Wanataaluma wetu kuzamia kwenye siasa: ‘Kunani’?Wanajiunga CCM sasa kina fikra za Mabwana na Watwana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanataaluma wetu kuzamia kwenye siasa: ‘Kunani’?Wanajiunga CCM sasa kina fikra za Mabwana na Watwana

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by nngu007, Oct 5, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [h=2]
  Alhamisi, Octoba 04, 2012 05:25 Na Chrysostom Rweyemamu
  [​IMG][​IMG][​IMG]

  *Wako tayari kufungia shahada zao kabatini, zikiwamo za Uzamivu (PhD)!
  *Wanapanda jukwaani kuhubiri kile ambacho katu hawakusomea

  NI tabia iliyoota mizizi sasa hapa nchini. Wasomi wetu wengi wanaacha taaluma zao walizozisomea na kujiingiza kwenye siasa. Wako radhi kufungia shahada zao kabatini, zikiwamo za Uzamivu (PhD) ili kufanya kazi ya kupanda jukwaani kuhubiri kile ambacho kamwe hawakusomea!

  Kuna utamu gani kwenye siasa? Profesa Charles Bwenge wa Chuo Kikuu cha Florida, Marekani (zamani alifundisha katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) aliwahi kulisemea hili la kukengeusha malengo ya taaluma.

  Aidha, mwandishi wa habari mkongwe na mahiri nchini, Balinagwe Mwambungu, naye aliwahi kuliandikia hili na kuishangaa hali hii(na pengine hadi sasa bado anashangaa), kwamba suala la wasomi kuacha taaluma na kukimbilia siasa, na wanasiasa kutamani'vyeo' vya kitaaluma wakati wao si wanataaluma ni kichekesho!

  Kwa hakika si kila mtu mwenye shahada ya Uzamivu ni mwanataaluma. Wako watu waliosoma wakafikia kikomo cha 'darasa' (Uzamivu) kama ‘Wabongo’ wanavyosema; hawakurudi darasani kwenda kufundisha, wala hawafanyi kazi za kitafiti kulingana na sifa (qualifications) zao, bali wameingia katika shughuli nyingine tofauti, na wala hawapendi kujulikana kama “madakta”.

  Lakini cha ajabu kuna watu wengi hapa kwetu, kwa sababu ya kutaka sifa tu ya kutambuliwa kama wasomi, wanasisitiza kuitwa “dakta” hata kama “udakta” wake umeishia kwenye kupata cheti tu.

  Kuna wengine wamediriki kughushi na kujifanya wana shahada za Uzamivu, kumbe ni ‘vihiyo’ wa vyeti hivyo! Na hawaoni tatizo wala aibu, hata baada ya kugundulika. Mifano ya wazi ya baadhi ya wanasiasa wetu hapa nchini inadhihirisha hili.

  Wengine wanadhani kuitwa “dakta” ni sifa inayomfanya mtu kukubalika ndani ya jamii; wengine ni kutaka kujikweza tu kwa vile walikosa nafasi ya kuendelea na elimu katika utaratibu wa kawaida na kuamua kuutafuta “udakta” kwa njia nyingine au ya mkato!

  Viongozi wetu wengi wa zamani (waliopigania uhuru) walipata shahada (digrii) zao wakati wakitumikia vifungo enzi ya utawala wa kikoloni. Lakini ni muhimu kukumbuka kuwa mtu akitaka kuwa kiongozi ndani ya jamii, si tu awe anakubalika, bali pia awe na uelewa wa masuala mbalimbali ya ndani na nje ya nchi ili aweze kuwaongoza vizuri wale anaotaka kuwaongoza.

  Hana budi kuwa na uwezo wa kufanya uamuzi wa busara. Mtu hawezi kufanya uamuzi wa busara kama hana taarifa na jambo lililo mbele yake.

  Lakini watu wengine wanafikiri kwamba usomi ni cheti, kwamba kinamtosha kumfanya kuwa kiongozi. Ndiyo maana hata hapa kwetu waheshimiwa wengine (kwa ubinafsi wao tu au kwa kuogopa kivuli cha mtu mmoja tu), walitaka kupeleka muswada bungeni, kuwazuia wananchi wasio na vyeti vya vyuo vikuu kugombea nafasi ya cheo kinachoitwa “rais”, na wakataka kipengele hicho kiingizwe kwenye Katiba ya nchi.

  Kwa hiyo suala la wasomi wetu wengi kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge, naamini hii inatokana na msukumo wenye ubinafsi zaidi kuliko kutaka kuwatumikia wananchi. Hakuna utumishi uliotukuka kama kukaa darasani na kufundisha wananchi ili waondokane na ujinga.

  Hakuna faraja kubwa kama kuona kwamba kupitia elimu uliyoitoa, wananchi wamepata silaha nzuri zaidi ya kuweza kujenga moyo wa kujiamini zaidi na kuuthamini utu na utaifa wao ili waweze kusimamia mambo yao kikamilifu, waweze kufanya uamuzi wa busara (informed decisions) hata kuamua nani wanataka awe mwakilishi wao bungeni.

  Lakini wasomi wetu wengi (kwa kuangalia chama walichokichagua kuwa ndicho kitakachowapeleka bungeni, walifanya hivyo kwa kutafuta utukufu na kuendeleza maslahi yao binafsi na si kutaka kuwatumikia wananchi.

  Wasomi wengi wanajiunga katika kinyang'anyiro hicho kupitia chama tawala kwa vile wana uhakika kwamba ndicho kinachoweza kuwatimizia ndoto zao za wao kukamata hatamu za uongozi wa nchi.

  Binafsi nawaheshimu sana wasomi ambao wamechagua njia tofauti, ya kupambana na mfumo mbovu, uoza wa rushwa na dhuluma uliojikita katika chama kikongwe, na hata katika vyama vichanga.

  Hawa wameamua kwa dhati kabisa kujitolea si tu nafsi zao, bali hata muda na rasilimali ndogo waliyonayo kuitumia katika kueneza 'injili' ya mageuzi na kuwaamsha Watanzania ambao ndio wenye nchi.

  Mwalimu Julius Nyerere, ndiye aliyeonyesha njia ya utumishi wa umma. Wakati wa kuutafuta uhuru wa Watanganyika, alikubali kujitolea, kufanya kazi ya kueneza 'injili' ya uhuru, bila mshahara, bila shangingi, bila ufahari na hata baada ya kupata ridhaa ya kuongoza nchi, alionyesha mfano mzuri wa kuishi kwa yale aliyoyahubiri, wakati viongozi wengine wa Kiafrika walikuwa wakikimbiza mamilioni ya fedha na kuyaficha Uswiss na kuishi maisha ya kifahari, ilhali watu wao wakiendelea kudidimia katika umasikini.

  Wasomi wetu wanakimbilia kujiunga na chama tawala ambacho kwa kiasi kikubwa kimekwisha kuacha njia ya kuwapeleka wananchi 'kwenye nchi ya maziwa na asali', bali kinajenga tabaka la wakubwa na watwana, walionacho na wasio nacho, watawala na watawaliwa, wenye haki na wasio na haki.

  Kila mtu anayo haki ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote anachokitaka, lakini akili ya kawaida inanituma kwamba, wasomi wetu wangelikuwa mstari wa mbele katika kuleta mageuzi ya kweli katika nchi yetu. Badala yake wanatimiza ile dhana potofu ya 'kama huwezi kuwashinda, jiunge nao'.

  Huu ndio msukumo ambao umewakumba wasomi wetu wengi kuacha kusimama kidete na kukemea ubadhirifu, wizi, ufujaji mali ya umma na ukandamizaji wa wananchi unaoendeshwa na mfumo kongwe unaowafanya wananchi wajione kuwa hawana sauti na kauli katika mambo ya nchi.

  Watu ambao hawamo katika kuta za wasomi wanajiuliza, hivi walimu wanafundisha nini vyuoni siku hizi? Kama wanafundisha masomo yale ya zamani ya kuichambua mifumo na tawala za dunia, wanawaambia nini wanafunzi wao kuhusu uongozi na hatima ya nchi yetu. Wanasemaje kuhusu rushwa iliyojichimbia katika mfumo wa utawala katika nchi yetu na nyingine za kiafrika?

  Wanafundisha nini kuhusu utawala bora, uwajibikaji na nafasi ya wananchi katika kuendesha nchi? Wanafundisha nini kuhusu ‘ugenishaji’ wa rasilimali za nchi unaoendelea chini ya kivuli cha utandawazi, na mambo mengine mengi?

  Kama kweli wasomi wetu wanayachambua masuala haya, hivi inaleta mantiki kwao kufundisha haya na halafu kuamua kugombea uongozi katika mfumo uleule? Kama msomi atakayesoma makala hii atatoa jibu la 'ndiyo' basi ni mnafiki kama walivyo wanafiki wote wanaojifanya wanaomba uongozi ili wawatumikie wananchi, wakati wanaomba uongozi ili wajinufaishe wenyewe.

  Lugha ya utumishi wa umma ni lugha ya ulaghai. Mtumishi wa umma ni yule ambaye hatangulizi maslahi yake mbele. Mtumishi wa umma kamwe hawezi kunyang'anya mali ya jumuia akaifanya yake binafsi au akajiuzia mali ya wananchi kwa bei anayotaka mwenyewe kwa vile anajua kwamba wananchi hawatamkaba koo, kwa kuwa ndiye aliyeshika mpini, na yeyote atakayejaribu kumzuia “atakiona cha mtema kuni!”

  Kwamba baadhi ya sera za vyama ambazo wanasema maudhui ya kuundwa kwake, na uzuri wake si sera bali ni misemo ya kuwarubuni wananchi ili waendelee kuamini kwamba wana vyama makini na tetezi, na kwamba ndivyo pekee vinavyojali maslahi na usalama wa nchi!

  Nchi hii haitapata mabadiliko ya haraka ya kiuchumi, kimfumo na hata kiutawala kama wasomi wetu wataendelea na mtindo huu wa kujitafutia maslahi binafsi.

  Uko wapi moyo wa miaka ya 1990, moyo ulioamsha ari ya mageuzi nchini na wasomi wakawa mstari wa mbele kutaka mabadiliko?

  Inakuwaje wasomi wetu wamegeuka kuwa wasaliti na wanaungana na upande wa pili unaokandamiza haki za wanyonge?


  [/h]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Wasomi Wetu Sasa ni Maboya... CHUO KIKUU SIO PAHALI PA WAALIMU WENYE ITIKADI TENA...
   
 3. M

  Mngendalyasota Senior Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Anaweza akawa na Dr Benson Bana yumo kwenye list hiyo nini?
   
 4. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Mkuu ivi inawezekanaje KIBAJAJI na elimu yake ya std 7 alipwe zaidi ya ml7 kwa mwezi na Dr.alipwe laki9 kwa mwezi? siasa inalipa ndio maana imevamiwa na makanjanja wanatafuta mshiko.kuna watu tuwajuwa maisha yao kabla ya siasa,na baada ya kuingia kwenye siasa nakupata vyeo vikubwa wamekuwa matajiri wakupindukia.
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  its abt maslah nan anataka kupigizana kelele na mitoto ilodata then mshahara kiduchu while waweza kuwa mheshimiwa na mijihela kibao
   
Loading...