Wanasingida mashariki kuandaa maandamano ya kuomba uchaguzi ili kumpata mwakilishi bungeni

mkuu acha kuleta siasa sisi tuliokuwa na ndugu zetu jimboni singida mashariki ndo tunajua shida gan wanazipata bibi zetu ilihali mbunge aliyetuahidi atazitatua anazurula tu ulaya
Unge muuliza bibi kwanza, nini lengo la kumpeleka (kumchagua) Lissu bungeni? Jibu atakalo kupa bibi ndio itakua mada nzuri yakuanzishia maandamano.
 
Risasi za wasiojulikana hazikuweza kuondoa uhai wa Lissu, kwa hiyo wameamua kutumia mawe? Ama una maanisha nini na habari zako zisizo rasmi?
 
mkuu acha kuleta siasa sisi tuliokuwa na ndugu zetu jimboni singida mashariki ndo tunajua shida gan wanazipata bibi zetu ilihali mbunge aliyetuahidi atazitatua anazurula tu ulaya
Mi' nilifikiri umekuja kutuhabarisha kinachoendekea huko, kumbe umetuletea mawazo yako!
 
Huu upumbavu wenu wa kishamba kuchukua pesa za umma kwenda kuwahonga wananchi wafanya maandamano haramu ya kijinga mtaacha lini? Kwani bila Bashite na kikundi chake kwenda Dodoma kumpiga Risasi angekuwa huko ulaya mda huu? Yaani CCM mnapiga mtu Risasi kaamua kuelezea Dunia mnaita uzurulaji? Ujue huko CCM kuna mbumbumbu na vilaza wa kutisha sana na mmewageuza watanzania ni wajinga kuliko nyie acheni dharau kwa wananchi Tambueni wana Akili kuliko nyie watetezi wa CCM mnaoshinda gheto kwa cyprian Musiba mkivuta Bangi na kukariri ufala wa Musiba
 
Hebu fafanua vizuri tuelewe!

Shida gani za wananchi zinazoweza kutatuliwa na mbunge?

Madiwani mnao?
Mkurugenzi yupo?
Mkuu wa Wilaya yupo?

Mbunge hana fedha za kujenga barabara wala kununua dawa.

Bajeti hupangwa na kila halmashauri ina mgawo wake.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwanza ukumbuke hata ukusanyaji kodi hufanywa na wengine siyo mbunge isitoshe wananchi hawana Tatizo na Tundu Lisu isipokuwa mbumbumbu wa CCM ndiyo wametengeneza Dili la kupiga pesa baada ya kupewa pesa za kwenda kuwahonga wananchi waandamane kufa kufaana Tundu Lisu kawanufaisha wengi huko CCM
 
Mimi nampiga Lissu lkn mwandishi adithi yako imekosa uhalisia hivyo haina radha hata kidogo. Usingewasingizia wananchi wa Singida,, ungesema kuwa hayo ndiyo mawazo yako..

Sent using Jamii Forums mobile app
Cyprian musiba na Le mutuz wameandaa Bajeti ya kifisadi wamempelekea Naibu Rais ndugu Daud Maliyamungu Bashite na yy baada ya kuipitia atampelekea mtukufu malaika toka chato kisha amwamuru Doto Katibu mkuu wizara ya fedha awape pesa za kuwanunua wananchi kisha wafanye vurugu ni mwendo wa kufa kufaana
 
Hivi shida za wananchi zinatatuliwa na mbunge? Akili zingine hizi ...hebu nenda hata chato uone kama wanachi wa huko shida zao zina tofauti na wanachi wa singida mashariki...jinga kabisa
Jimboni kwa Ndungai kunatisha wakati yeye ni Spika kuna kero zote za Duniani hata jimboni kwa Livingston Lusinde kibajaji wananchi wana funza miguu wanatembea nusu Uchi hakuna Bomba za maji ni shiiida kwa kwenda mbele hivyo hivyo kwa majimbo ya Msukuma, simbachawene, Nkamia na wenzao huko CCM
 
CCM ni chama tawala kinachotawala kama waasi waliopimdua Nchi wanatengeneza mazingira ya kuogopwa ili watawale milele, pesa za umma zinapotelea kwenye propaganda na mambo ya hovyo hovyo yasiyo na Tija kwa Taifa.
 
Record zinasema, wakati biashara ya kununua madiwan, wabunge na viongozi wa upinzani ikipamba Moto mwaka Juzi na mwaka Jana, Jimbo la singida mashariki halikuguswa na huo uhuni.
Sasa madalali wa siasa huko CCM wanaelekea huko yaani majimbo ya upinzani yamegeuzea Dili za kupigia pesa za umma zinazoidhinishwa na mtukufu malaika toka chato kwa ushauri wa Naibu Rais ndugu Daud Maliyamungu Bashite
 
Wananchi hao wataandamana lini kulaani waliotaka kuua mbuge wao?
Ni swali fupi tu kwa sababu fikra kama hizo ulizoweka hapo hazihitaji maelezo mengi.
 
mkuu acha kuleta siasa sisi tuliokuwa na ndugu zetu jimboni singida mashariki ndo tunajua shida gan wanazipata bibi zetu ilihali mbunge aliyetuahidi atazitatua anazurula tu ulaya
Mtetezi wa wanyonge,Mzalendo Namba moja Jembe na buldozer la kusafisha Mitaro HALIJAWANA wanyonge hao na kiwajali?, ama mpaka nao wawe wasanii ndo watalumbukwaa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwalimu enzi za uhai wake aliwahi kuonya juu ya mtu kujitabanabaisha kama "sisi" au "wananchi". Haya uliyoyasema hapa ungekuwa unasema 'mimi' yangekuwa sahihi sana kwa sababu tuna haki ya kutoa maoni, ila kutumia watu kuwakilisha mawazo yasiyo na mpangilio ya ubongo wako ni upuuzi wa kuachwa mara moja.

#Ningeona sana aibu kuandika thread kama hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani, majimbo ambayo wabunge wake, hawajaondoka, na wana hudhuria vikao vya bunge daily hali ikoje?....tuanzie kwanza hapo. Maana mie huku jimbo langu ni kama limetelekezwa ilihali mbunge yupo tu. Sasa mtoa mada utuambie ni jimbo gani ambalo kwa sasa wabunge wapo na limepiga hatua?
 
Subirini siku akiteuliwa kuwa Katibu mkuu wa UN mtaandamana na nchi nzima kumpongeza.
Dunia ya sasa ni kama kijiji. Masuala ya kusema sisi na wale ilikua ni enzi za ubaguzi na wabaguzi wapo bado wanarithi hulka za kibaguzi tena kwa kutumia mauaji kama mtoa mada alivyomuuaji mana amehamasisha Lisu apigwe mawe.
Upuuzi mtupu!!

Singida mnawaza vyeo badala ya Uhai wa Lisu.
Singida mngekua na busara nyie mngeandamana kushinikiza Lisu ahakikishiwe Usalama wake kwa kuwasaka magaidi waliofanya jaribio la kumuua.
Wauaji hawana rafiki.
Muuaji anaipenda roho yake mwenyewe .

Ni jimbo gani la Singida limeendelea kwa sababu ya Mbunge.
Bunge la sasa halina jipya. Ndio maana miradi mingi hawajawahi kuisemea na imeanzishwa.

Angalieni nyie watu wa Singida msije mkaachukiana kwa sababu ya wasaka vyeo na ubunge na Ubinafsi.
Kuna watu walifurahia kupigwa risasi kwa Lisu wakitegemea atakufa ili wachukue Jimbo kwa dhulma mana kwa kura hawapati.
Kama ndio mawazo yenu hayo hata maendeleo hamtapata ,mtachelewa sana.
Hakuna baraka kwenye kushangilia umwagaji wa damu isiyo na hatia.

Nabii Yusuf aliuzwa na ndugu zake ili afie utumwani,kwa sababu ya chuki na wivu wakihofia ndoto zake zisije zikatimia lakini Mungu alimuinua huko huko ugenini na akawa ndiye msaada kwa ndugu zake.

Singida Msichezee Lulu( Lisu) yenu kwenye choose cha Shimo. Watu wasiojulikana wakifanikiwa kwa Lisu watafanya mradi kwa kutumiwa na waroho wa madaraka na Ubunge kuwadhuru wengine kwa manufaa yao.
Hata katiba pendekezwa ilikataa kipengele cha kumtoa mbunge anayeumwa kwa sababu itafikia mahali watu watalogana au kutumiana majambazi kama waliotumwa na Hao wanaoutafuta ubunge ili wamshambulie mtu au hata kuuana kwa sababu ya kulifanya Jimbo liwe wazi.

Singida msikubali kuambukizwa Roho Mbaya.

Kodi tunalipa watanzania wote ili kila kijiji kipate zahanati,shule na maji . Lisu hakusanyi Kodi zetu na hana mamlaka ya kuagiza pesa za hazina zikatoka kama wanavyofanya wale na kupeleka kujenga stand ya ndege kwenye vijiji vyao.

Je ,Watakao andamana hawaoni kuwa wanaweza wakaibua maandamano makubwa ya kutaka waliomuua Mawazo wakamatwe na wale waliojaribu kumuua Lisu nao wasakwe???



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom