Wanaume: Je mnakipa tafsiri gani kitendo cha mwanamke kukubali kujamiiana mapema...?

sipendi demu wa kunizungushazungusha, kwamngu mie, date ya kwanza story, date ya pili kuomba mchezo, tukipanga appointment ya kwenda ku do akinizingua tu na mimi nakula kona
 
Mkuu Mtambuzi nakubaliana na maelezo yako kwa 100%. Unajua dada zetu na sio dada zetu tu bali na vijana wote pia kwa ujumla wanapaswa kuwa makini wanapoanzisha uhusiano wa kimapenzi. Watambue kuwa kila mtu huwa ana sababu au madhumuni ya kuanzisha uhusiano huo. Hivyo hata siku moja wasije wakadhani na kuamini kuwa wazo au dhumuni ulilonalo la kuanzisha uhusiano huo ndilo hilo hilo ambalo analo mwenzako. Ukifanya hivyo utakuwa umekosea sana na hapa ndio vijana wengi tunapoangukia pua.

Kutambua sababu au dhumuni la mpenzi wako kuanzisha uhusiano na wewe ni hatua muhimu sana ambayo vijana wengi huwa tunaipuuza na matokeo yake tunaishia kulaumu kwamba wanaume ni wabaya au wanawake ni wabaya wakati kosa umelifanya mwenyewe.

Mkuu Young Master, umedadavua vizuri sana. Ni kweli wengi wetu huwa tunajiweka kwenye viatu vya wapenzi wetu tukidhani au kuwa na hisia za nikifanya hivi au nikikataa kukutana nae kimwili mapema hueanda atanikataa. Ni vizuri wapenzi kuelezana mapema kabisa kuwa tuko kwenye uhusiano huu kwa sababu kadhaa. Hata ikiwa ni ngono pia ni vizuri kukubalia tangu awali ili pale mmojawapo anapohitaji usije ukamshangaa au kuanza kumpiga chenga kwa coz pengine matarajio yako hayakuwa ngono ya mapema!
 
Mimi nilikutana na dada mmoja hivi ambaye wakati tunakutana mimi nilikuwa niko ''single'', nikimaanisha nilikuwa nimeachana na mpenzi wangu wa muda mrefu.

Sababu mpenzi wangu nilikuwa namuona kama malaika etc, nikaamua kudate na kichaa!! Ndiye nilikutana nae dada ambaye alikuwa na historia ya kufanya ufuska sana alivyokuwa chuoni kwao. Nilikuwa namsikia tu lakini siku namuona nilivutiwa nae, nikampenda.

Yule dada yeye pombe, outings, na marafiki zake wa kike na wa kiume kwenye BBM, facebook na wengineo kibao simu kila saa.

Siku tunakutana tukapiga bia mbili tatu, nikachukua namba ya simu tukaanza kuchat baadae. Tukaanza ku flirt kwenye simu.

Akaanza kunitumia picha zake lakini kila akijiremba nikawa namponda, nataka awe natural, basi akaacha kujipaka ma lip stick na akasuka na kuwa ananitumia picha. Nadhani hii ilimfanya anione niko tofauti sana. Akipiga picha na mawigi namponda. Akayaacha.

Siku ya pili ya tatu, tukaenda hotelini. Hotelini tukakaa kwa nje pale tunagonga bia na wine kidogo then nikachukua room.

Nikambembeleza bembeleza, tukaingia room. Romance kidogo hapa na pale nguo zikavuliwa, akawa ameshalegea. Kidume nikaingia bila zana, tukalala usiku kucha.

Sikuwa nahofia UKIMWI, sikuwa nahofia MIMBA, kiukweli nahisi nilimpenda. Sasa kila tukipiga breki bibie anazungumzia kupima HIV kesho yake, mimi nikawa namwambia sina tatizo.(Bahati nzuri sikuwa na tabia ya kulala na wanawake wengine zaidi ya mpenzi wangu tu).

Kesho yake tukachukuana mpaka pale hospitali, dada wa watu anatetemeka sijawahi kuona. Alidhani nitakataa. Tuko pale tumechukuliwa damu anachat na rafiki zake kuwa nimekubali na yuko pale anatetemeka. Majibu yakatoka wote Negative.

Dada akabadilika, akanipenda, akapunguza pombe, akapunguza marafiki wa kiume, akapunguza marafiki wa kike wenye ushawishi mbaya, akaanza kuwa responsible mno.

Baada ya miezi kadhaa tukaenda tena kupima na ikawa hivyo hivyo.

Bahati mbaya tuliachana kwa sababu zilizokuwa nje wa uwezo wangu(mimi niliamua) lakini kujibu maswali yako,;;;

1. Je ni malaya? Kama umalaya unamaanisha kujiuza sio. Kama umalaya unamaanisha kupenda kufanya mapenzi na wanaume wengi sio. Kama umalaya unamaanisha kupenda kufanya mapenzi na mtu mmoja anayemuamini,,, NDIO

2. Je, anakupenda sana? NDIO

3. Je kuna kitu kimemvutia kwako na anataka kukunasa haraka? Kuninasa sidhani

4. Anajiamini na amekuamini na hana cha kupoteza hata ukimuacha, HAPANA

5. Ana matarajio makubwa juu yako na anaamini uhusiano wenu utafika mbali kwa kuwa kuna mambo mengi mnaendana
.NDIO
 
Dah! Mpwa taratibu, mwalimu wetu mmoja?

Kwa karne hii, mwanamke msumbufu hana nafasi kwangu.

Kwa karne hii, mwanamke asiye msumbufu SI lazima awe malaya

Kwa karne hii mwanamke msumbufu SI lazima ASIWE malaya

Kwa karne hii kufanya ngono kwa wakati gani ni UAMUZI na siyo KUFIKIRIA au KUSUMBUA.

Mwanamke atakayengonoka nami baada ya kukutana naye siku moja hana tofauti na nliyesumbuana naye kwa miezi sita. Wote ni walewale tu. Mwalimu wao ni mmoja.
 
kwa mtizamo wangu ni kuwa kuna wanawake wengi ambao ambao wanatoa nanihii cku ya kwanza wako honest zaidi kuliko wanaopiga danadana ili waonekane credible, kwa sababu jamii na tamaduni nyingi zinaelekeza kuwa eti kujiachia kirahisi ni umalaya.

Nakubaliana na wewe.....!
 
iyo inasababisha matatizo baadae cos ,wanawake wengine hufanya hivyo kwa ajili ya kumuonesha man jinsi anavyo mpenda, but inaleta madhara baadae hasa maisha tunayo enda nayo sasa hivi ,cos most of time girl utapigwa na chini ,una bakia kuumia bure , me nahisi kukubali kufanya mapenz kwa muda mchache kujuana na mweza wako n wrong na inaleta chuki tu na maumivu baadae hasa kwa wanawake cos wao ndio wanaopenda deeply kuliko man
 
black-couple-in-bed.jpg


Inawezekana ikawa ni kwenye mtoko wa kwanza, kutokana na mazingira kuruhusu na kuwa muafaka kwenu mkajikuta tu jambo hilo limefanyia bila nyie kujijua, au inawezekana baada ya mitoko miwili mkajikuta mmefikia hatua ya kujamiiana.

Hebu fungukeni, mnamchukulia vipi mwanamke anayekubali kujamiiana muda mfupi tu baada ya kujuana?

cheating-husband-450a121208-1258748685-378x394.jpg


1. Je ni malaya?

2. Je, anakupenda sana?

3. Je kuna kitu kimemvutia kwako na anataka kukunasa haraka?

4. Anajiamini na amekuamini na hana cha kupoteza hata ukimuacha,

5. Ana matarajio makubwa juu yako na anaamini uhusiano wenu utafika mbali kwa kuwa kuna mambo mengi mnaendana.

Hakuna jibu sahihi qani maisha ni fulu mitego na maajabu!
 
ukitaka ngono mara tu mnapokutana nenda mitaani,kwa wanaojiuza kupata fedha.
Swali la kujiuliza nyie wadau vidume hi hili, je ungekutana na mwanamke, akwambie amevutiwa na wewe na anapenda ufanye naye mapenzi siku hiyo mliyokutana, je muitikio wako ungekuwaje?
 
black-couple-in-bed.jpg


Inawezekana ikawa ni kwenye mtoko wa kwanza, kutokana na mazingira kuruhusu na kuwa muafaka kwenu mkajikuta tu jambo hilo limefanyia bila nyie kujijua, au inawezekana baada ya mitoko miwili mkajikuta mmefikia hatua ya kujamiiana.

Hebu fungukeni, mnamchukulia vipi mwanamke anayekubali kujamiiana muda mfupi tu baada ya kujuana?

cheating-husband-450a121208-1258748685-378x394.jpg


1. Je ni malaya?

2. Je, anakupenda sana?

3. Je kuna kitu kimemvutia kwako na anataka kukunasa haraka?

4. Anajiamini na amekuamini na hana cha kupoteza hata ukimuacha,

5. Ana matarajio makubwa juu yako na anaamini uhusiano wenu utafika mbali kwa kuwa kuna mambo mengi mnaendana.

5. Ana matarajio makubwa juu yako na
anaamini uhusiano wenu utafika mbali
kwa kuwa kuna mambo mengi
mnaendana.
 
Back
Top Bottom