Wanaume mbona mnakaa 'kibwege' sana? Huzuni yangu imeyeyuka ghafla

Zee Korofi

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,612
1,410
Hakuna cha salamu, siku takribani saba nimekuwa nikisikitika mno kwa mambo kadha wa kadha.

Leo moyo umepiga 'paaa' baada ya kuangalia 'list' ya majina ya wanafunzi kumi bora kitaifa waliofanya vizuri zaidi katika mtihani wa Taifa wa kidato cha sita mwaka 2022.

wa kwanza na wa pili ambao wote ni 'PCB' ni wadada. Wawili wa mwisho katika hao kumi bora ni wakaka.

Yaani wadada wanakuja juu midume chali. Hivi inakuwaje hii? Ndiyo kusema mwanamke si dhaifu kama ilivyozoeleka?

Wanaume wameniangusha sana, na inauma mno. Leo sili chakula, yaani sijui ndiyo tuseme wanaume wanazidi kupungua au? Yaani bora ingekuwa mara moja moja, ila kila mwaka wanawake wanaongoza, na wanazidi kuja juu.

Hali hii haitoishia kwenye elimu tu msipoangalia, mpaka kwenye sekta zingine itafika. Tujadili hili tuone shida ni nini? Wapi tunakwama/madogo wamekwama? Nini kifanyike?

Kuanzia leo kwa muda usiojulikana, sili nyama na sitonyoa nywele wala kupaka mafuta, kucha sitokata. Hii ni adhabu niliyojipa kwa niaba ya magoi goi wote wa kiume.
 
Vitu vya kuongelea ni vingi mno na vyenye tija, na ndiyo maana nyuzi pia zinakuwa nyingi, na hapa naona bado hazitoshi, nina mengi sana ya kuandika.
Pumzika inatosha sasa..unakuwa Kama aslay enzi zile anatoa nyimbo back to back!!

Alafu mkuu;hivi wewe,mpwayungu village na man bizness mna undugu? Hao wawili niliowaongeza wanashusha nyuzi back to back alafu nyuzi zao chai tupu km zako 😅😅
 
Na mimi nmekasirika, inakuweje wadada waongoze?! Haiwezekan! Vijana mlishindwa kuwavuruga hao wadada? Sisi enzi zetu wadada walikuwa hawashiki hata kumi bora, nyie mmeshindwa wapi?
 
Pumzika inatosha sasa..unakuwa Kama aslay enzi zile anatoa nyimbo back to back!!

Alafu mkuu;hivi wewe,mpwayungu village na man bizness mna undugu? Hao wawili niliowaongeza wanashusha nyuzi back to back alafu nyuzi zao chai tupu km zako
Ninawafahamu, ila sina undugu nao kabisa. Mimi siyo muumini wa kitu kinachoitwa chai. Nashusha nyuzi za kweli na kama ukizipima kwa akili utagundua hilo!
 
Na mimi nmekasirika, inakuweje wadada waongoze?! Haiwezekan! Vijana mlishindwa kuwavuruga hao wadada? Sisi enzi zetu wadada walikuwa hawashiki hata kumi bora, nyie mmeshindwa wapi?
Nazidi kuumia, please usizidi kunilasirisha, nisije kuongeza adhabu niliyojipa.
 
Pumzika inatosha sasa..unakuwa Kama aslay enzi zile anatoa nyimbo back to back!!

Alafu mkuu;hivi wewe,mpwayungu village na man bizness mna undugu? Hao wawili niliowaongeza wanashusha nyuzi back to back alafu nyuzi zao chai tupu km zako
Pia nakumegee siri, jaribu kuchunguza hata miandiko na mitiririko yake(nukta, matumizi ya herufi, aya n.k), utagundua tupo tofauti mno.
 
Wanawake hata waongoze nini lakin kwenye inshu ya pesa watatusubiri tu

Hayo matokeo inawezekana ikawa ni siasa siunajua tena toka wizara ilipokaliwa na mwanamke ndo mambo yakaanza kuonekana hv
 
Wanawake hata waongoze nini lakin kwenye inshu ya pesa watatusubiri tu

Hayo matokeo inawezekana ikawa ni siasa siunajua tena toka wizara ilipokaliwa na mwanamke ndo mambo yakaanza kuonekana hv
Hata kama kaka, ila bora ingekuwa mara moja moja, ila karibu kila mwaka wanawake wanakuja juu tu. Hii si ishara nzuri.
 
Wanaume wamegundua kwa sasa hakuna cha maana kwenye elimu ya makaratasi wanataka elimu ya vitendo, acha wadada wajivinjari na matokeo ya kuongoza.
 
Na mimi nmekasirika, inakuweje wadada waongoze?! Haiwezekan! Vijana mlishindwa kuwavuruga hao wadada? Sisi enzi zetu wadada walikuwa hawashiki hata kumi bora, nyie mmeshindwa wapi?
Kazi za mtoto wa kike siku hizi zinafanywa na wadada wa kazi hivyo inampa fursa msichana kupasua anga, hapo zamani majukumu yalimvunja mgongo binti.
 
Back
Top Bottom