Wanaume: Je unaweza kuruhusu mkeo kwenda kumuona daktari wa magonjwa ya kike ambaye ni rafiki yako?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
upload_2017-10-5_11-9-55.png

Inatokea mkeo au mpenzi wako anasumbuliwa na maradhi ambayo anatakiwa kumuona mtaalamu wa maradhi ya kike. Halafu kwa bahati nzuri unaye rafiki yako ambaye ni mtaalamu wa fani hiyo na anafanya kazi kwenye hospitali kubwa ya serikali. Je unaweza kuruhusu mkeo kwenda kumuona rafiki yako huyo daktari wa magonjwa ya kike kwa ajili ya vipimo na matibabu?
 
View attachment 602491

Simuruhusu hata kidogo, atatibiwa na wale ambao sio rafiki zangu
 
Hapo kazi ipo kwakweli
Ila niliwahi sikia Kisa kimoja mdada aliolewa na baba yake ni daktari wa kuzalisha sasa akabeba mimba ya kwanZa wakati anajifungua hospital ile baba yake anafanya kazi mtoto akafa akabeba mimba ya pili pia mtoto akafa wakati anajifungua ya Tatu baba akaona ujinga akaingia labour akamzalisha mwanae na mtoto akatoka hai
Sasa naona kama ungonjwa ni mkubwa na una risk maisha ya umpendae nadhani hutojali Ila karoho katapwita kidogo
 
Mmmmh
Mwenyewe ndo nitakuwa na shida lakini hapana!!! Nikikutana nae daah, siendi kwa kweli
 
Back
Top Bottom