Wanaume andikeni majina ya mama zenu kwenye hati ya viwanja na nyumba

Andika Jina lako tu we jiamini ukija ukiandika Jina la mama Yako AF ukapata ndugu washenzi ,Mama akitangulia mbele ya haki wanaeza kuja kukugeuka wakakudhulumu au mkasumbuana mno mahakamani
 
kimsingi kama utaandika mama yako ukae ukijua hizo mali ni za wanae sio' zako'likitokea la kutokea jiandae
 
Sijaelewa, kwa hiyo Wakopeshaji hawakuwa wameiona hati mwanzo?.

Kama ndivyo basi huo hata ukiita uzembe bado utakuwa umelainisha maneno.
 
Asee sikushauri kaka ni bora ukasajili hata kampuni ya Mchongo pale Brela ukaandika asset zako kwa jina la kampuni . Kuna ndugu washenzi sana asee wanaweza wakamtengeneza mama yako akakugeuka wakaungana kukudhulumu mali yako. Katika swala la pesa kaka hata ndugu yako usimuamini. Naongea hili sio kwa kubuni bali kwa yaliyotukuta
 
Back
Top Bottom