IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,184
- 7,819
Nimeingia bar moja maarufu hapa Dodoma nikitokea Kigoma ili nipate mlo na bia mbili tatu.
Sasa meza jirani nami mwanaume mmoja kaagiza ugali na makange naona ya mbuzi au ng'ombe, mdada mmoja mrembo sana anajituma kweli kumhudumia, huku akichombeza hapa na pale kwamba na yeye toka asubuhi hajala. Jamaa anamwambia usijali utakula mpaka uvimbiwe.
Mwisho wa mchezo jamaa ule ugali ameutia mavidole yake woootee na nyama kala zooteee halafu kamuita mdada wa watu akamsukumia ile left overs huku jamaa anaondoka. Sasa kilichonitia huruma ni yule dada kuamua kuanza kule ile left over huku akilalamika!! Kwa kuwa nilikuwa meza jirani nikamuuliza mbona wala huku walalamika?
Akajibu nifanyeje sasa? Wataka nilale na njaa kama jana? Aisee ilibaki chenji yangu buku 4 nikamwambia akachukue.
Muda nataka kuondoka akanipa kikaratasi kumbe kina namba yake, nilipofika gest nikampigia akaniambia ukitaka nije ulikofikia nipigie maana umeniokoa leo, nikamwambia nimeguswa tu na shida zako.
Back to wanaume kwa nini tufanye hivi kwa hawa ndugu zetu? Kwani ungemeambia nina pesa ya mlo wangu tuu si angeelewa?
Kwanini umdhalilishe binadamu mwenzako kwa kuwa tuu umemkuta bar?