Wanaume kuweni makini, Wanawake wengine ni gundu na mikosi kwenye maisha yako

Unaweza kuta wewe ndio uko na gundu na mikosi, ukahisi mwenzio ndio tatizo kumbe wewe ndio unakwamisha mambo yake.
 
Tatizo letu waafrika tunapenda sana kutafuta "mchawi" pindi mambo yanapoenda ndivyo sivyo. Mafanikio ya mtu yanategemea na mtu mwenyewe, mipango aliyojiwekea, jinsi anavyoitekeleza, channel aliyo nayo na discipline yake kiujumla.. Wapo watu wanabadili wanawake kila siku na mambo ndio kwaanza yanazidi kuwanyookea, wewe kaa hapo ukisema kuna wanawake wana gundu usifanye kazi ukatafuta pesa.

Ina maana watu wenye mafanikio wao hawajawahi kukutana na huyo mwanamke mwenye gundu, wao hua wanakutana na malaika tuu? Fanya kazi acha visingizio!
 
Mi naona ni imani tu, hakuna uhusiano wowote kati ya mwanamke ulie nae na mafanikio. Unaweza usiwe na mwanamke kabisa na bado mambo yakiamua kuyumba yanayumba tu.

Ujatembea wewe au inaonekana wewe bado unalellewa kwenu
 
Laana na baraka za mtu zimo kwenye ulimi wake.Huwezi ukawa na ulimi mchafu ukawa na baraka
 
Back
Top Bottom