Wanataaluma Wakristo watoa waraka wa 'Tafakari' kabla ya kuichagua CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanataaluma Wakristo watoa waraka wa 'Tafakari' kabla ya kuichagua CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Mar 9, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Habari Leo

  CHAMA cha Wanataaluma Wakristo Tanzania (CPT) kimekiri kutoa waraka ambao wenyewe wameuita ‘tafakari' ukikishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kukituhumu kuwa ndicho kikwazo cha ukuaji demokrasia nchini.

  Waraka huo uliopewa jina la ‘Tafakari ya CPT, Uchaguzi Huru na Halali', umeishambulia CCM na kuitaja kuwa kikwazo cha demokrasia ndani ya vyama vya siasa visivyokuwa na nguvu kiuchumi.


  Pia CCM imesema kwa sasa haina muda wa kujibizana na mtu au waraka wowote na badala yake inatumia dakika zilizobaki kuelekea uchaguzi mkuu ujao, kufanya kazi kwa mujibu wa ilani yake.


  Akizungumza na HabariLeo jana, Mwenyekiti wa CPT, Joseph Ibreck, alisema chama hicho hakina ugomvi na CCM isipokuwa kimetoa ‘tafakari' hiyo, kwa lengo la kushirikisha wananchi kutoa mawazo katika masuala yanayohusu mustakabali wa nchi. "Huu si waraka ni tafakari ambayo ni mwendelezo wa Ilani iliyotolewa na chama hiki kuhusu Uchaguzi Mkuu na tutaendelea kutoa tafakari kama hii hadi mwisho wa dunia," alisema Ibreck.


  Alisema ‘tafakari' hiyo inalenga zaidi sheria ya gharama za uchaguzi iliyopitishwa hivi karibuni bungeni. "Lengo hapa ni kutaka kujua kwa nini sheria hii imekuja sasa, inamlenga nani, madhumuni ya gharama za uchaguzi ni nini na nani atafaidika."


  Hata hivyo, alisema ‘tafakari' hiyo ilitoka muda mrefu kabla hata rasimu ya sheria ya uchaguzi haijaenda bungeni, lakini ilichelewa kutolewa na kusambazwa.


  "Napenda ieleweke kuwa hatuna nia mbaya, tumewatumia CCM kwa kuwa wao ndio wanaotoa mapendekezo ya sheria, hatuna ugomvi nao."


  Akizungumzia suala hilo, Chiligati alisema chama chake hakina muda wa kupoteza kujibizana na watu na kuwataka wenye malumbano dhidi ya CCM, wasubiri kampeni.


  "Huu si wakati wake, wasitupotezee muda, tuko kazini na hatutaki malumbano na kundi lolote, maneno au malumbano yatafanywa wakati wa kampeni, ila wanaosema waacheni waendelee sisi tupo kazini," alisema Chiligati.


  Alisema kama ni soka kwa sasa ni dakika za mwisho ambazo hazijaisha. "Tukiendekeza malumbano au maneno tutafanya kazi saa ngapi?"


  Kwa upande wake, Makamba alipoulizwa alisema "hata kama waraka huo ukitufikia hatuna muda wa kujibu, ukweli ukitokea uongo utajitenga." Alikanusha tuhuma zilizotolewa dhidi ya CCM na kuongeza kuwa hakuna ujanja wowote unaotumiwa na chama hicho kujipatia mamlaka na katika suala la kujitwalia mali zisizohamishika na hisa, alisema mali zote ni za chama hicho.


  Kwa mujibu wa waraka huo ambao umeshambulia CCM, pia unakosoa mwelekeo wa kisiasa nchini hasa baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa siasa ya vyama vingi miaka 18 iliyopita, ambapo pia umeitaka CCM kutangaza hesabu za gharama halisi zilizotumiwa na vyama vyote vya siasa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2005.
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  wanataalum au udini mtupu..blah blah ...anzisheni chama cha siasa..au jiungeni na CCJ maana tunafahamu imetokana na waraka wenu ...msisumbue watu ...hakuna jipya kutoka kwa wakatoliki zaidi ya kupenda kupendelewa na kupenda kupita kutawala watu wenginee.. ...tunafahamu mmeshaanza kampeni zenu kanisani lakini.hadangayika mtu..siku hizi..
   
 3. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  kutokana na kauli zako inaelekea wewe ndo una udini sana
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Wamependelewa vipi wakati 75% ya viongozi wetu ni waislam
   
 5. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Usitake kubadili mwelekeo kama kawaida yenu...wanataalum wanahangaika kutoka waraka si upuuzi mtupu si wajiunge na vyama vya siasa..blah blah...

  Sijaona wakitoka waraka wa kulaini ushoga kanisani ..kama siyo upupu ni nini?
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Mar 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  PCT endeleeni kuamsha waliolala, Makamba na Chiligati wanadai kuwa hawana muda wa kujibishana na mtu lakini wameshaanza kujibu tayari kama ilivyo kwenye quotation hapa chini:
  Unajua mtu anaweza kudai kwamba halii wakati machozi yanamdondoka toka machoni! Kazi ipo mwaka huu!
   
 7. Kabuche1977

  Kabuche1977 JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  utakuwa huna data wewe, mbona Misikitini USHOGA umejaa kuliko hata makanisani, au kwa sababu wakristo wako wazi na mambo yao ndo unafikiri misikitini hakuna ushoga--------mbona mashekhe wengi mashoga kwa kwenda mbele
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  -Hebu tuajadili hii hoja bila ushabiki wa kidini.mimi kwa kusema kweli sikupenda hii kitu ambayo watu wamejitangaza wanataaaluma wa kikristu,sasa hapa ndipo udini unapokuja.

  Mimi napinga hiyo taasisi kujihusisha na masuala ya kisiasa coz casuality yake ni kubwa kuliko wanavyofikiria.Tuacheni hizi elements za ubaguzi

  Kwenye Hoja:

  Hawa wanataaluma wangefanya jambo jema sana kama wangewaamsha tu wananchi na kuwapa elimu ya Uraia bila kuishambulia CCM.
   
 9. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #9
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kama kawaida.Mzee wa imani kali.Na nyie si muandae ya kwenu.Acha kulia lia...Kama hakuna jpya kinachokusumbua nini si utulie tu Mkuu?
   
 10. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #10
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Yaani huu ni upeo mdogo kabisa wa kufikiria. Unaacha kujadili hoja unaanza kumjadili mleta hoja. Huu ni ukosefu na ni utindikivu wa mawazo na fikra zinazotokana na kujengwa kwa fikra potofu na chuki katika vichwa vya hawa watu.

  Jadili hoja sio mleta hoja please hebu onyesha ukomavu kidogo, walau katika hii hoja ambayo haihusiani na dini kabisa, sont turn everything in JF to be the way you like (mlolongo wa mgongano wa kimawazo ya kidini).

  Yaani hapa ni sawa kuwa Dk Slaa kwa sabau ni mkristo basi hata hoja zake utakuwa unazichukia-what a crap! Mature now, dini haitokufanya ufike kwa the man upstairs!
   
 11. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #11
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu GS,
  Nope,mkuu hapa hatutakubaliana.Two wrongs cannot make one right!

  Na wewe mkuu Tumain,

  Hivi udini utakufikisha wapi ndugu yangu?
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Niambie basi mkuu.hukubaliani na mimi wapi?wapi nilipokosea kwa mtazamo wako?
   
 13. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #13
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  umeusoma huo waraka, ama kukurupuka tu, nawewe nawe.
   
 14. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #14
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  kwani wamevunja katiba ? jadili katika mitizamo sahihi......! kwanini kila anaejadili siasa ni mwanasiasa.
   
 15. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #15
  Mar 9, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Yaani inatisha sana pale mtu anapokuwa blackened na hizi vitu hata kufikiri kunapungua, can you imagine mtu anakuwa wa kwanza kuchangia hoja kama hii, ambayo has no religious conflict but he wants to turn it into religious battle? What a mind!!?? Mtu anaacha kujadili point ya msingi, they cant read through lines. Yaani mtu akiona neno Mkristu tu anajua sasa hii ni thread ya dini sasa wacha nianze!-C'mon wake up from that deadly minds
   
 16. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #16
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Pale ulikomwambia Tumain ,wao waanzishe waraka wao.Yote haya yanachochea udini kama tukiyapeleka ktk siasa ndugu yangu.It's risky!
   
 17. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #17
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hapo umenena, maana anaitoa haki ya kujadili mustakabali wa taifa kwa watu wamakundi yoote, na by the way mtu mwenyewe anatoa hukumu kwa waraka ambao hajausoma.....kweli nashangaa haya mawazo dhalili.
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Mar 9, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Udini katika kuendesha siasa umegharimu na au umeyaweka mataifa mengi katika delicate situation.

  Kesho nao wataibuka waislamu watatoa waraka wao kuipa support CCM au CUF.Wapagani nao sijui watampa sapoti Mrema na TLP au itakuaje,tujaribu kuepuka risky kama hizi.Hao jama wangeweza tu kufanya jambo la kuwaelimisha wananchi na kuwapa elimu ya Uraia bila kujiingiza moja kwa moja kwenye mjadala kama huo

  Unadhani watu wa kawaida wataelewa vipi?Ona Tumain alivyoanza kulalama,kuna watu kama huyu mkulu wangapi huko Tanzania?Watauchukulia vipi huo waraka?Hebu tumia mawazo kama haya ya Tumain uaangalie ni watu wangapi kule Bongo wanafikiria hivyo hivyo
   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Mar 9, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ben, swala moja ni kuwa sio lazima Waislamu waige kila Wakristo wanachofanya, maaana waswahili walisema kumuiga tembo huishia kuchanika msamba !
  kwani wao waislamu wanawasiliana vipi na waumini wao ? wao waendelee na taratibu zao katika kujadili ujenzi maridhawa wa taifa hili.
  kwa mfano Wakatoliki wamekua na taratibu zao za kupeana nyaraka zao kila baada ya muda fulani, wao wanamambo wanayoamini kuwa ili mtu aweze kuabudu vyema ni lazima mazingira yaletwayo na hali ya kisiasa yawe tulivu, uchumi uwe mzuri na mambo kama hayo.
  sasa kukaa nakujadiliana eti na watu wadini nyingine namna yakuendesha kanisa huo ni ujinga, na haukubaliki.
  kuna makundi ya watu yanadeka sana nnchi hii, wanapenda kulialia, wanahamishia matatizo yao yakihistoria kwa wengine. kifupi adui yao namba moja ni wao wenyewe.
   
 20. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #20
  Mar 9, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kila mtu anayo haki ya kusema na kutoa maoni yake mwenyewe maana kila mtanzania ni haki yake ya msingi
   
Loading...