Inasikitisha sana, kuna mdada tumekuwa normal friends bila ya kuwa na makubaliano ya kuoana, hatimaye mwezi wa 8 tukafanya mapenzi na ikapelekea kupata mimba.
Cha ajabu anadai kuwa lazima nimuoe la sivyo atanishtaki kwa wazazi wangu na ikibidi kwenye vyombo vya sheria.
Nimekataa katu katu isipokuwa nitamtunza mpaka mtoto atakapofikisha mwaka mmoja, na ntaendelea kumtunza mwanangu katika maisha yake.
Hivi wadada mkoje?
============
SIMILAR CASE:
USHAURI:
Cha ajabu anadai kuwa lazima nimuoe la sivyo atanishtaki kwa wazazi wangu na ikibidi kwenye vyombo vya sheria.
Nimekataa katu katu isipokuwa nitamtunza mpaka mtoto atakapofikisha mwaka mmoja, na ntaendelea kumtunza mwanangu katika maisha yake.
Hivi wadada mkoje?
============
SIMILAR CASE:
=========Kuna dada mmoja anasoma chuo cha nursing huku Iringa ameniambia ana mimba yangu baada ya kufanya mapenzi bila condom mwezi moja uliopita.
Pagumu ni pale atakaponiambia nimuoe kwani sina hata chembe ya upendo kwake isitoshe nina mchumba niliyempenda na kupanga kumuoa.
Niko tayari kumhudumia mwanangu atakayezaliwa kwa mahitaji yote anayostahili na huo uwezo ninao ila huyo nurse, nifanye jambo gani la busara kwani maji yashamwagika.
Naombeni ushauri wenu wadau
USHAURI:
I greet you all my elders.
Maisha ya ndoa ni zaidi ya uhusiano wa kawaida ya mwanaume na mwanamke yana changamoto nyingi na kuhitaji chemistry ya kimbingu kuliko akili yako ya kawaida.
Mara nyingi wanaume tunaanzisha mahusiano kutokana na matamanio yetu ya miili na macho.(utu wa nje) na kusahau umuhimu wa kuona zaidi ya hapo kwa mwanamke/mwanaume wa kuishi naye katika ndoa.
Matokeo ya kujiingiza kichwakichwa katika mahusiano. Kuna ndoa nyingi ambazo zinafungwa kimila, serikalini na taasisi za kidini ambazo chanzo chake ni Mwanamke alipata uja uzito, ili kuondoa social stigma kwa mwanamke na kuwajibika kwa kosa lake mwanaume anafanya maamuzi ya kuoa. Kama malengo ya uhusiano hayakuwa kuoana zaidi ya kushake, ukifanya maamuzi kama hayo, ndoa nyingi zinapopitia katika changamoto, hilo linakuwa ni tanzi kubwa na kusababisha sononi na kujuta kwa baadhi ya wanandoa.
Sio malengo yangu kulaumu wanawake
wanaopata mimba na kulazimisha ndoa
katika mazingira hayo ila ni kupambanua
upande wa pili wa shilingi. Hivyo kwa wanaume ukiamua kufanya usajili usikurupuke, elewa unaweza kujikuta upo kwenye ndoa utakayopenda kutoka lakini dhamira itakuwa inakusuta.
Kwa wanawake:
Kulazimisha mwanaume akuoe kwa ajili ya mimba, kunaweza gharimu furaha yako huko mbele katika maisha haya ya Duniani mafupi.
Mwisho wanawake na wanaume tusiamshe mapenzi kabla ya kujipanga kwaajili ya ndoa, utaishia kula makande wakati Mungu alikupangia ule biriani.
Nice week end JF.