Wanaume: Kwani kuna ubaya gani mkeo akijua kuendesha gari?

Huyo jamaa ni mchoyo a mbinafsi... Bora waliuze wagawne pesa kila mtu anunue ki Vitz chake, wasichoshane!
 
Aisee gari moja nyumbani ni shida na hasa pale wote mmejifunza wakati mmoja na wote mna-interest za kuendesha gari, aaah lazima mgombane now and then inapokuaj swala la mitoko.

  • Gari uliyoinunua (ya kwanza) tena kwa kujichanga sana, huwa inauma sana hata ukiipitisha tu kwenye majani. Maana unahisi itaharibika hapo hapo na ungependa uione ikiwa mpya siku zote maana uhakika wa kupata gari nyingine hivi karibuni sio rahisi.
  • Inapokuja swala la service ( zile za kawaida ) baba lazima atahusika, kwa ufupi, gari ikiharibika baba utatakiwa kutengeneza. Hivyo anakuwa mchungu sana kuitoa gari kwa mama.
  • Pia baba anaamini anaweza kuendesha vizuri kuliko mama hivyo gari kukwaruza na kugonga itakuwa nadra sana, tukumbuke kuwa kama wamejifunza pamoja kujua dereva mzuri itabidi kiwango cha kuendesha hiyo gari iwe sawa ili kumtambua ( hapa baba atataka kudominate).
  • Na kama baba anajua mke wake ni mtu wa majigambo na yeye hapendi hizo tabia, atamwekea ngumu kwani anaamini anataka kuendesha gari kuonesha mashoga zake kuwa nae anajua kuendesha gari.
NB: Tuendeshe wote ( baba na mama) mara kwa mara ili tupate uzoefu sawa. Pia kujua kuendesha wote ni faida kwa familia.
Ila hii tabia ya kushika ufunguo wa gari mkononi na kuwa unauzungusha zungusha ni ushamba, mifuko ya suruali mnayo na pochi ( wadada) mnazo kwa nini msiweke, au ni nzito sana zikikaa mifukoni na kwenye pochi?. Remainder: Hata mimi ninalo gari la bei ndogo ila linamaliza shida zangu.
 
Back
Top Bottom