Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 864
Jana nilikuwa napita karibu na bar fulani,nikasikia wimbo wa Jide wa Wanaume kama mabinti ukanikumbusha mbali.Nikatafakari sana na baadaye nikaja kugundua kuwa Lady Jaydee ameimba kitu cha ukweli mtupu.Mapenzi ya siku hizi yameshuka sana,si wanaume si wanawake hatuoi wala kuolewa bila kuweka vigezo kwa yule unayetaka kuwa naye.Wanaume wa siku hizi utasikia mimi mchumba wangu au mke wangu lazima awe na kazi,elimu kuanzia kidato cha sita na kuendelea na vigezo vingien ,wengine wanaangalia hata uwezo wa wazazi wako.Jamni haya mambo yametokea wapi?Mbona hayakuwepo zamani na wazazi au babu zetu walifaidi maisha ya ndoa tena kuliko sasa kila kukicha watu wanalia ooh ndoa,imenichosha n.kZaidi ya hayo ndoa nyingi siku hizi zinavunjika uklinganisha na miaka ya zamani.Hivi ninyi wanawake na wanaume mnaoweka vigezo je mnaoa ama kuolewa na vigezo au mtu?je vigezo hivi tunavyoweka vinongeza nini katika maisha ya ndoa?na je vingekuwa na maana mbona ndoa za siku hizi nyingi zao hazina mvuto?kila siku kufumaniana,kama sio laivu basi kwenye simu n.k.Jamani hebu tuache mapenzi yachukue mkondo wake,tusiilazimishe mioyo yetu ijifunze kupenda kwasababu tu ya kuangalia vigezo,tukumbuke mioyo huwa haijifunzi badala yake ina penda yenyewe kwa kuamua yenyewe.