Wanatakiwa kuweka tangazo kuwa unywaji wa soda kupita kiasi ni hatari kwa Afya yako

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Soda na Soft drinks zote ni hatari kwa afya ya binadamu. Binadamu hakuumbwa kubugia sukari nyingi namna anayobugia leo. Sukari nyingi huleta unene wa kupitiliza, kitu ambacho huleta kisukari, magonjwa ya moyo nk.

Ni wakati sasa, kama ilivyo kwenye bia; Kwa matangazo yote ya vinywaji laini na kwenye chupa zao kuwa na tangazo la onyo kuwa unywaji kupita kiasi ni hatari kwa afya yako.
 
Ni kweli hivi vinywaji ni hatari kwa afya ya binadamu. Kuna hizi soda nyeusi ukinywa zinapunguza ufanisi wa kupiga shoo na huondoa usingizi.

Ni vinywaji vitamu na laini ila vina madhara mficho, ni bora tu waweke tangazo kwa wanywaji wake kuwa ukinywa sana ni hatari kwa afya yako
 
Ni kweli hivi vinywaji ni hatari kwa afya ya binadamu. Kuna hizi soda nyeusi ukinywa zinapunguza ufanisi wa kupiga shoo na huondoa usingizi. Ni vinywaji vitamu na laini ila vina madhara mficho, ni bora tu waweke tangazo kwa wanywaji wake kuwa ukinywa sana ni hatari kwa afya yako
Kwenye ufanisi wa kupiga shoo naunga mkono hoja kabisa ni kweli
 
Kwa nilivyo kimbao mbao acha nimnywe tu
Zaman mgonjwa wa moyo tulikariri ni yule mnene, hivohivo presha na kisukar tulidhani wanene ndio wenye hiyo hatari, lakin saizi ata uwe kimbao mbao hayo magonjwa hayachagui.

Kikubwa kuzingatia mlo mzr tu. Maji ni kinywaji fulani kitamu lakini hakina sukari.

Mimi naelekea kumaliza mwaka sasa sijatumia soda yoyote au juice yoyote 😁, najua kuna mtu atakuja kusema ni ukata nilio nao, ila ndiyo nakubali😁😁 ila huwa sipo interested na hivyo vinywaji.
 
Back
Top Bottom