Wanaume ehh! Hivi Huwa mnazingatia/mlizingatia nini zaidi ili kumpenda Mdada/Mwanamke?

Nikimpata

Mwanamke mwenye sura nzuri lakini mwenye tabia njema.

Mwenye furaha Kuwa na mimi lakini anayependa kukiri makosa na kujifunza Kutokana na makosa.

Mwanamke atakayeitunza na kuijali familia kwa katika hali yeyote ile.

Mwanamke anayeamini katika dini na mwenye staha na heshima anayejipenda na kujijali pia.

Mwanamke mwenye kuchangia katika uendeshaji wa familia na maisha kwa ujumla.

Mwenye kuridhika na kile alichonacho na asiye na tamaa bali mvumilivu.

Sijui ntampata kweli
Mwenye sura nzuri na tabia nzuri mkuu utasubiri mpaka uote upara...
 
Aisee wanaume najua wengine hapa mpo kwenye mahusiano na wengine ndo bado wanatarajia kuoa.

Huwa vijana wana shauku sana pindi wanapotaka kuoa na huwa na mapendekezo mbalimbali juu ya wanawake watakao taka kuwaoa/kuwa nao kwenye mahusiano.

Na ule usemo wa mwanamke sio sura ni tabia haujawahi waacha salama wengi hawakubaliani nao kabisa. Ila kuna mambo mbali mbali ambayo wanaume huzingatia. Wengine huzingatia uzuri wa sura au shape...

Wengine huenda mbali zaidi na kutaka wanawake wataokuwa nao kwenye ndoa/mahusiano wawe na kiwango fulani cha elimu utaskia "Mi sioi demu wa elimu ya form 4"

Wapo ambao hadi makabila wanazingatia eti akiwa mzigua basi lazima mwanamke naye awe mzigua

Na wale ambao wanazingatia umri eti mwanamke akiwa anamzidi umri hawezi kuwa nae

Wengine ndo wanakwambia akiwa mcha Mungu na mwenye tabia njema. Inatosha..

Ila kwa mfano Mimi ntazingatia mrembo na mzuri yaani nioe mtu anafanana na Ebitoke hata Kama anatabia nzuri duh!
Kabla ya Mambo yote tamaa Ni zingatio la kwanza tamaa huwa Ni sababu yawanaume kumfuata mwanamke na kumtongoza kupenda huja baada ya tamaa kufanya jukumu lake mengine kila mtu ana sababu zake ila hakuna mwanaume asie na tamaa akiwepo achunguzwe Kuna Shida japo tamaa nayo Ina sehemu zake siki sehemu tamaa hujitokeza
 
kwa hiyo wote tuwe mawaiter sasa

Sorry dadaa, ngoja nikishapiga supu nitakuja kunyoosha maneno vzr.... nimeshtuka kitu. Nimetema mate kulia nimefukia kushoto...... hii haikubaliki hata kidogo.....Hata ukitumia kanuni ya kipenyo na pi kutafuta...dadaa badae kidogo....
 
Anayemjua kristo kwa dhati, mnyenyekevu na mtiifu.
Hapo siangalii sura wala chura.
 
Huu Uzi mzuri sana, mi binafsi nazingatia tabia zaidi, wanawake wengi au karibu wote ni wazuri shida ni tabia je tutaendana. Kiufupi napenda mwanamke mwenye utimamu
 
Aisee wanaume najua wengine hapa mpo kwenye mahusiano na wengine ndo bado wanatarajia kuoa.

Huwa vijana wana shauku sana pindi wanapotaka kuoa na huwa na mapendekezo mbalimbali juu ya wanawake watakao taka kuwaoa/kuwa nao kwenye mahusiano.

Na ule usemo wa mwanamke sio sura ni tabia haujawahi waacha salama wengi hawakubaliani nao kabisa. Ila kuna mambo mbali mbali ambayo wanaume huzingatia. Wengine huzingatia uzuri wa sura au shape...

Wengine huenda mbali zaidi na kutaka wanawake wataokuwa nao kwenye ndoa/mahusiano wawe na kiwango fulani cha elimu utaskia "Mi sioi demu wa elimu ya form 4"

Wapo ambao hadi makabila wanazingatia eti akiwa mzigua basi lazima mwanamke naye awe mzigua

Na wale ambao wanazingatia umri eti mwanamke akiwa anamzidi umri hawezi kuwa nae

Wengine ndo wanakwambia akiwa mcha Mungu na mwenye tabia njema. Inatosha..

Ila kwa mfano Mimi ntazingatia mrembo na mzuri yaani nioe mtu anafanana na Ebitoke hata Kama anatabia nzuri duh!
😂😂😂 tonatofautiana kwenye kuchagua ila hata mm ebitoke hamna aisee... Mfano mimi napenda kuoa/kuwa kwenye mahusiano namwanamke ambae yani kikubwa nikimwona ama kumwangalia napata furaha, ani nikiwa nae nafurahi (hapa nazungumzia zaidi phyisical appearance) rather than tabia, na ili sasa nikuone nifurahi inabidi uwe na vitu ambavyo mimi navipenda ambavyo ni Cha kwanza kabisa awe mweupe au maja kunde ( maana mimi ni mweusi) ili hata nikimwoa anizalie watoto wenye mchanganyiko wa rangi siyo tuoane weusi wetu anizalie watoto wana sura kama ya mizengo pinda au steven wasira hiyo hapana aisee, kingine awe na mwili wa wastani mnene kiasi na asiwe mwembamba sana kama ruby, awe tu na nyama nyama kiasi ivi ila siyo tukunyema na pia awe na urefu wa kunifikia mabegani au zaidi maana mimi huwa mrefu sana na madem wa wafupi sana huwa wananikera sana ingawa pia wanajua kupenda kuliko warefu, dini na kabila mimi huwa siangaliagi, mm ni mkristo ila naweza oa wa dini yeyote au hata mpagani ili mrad tu tumependana na pia asinizidi umri, bora tuwe sawa kiumri au nimzidi kuliko ye kunizidi. Kwa hiyo ani mi mwanamke kikubwa akiwa na mwonekano huo basi ambao nikimwona tu ani nafurahi basi ataniteka akili zangu zote, vitu vingine kama tabia mimi huwa siangalii sana kwa sababu najua ni vitu vya kurekilebishana tu, tabia hubadilika tu so unaweza oa hata kahaba alafu ukambadikilisha akatulia kwenye ndoa vizuri tu, so hakuna tabia sugu, tabia hubadilika kulingana na mazingira na umri pia, mfano unaweza oa mwanamke alikuw si mlevi ila ukaja kuwa mlevi kwako kwa sababu we mume n mlevi so ni kama umemfundisha
 
Back
Top Bottom