Wanaume: Je unaweza kuruhusu mkeo kwenda kumuona daktari wa magonjwa ya kike ambaye ni rafiki yako?

Haina complications kabisa, unampeleka tu. Kama missus atahitaji uchunguzi/vipimo, jamaa atamuelekeza kwa msaidizi wake na yeye atashauri kuhusu matibabu tu. Same thing ingekuwa mwenye shida ni dada, mama au ndugu yeyote wa karibu.
 
View attachment 602491

Inatokea mkeo au mpenzi wako anasumbuliwa na maradhi ambayo anatakiwa kumuona mtaalamu wa maradhi ya kike. Halafu kwa bahati nzuri unaye rafiki yako ambaye ni mtaalamu wa fani hiyo na anafanya kazi kwenye hospitali kubwa ya serikali. Je unaweza kuruhusu mkeo kwenda kumuona rafiki yako huyo daktari wa magonjwa ya kike kwa ajili ya vipimo na matibabu?

Hivi unaweza kumpeleka Mbuzi akacheze na Chatu mwenye njaa kweli Mkuu?
 
Panapo uugonjwa mkuu sioni tatizo la yeye kutibiwa. Hali ya ugonjwa ikizidi utamwita mwenyewe tu huyo dakitari amhudumie..
 
Hamna ubaya wowote,

Kwanza mtu anapokuwa anasumbuliwa na malazi , aibu huwa haina nafasi, na katika hali ya kawaida jinsi wanavyokuwaga huwezi tamani kabisa,

From the first time tulipokuwa tunafundishwa wodini jinsi ya kuzalisha mama mjamzito huku tukishuhudia, nikiri tu kwamba nilipoteza hisia za kugegeda kwa wiki kadhaa,
Ndio maana mume haruhusiwi kuingia ktk chumba cha kujifungua pindi mkewe anapo jifungua.

Wakati huo tukiwa wanafunzi mke wa daktari flani alikuwa anajifungua , wakati huo tukiwa clinical area tulihudhuria pasipo kuwekewa kikwazo chochote sababu naye ni mgonjwa kama wagonjwa wengine,

Jambo ambalo mtumishi wa afya hatakiwi kufanya ni kuwa msiri na kulinda privacy ya mgonjwa,

Pia mgonjwa anahaki ya kumkataa daktari endapo atahisi privacy haitakuwepo, but kwa hali ya kawaida hamna mgonjwa anayeletaga ujuaji mbele ya daktari,

Mkeo akiugua kisawasawa utampeleka hata kwa ex wake ambaye ni daktari kwa moyo mmoja,

Believe me
Mkuu rekebisha kidogo hiyo aya ya tatu tok mwisho, hilo neno 'hatakiwi' sidhani kama ni sahihi.
 
Back
Top Bottom