Wanaume hii siri nawapa; zama zimebadilika, Tusioe!

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,305
8,655
Zamani suala la kuoa lilikuwa miongoni mwa suala la muhimu sana katika maisha ya mwanaume.. pamoja na kwamba mwanaume hufanya mipango na projections za maisha yake lakini hakuna swala lililokuwa zito mbele yake kama Kuoa.. Huo ndio ukweli!

zama hizo wanawake waliogopa wanaume na kuwaheshimu.. hili liliwapa wanaume hamasa ya kuoa..kwa sababu alijua anaenda kuheshimika tofauti na sasa 50/50
Je kwa miaka hii bado wanaume tunatakiwa tuoe? itakuwa miongoni mwa maoteo mabovu ambayo utafanya.. Niamini mimi kila mtu anayeoa/kuolewa anaamini ndoa itadumu milele.. lakini ukweli ndio uko hivyo?? Sio kweli.. uwezekano wa ndoa kuvunjika ni mkubwa kuliko kudumu!

Hizi ni zama ambazo mwanaume hana nguvu kama zama zilizopita.. zama ambazo sheria imempa nguvu mwanamke.. Jamii kwa sasa imeandaa aina ya wanawake ambao kwa bahati mbaya hawajaandaliwa wanaume kwa ajili ya kucopy nao (Women empowerment).
Hizi ni zama ambazo Jane ameolewa na Juma ila hisia zake za kimapenzi zipo kwa Hamisi wakati Hamisi hisia zake zipo kwa Aisha(Mduara Huendelea).. kwa maana hii Jane ni Rahisi kumsaliti Juma!
Zama ambazo mwanamke anaolewa kwa kuangalia usalama wa maisha yake kwa suala la uchumi.. Hawaangalii Upendo tena!

Zama ambazo wanawake wana haki sawa na mwanaume, zama ambazo utandawazi(Mitandao ya kijamii) umekuwa na nafasi kubwa katika maisha ya mwanamke kuliko mwenzi wake!.. Unadhani aina hii ya wanawake inafaa kuoa? Hapana!

Hizi ni zama ambazo mwanamke anajua mumewe anakufa kabla yake.. zama ambazo mwanamke mtoto anavyokua mapenzi ndivyo yanavyopungua kwa Mume..(Mtoto/watoto wakikua mume hauna thamani)

Zama ambazo mwanaume ukiteleza kidogo utapelekwa kwenye madawati ya kutosha.. zamani haya hayakuwepo ndio maana ndoa ilikuwa muhimu!

Mwishowe niwasihi ndugu zangu wanaume.. kama una ishu yako ya Msingi unaifanya Komaa nayo.. Muda wako mwingi invest kwenye Career yako.. Hutojutia na pia hutokosa wanawake wa kuhook nao!

Niwape Mifano Michache kuna watu walipata mafanikio makubwa bila mke.. Mfano Ratan Tata, Keanu Reeves, Henry David Thoreau,Nikola Tesla na wengine wengi.. na siri hii nawapa..Kuwa katika Mapenzi/Mahusiano kwa Kiasi kikubwa kunapunguza Ufanisi!

Mwisho wa siku kila mtu atabeba msalaba wake lakini sisi wa kusema wacha tuseme..(Ukweli hutuweka Huru).. Ndugu yangu mwanaume Chonde Chonde Usioe..

1102417

Huyo Jamaa anaitwa Ratan Tata.. Hajawahi kuoa.. Je unavyomwona Hana Furaha??

Believer!
 
Kwenye maisha kila mtu anafanya kile kinachoufirahisha moyo wake na kuuridhisha moyo wake!

Wewe unaamini bila kuoa utakuwa na furaha daima, ila kuna ambao wanaamini bila ndoa furaha zao hazijakamilika!

Sio wanaume wote wataoa, na sio wanawake wote wataolewa! Kila mtu aamue venye moyo wake unapenda!
 
Ila nimewashauri tu vijana wangu.. Aisee wasioe.. Watajuta!
 
Ila ukweli usiopingika now days hakuna ndoa....na hata zile ndoa zilizofungwa zina hatihati ya kuvunjika

Sijui nn tatzo ila vijana wengi now ni wa kuonja na kusepa..!!waoaj n wachache nao ndo hutendwa vby

Mimi n mmojawapo kwa sasa sifikirii kuoa....maybe huko mbeleni..!!

Siku hz usaliti...kuigiza mapenzi na break ups zmkuwa nying kuliko shanga

Siku hizi ni rahis kushinda biko kuliko kupata penzi la kweli

Vijana tutafute hela
 
Asante mkuu kwa kuwa huru kifikra.. sisi kazi yetu kuwaambia uamuzi juu yao😂😂
 
Back
Top Bottom