Wanaume ambao hawana mpango kuoa hebu njooni mtueleze nini kiliwafanya mfikie maamuzi hayo

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,802
Kama kichwa cha habari kinavuojieleza ilikuweje ukafikia hatua ya kufanya maamuzi ya hutokuja kuoa au hiutokaa Luciano

Je, tazizo ni nini?

1620803399902.png

 
Miaka kenda iliyopita, nilikua natoka na staff mwenzangu,ila baadae nilipata kazi yenye maslai zaidi nikahamia kampuni ingine. mambo yakaenda tukaribie kufikia hatua ya uchumba, tukaishi pamoja kwa miaka kadhaa.

Kazi zetu unakwenda leo unarudi kesho ndio ratiba ilivyo, so kila nikienda narudi siku inayofuata jioni, yeye mwenzangu anaenda asubuhi anarudi jioni kila siku.

Nyumba tuliopanga ilikua na familia mbili pamoja na sisi jumla ni familia tatu.mimi ni mtu nisiyejichanganya, hata rafiki ninaye mmoja tu(rafiki rafiki kweli wa kufa na kuzikana na ni urafiki wa zaidi ya miaka saba)waliobaki ni washikaji tu, tumezoeana sababu ya kazi. Hata mtaani sina mazoea nao zaidi ya salam, hivyo hata nyumba ninanyoishi.

Sasa kuna kipindi nikashanga! Kila nikirudi kutoka kazini hao jirani zangu nikiwakuta wananiangalia kama kuna jambo ila wanashindwa sema, kama dizain wanasikitika, nilihisi kama kuna kitu hakiko sawa lakini sikutilia maanani.

Iko siku nilikaa nje masaa 4 kwenda matano namsubiri mwanamke, anasema kwa sms yuko dukani,nikimpigia anakata.

Stori isiwe ndefu, kumbe kuna mwana anakuja na tukutuku saa saba za usiku nikiwa kazini, anajilia mzigo alfajiri anasepa.

Sitaki kukumbuka, inatosha nyie fungeni ndoa tu, mimi bado nipo sana.
POLE SANA NAOMBA UNISAMEHE YULE JAMAA ALIKUWA NI MIMI.
 
Back
Top Bottom