Wanaume: Kosa dogo linaweza kutufanya tusipendwe na watoto wetu hapo baadaye. Mwanangu wa miaka mitano amenistua leo

Rasterman

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
33,905
44,011
Habari za Ijumaa wikenda wapenzi wasomaji wa MMU.

Kwanza napenda nitoe maelezo kuhusu tabia yangu ya kimaisha.

Declaration; Mimi nimeoa mke wangu Mama wa nyumbani. Nimefanya hivi kwa kuwa napenda sana starehe. Yaani napenda ninaporudi nyumbani nikute nyumba imesafishwa, inang'aa, chakula kimeandaliwa cha kifalme. Chumba ninacholala kimewekwa maridadi kama vile Mwana wa Mfalme Mohamed Bin Salma wa Saudia anaingia leo. Hivyo kwa tabia zangu hizi na zile zingine za kiutu uzima ambazo sote tunazifahamu nilipendelea sana niwe na mke asiyechoshwa sana na mihangaiko ya hapa na pale. Napenda kuona watoto wasafi muda wote walishwe vizuri na kumwagiwa upendo na mama yao muda wote.

Baada ya maamuzi yangu haya mimi nikajipa wajibu 100% kutafuta pesa, kuwaza vitu vikubwa kama vile kusaka madaraka kwa kuchukua nchi kikatiba na kidemokrasia na amani, kumiliki njia kuu na miundo mikubwa ya kiuchumi, kununua magari, ndege na kwenda masoko makubwa ya kibiashara kama Tokyo, Yokohama, Gwanzhou na Shenghanz n.k

Hakuna hata siku moja utanikuta nanunua fenicha za ndani, vyombo, nguo wala vifaa vya umeme. Hata Ada hata siku moja sijawahi kwenda shule za watoto wangu. Nyumba na viwanja sijawahi kutafuta. Kuanzia hatua ya ununuzi, ujenzi hadi kukamilika kwake yote anasimamia Mama watoto. Kazi yangu ni kukamilisha michakato ya hatimiliki na taratibu zingine za kiserikali na kisheria.

Nguo za watoto hata namba za viatu sizijui.

Ofcourse nikitoka kazini au safarini natumia muda mwingi kukaa na wanangu na mke wangu.

Baada ya kueleza tabia hizi ambazo japo sio mbaya lakini zinaweza kunicost. Nimeelezea ili wale wenye tabia kama zangu tushtuke. Tubadilike for good reason.

Leo baada ya kutoka kazini nimeshaoga na kula chakula kizuri sasa niko na pitia habari za hapa na pale kwenye account mbali mbali( Tundu Lissu account). Of course he is my role model. Tuache siasa.

Mwanangu huyu wa kiume miaka 5 akanijia nilipo. Akaniambia Baba naomba hela nikanunue glori( ball za kuchezea watoto). Nikamjibu sina pesa. Nakwepa kumpa pesa kila wakati asije kuwa na tabia mbaya.

Akanijibu Wewe Baba hujanipa pesa siku nyingi naomba leo pesa sh miatano nikanunue glori na bofu(maputo ).

Akaendelea kulalamika kuwa Mama ananipa pesa lakini wewe nikikuomba hunipi.

Likanijia wazo kichwani palepale. Nikawaza nikatafakari. Inamaana huyu mtoto anaona kabisa mimi simjali? Hajui hata hizo miatano anazopewa na Mama zinatoka kwangu?

Inamaana kuna siku nikizeeka nikawa sina nguvu hawa watoto watampenda mama yao na kuniacha mimi kwa kuamini kuwa sikuwa nawathamini enzi za ujana wangu?. Sasa itakuwaje? nitajiteteaje niaminike.

Ndipo nikasogea pembeni kwenye droo nikachukua sarafu ya jero nikampa akashukuru akatoka nje kwenda kucheza na watoto wenziwe.

Ni hayo tu.

Wanaume wakati tunawaza mambo makubwa kama kushika nchi, kumiliki viwanda vya Uraniam na nyukilia tusisahau mambo madogo madogo kwenye familia zetu yasije kutucost badae.

Na nyie wake zetu basi muwe mnatuwakiliasha wambie hizo pesa na mali wanazoona watoto nyumbani kuwa zimetokana na nguvu zetu sote. Tusije tukatengwa huko mbeleni.

Yangu ni hayo tu Nawatakieni Jumaa Kareem.

Asalaam Aleykum
 
Jambo la kuzingatia mwanaume yeyote ni kuhakikisha unatunza pesa ztakazo kutunza uzeen,hakksha hukos hela mpaka utakapo kufa panda hata miti iwe kama akiba au fuga mifugo za kutosha kama akiba.

Maana kuna kutengwa uzeen,wanao na mama yao wakawa mbali na wewe
 
Jambo la kuzingatia mwanaume yeyote ni kuhakikisha unatunza pesa ztakazo kutunza uzeen,hakksha hukos hela mpaka utakapo kufa panda hata miti iwe kama akiba au fuga mifugo za kutosha kama akiba.

Maana kuna kutengwa uzeen,wanao na mama yao wakawa mbali na wewe
Ili kuepuka hili tujitahidi kufuta dosari zilizopo
 
Siku moja moja mpe mkeo pesa mbele ya watoto wako itawasaidia kujua wewe ndio unatoa hizo pesa mama aweza waambia lakini wakiona kwa macho itaweza saidia zaidi
Kweli hii ni mbinu moja wapo. Asante. Wanaume tujifunze
 
KAMA UNA MPANGO WA WATOTO WAKO WAJE KUKUKUMBUKA BAADAYE SAWA....ILA TIMIZA WAJIBU WAKO ...wape wanachohitaji..WATOTO WAKIMPENDA MAMA YAO KWASABABU HIYO SAWA..ILA KUMBUKA UKWELI WEWE NDIO UMEWALEA...cha msingi ninachokushauri kuwa na akiba yako akiba ya kukufanya usikose BIA NA NYAMA CHOMA mpaka unakufa
 
Mimi nafikiri ni ubinafsi tu wa baadhi yetu wanawake, unajua fika kabisa “BABA” anapambana mchana na usiku ili familia yake iwe na furaha kwa kupata kila inachohitaji inagharimu nini kuwaeleza watoto kuwa “BABA” haonekani nyumbani muda mwingi kwasababu anawatafutia pesa ya ubwabwa na ada ya shule!!!

Ingawa pia wazazi wa kiumeni muwe mnatenga muda angalau siku 2 tatu za kukaa nyumbani na familia.
 
Jambo la kuzingatia mwanaume yeyote ni kuhakikisha unatunza pesa ztakazo kutunza uzeen,hakksha hukos hela mpaka utakapo kufa panda hata miti iwe kama akiba au fuga mifugo za kutosha kama akiba.

Maana kuna kutengwa uzeen,wanao na mama yao wakawa mbali na wewe
Pweti
 
Back
Top Bottom