Wanasiasa wengi wa kizanzibari ndani ya serikali ya muungano wana "inferiority complex"?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,983
Habari wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia sana wanasiasa kutokan zanzibar walioko katika serikali ya muungano na nimegundua wengi wao wanaonekana kuupooza sana kiutendaji kwani ni nadra sana kupata mwanasiasa "machachari" ndani ya serikali ya muungano.Siku zote wanasiasa wenye majina kutokana na uchapakazi wao ndani ya serikali ni watu kutoka Tanzania bara.

Wanasiasa hawa ninaowaongelea ni wale walioko au waliowahi kushika nafasi za umakamu wa raisi,waziri mkuu,mawaziri na hata nafasi ya ukatibu mkuu.Siku zote katika serikali ya muungano, majina yanayovuma miaka nenda,miaka rudi ni ya watu kutoka bara,mfano,majina kama,Sokoine,Mrema,Mwakyembe,Magufuli n.k lakini kamwe si watu kutoka Zanzibar licha ya wao nao kushika nyadhifa kama hizo.

Nadhani kwa mazingira hayo hayo ndio maana hata pia ni nadra kusikia mwanasiasa kutokan Zanzibar akituhumiwa kwa kashifa kubwa kubwa kama ufisadi,wizi,matumizi mabaya ya madaraka n.k.

Mimi nafikiri tatizo kwa hawa ndugu zetu wanapokuwa ndani ya serikali ya muungano wanakuwa na kitu kinachoitwa "inferiority complex" na pengine msingi wa hali hii ni serikali ya muungano kutazamwa zaidi kama ni serikali ya Tanzania bara na Zanzibar kuonekana kama haina nafasi,imetengwa au haihusiki sana.

Jamani hili ni tatizo ambalo linapaswa kuwekwa hadharani na pengine limo ndani ya zile "kero za muungano".

Ni mtazamo tu based on "circumstantial evidence".

Nawasilisha.
 
wazanzibari as a whole wana INFERIORITY COMPLEX

si wanasiasa tuu mpaka raia

mie wananiudhi kijidai wao waarabu na kujiita AL SAID sijui al HABSHI sijui al BARWANI

sasa kama wao wanajiona wa Oman kwa nini wasirudi kwao MASKATI?

sasa naelewa kwa nini karume aliwalazima waolewe na waafrica
 
Wazanzibar hawajui wanawakilisha nini kwenye JMT. Hawajitambui hata wabunge wao hawaeleweki bungeni wanawakilisha nn. Huwa waniacha hoi unapokuta wanashupaa na ishu ya wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Geita wakati jambo kama hilo halina effect yoyote kwa Zanzibar.
 
Wanapoa kwa sababu ya mawimbi ya kuvuka bahari! Na ule mchezo wa baharini una waadhiri
!
 
Wazanzibar hawajui wanawakilisha nini kwenye JMT. Hawajitambui hata wabunge wao hawaeleweki bungeni wanawakilisha nn. Huwa waniacha hoi unapokuta wanashupaa na ishu ya wachimbaji wadogo wa dhahabu wa Geita wakati jambo kama hilo halina effect yoyote kwa Zanzibar.

Wanajiona wako less concerned na nahisi hawana uchungu na mambo ya bara.
 
Mkuu,hio ndio hali halisi na pengine hawana uchungu na mambo ya bara ndio maana wako less responsible!
Wanzanzibar wamekomaa kisiasa,pia msimamo wa dini inawafanya wawe na uadilifu!unaposema hawana uchungu ni nani alifanya mapinduzi ya uchumi huria kama sii mzee mwinyi???
 
Wanzanzibar wamekomaa kisiasa,pia msimamo wa dini inawafanya wawe na uadilifu!unaposema hawana uchungu ni nani alifanya mapinduzi ya uchumi huria kama sii mzee mwinyi???

Ndio maana nimesema majority ila si wote.
 
Wanzanzibar wamekomaa kisiasa,pia msimamo wa dini inawafanya wawe na uadilifu!unaposema hawana uchungu ni nani alifanya mapinduzi ya uchumi huria kama sii mzee mwinyi???

Watu kama Mzee Mwinyi ni Wazanzibar jina, maana Vitega Uchumi vyao vingi viko Tanganyika.
 
Uliza bei ya sukari,mafuta ya kula zanzibar kwa sasa halafu linganisha na bara!unachekelea mawaziri wa bara huku wanakuumiza ktk maisha ya kila siku ujinga gani huo?
 
Uliza bei ya sukari,mafuta ya kula zanzibar kwa sasa halafu linganisha na bara!unachekelea mawaziri wa bara huku wanakuumiza ktk maisha ya kila siku ujinga gani huo?
BONGOLALA najua wewe ni kada wa chadema lakini ndugu yangu katika IMANI hawa jamaa sio wenzako,wanaichukia dini yako kupita maelezo,ndugu yangu STUKA,hebu anza kufanya research haya niyasemayo halafu njoo na feedback cc Ritz
 
Last edited by a moderator:

Watu wanaongelea Siasa wewe unaleta Udini?
 
Last edited by a moderator:
BONGOLALA najua wewe ni kada wa chadema lakini ndugu yangu katika IMANI hawa jamaa sio wenzako,wanaichukia dini yako kupita maelezo,ndugu yangu STUKA,hebu anza kufanya research haya niyasemayo halafu njoo na feedback cc Ritz

Hoja hapa ni utendaji,sasa udini unaingiaje?

Nyinyi ndio mnaendekeza udini!

Kama umeshindwa kujibu hoja usituvuruge kwa kutuletea udini hapa.
 
Last edited by a moderator:
HE kumbe kua fisadi ni sifa?
Hata hivyo kimsingi kuna baadhi ya vyeo ktk Jmt vipo kama picha tu kuwahadaa wazanzibar wajione nao ni sehemu ya Serikali.
 
Hoja hapa ni utendaji,sasa udini unaingiaje?

Nyinyi ndio mnaendekeza udini!

Kama umeshindwa kujibu hoja usituvuruge kwa kutuletea udini hapa.

Wewe unaona mimi naleta udini while at the same time wewe unaleta ukanda kwa kutaka kuibagua zanzibar,usizunguke sana mkuu znz mnaichukia sababu ya __________ nadhani jibu unalo
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom