi utasikia mwanamke anaaza kulia lia kuwa mwanaume ametelekeza mtoto/watoto hatoi pesa ya matunzo na ndio maana wanaume wengi huamua kula kona. Nina ndugu yangu alipatwa na mkasa wa aina hiyo mama anataka kwa mwezi kila mtoto apewe pesa ya matumizi 100,000 na wana watoto watatu cha kushangaza yeye mama anajitoa kwenye suala la matunzo as if watoto si wake! Why?? Jeuri za wanawake ndio chanzo cha hayo yote...
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Nov 24, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna mtu na mkewe, wakiwa na watoto 5 waligombana. Mke akakimbilia kusema kuwa anarudi kwa mama yake.
  Bwana akapiga hesabu ya fasta akaona itakuwa shida na watoto. Akaanza kupaki nguo zake naye, alipoulizwa na mkewe, kunani, akasema naye anaenda kwa mama yake, na akaagiza NA WATOTO NAO WAENDE KWA MAMA YAO.
  Mwanamke akaishiwa nguvu, na kumwambia bwanake kuwa...BASI YAMEISHA, WAKARUDIA MAISHA YA KAWAIDA!
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  Nov 24, 2009
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  1. Inategemea tatizo ni nini/chanzo cha ndoa kuvunjika e.g baba kagundua watoto si wake je atawapenda baada ya ndoa kuvunjika?
  2. Malezi ya hao watoto, labda walikuwa karibu sana na mama na lazima watapenda kuishi na mama yao.
  3.Umri wa hao watoto ukoje? kama ni wachanga lazima wabaki na mama yao hata sheria haitakubali baba awalee watoto.
   
Loading...