Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,986
- 144,313
Habari wakuu,
Nimekuwa nikifuatilia sana wanasiasa kutokan zanzibar walioko katika serikali ya muungano na nimegundua wengi wao wanaonekana kuupooza sana kiutendaji kwani ni nadra sana kupata mwanasiasa "machachari" ndani ya serikali ya muungano.Siku zote wanasiasa wenye majina kutokana na uchapakazi wao ndani ya serikali ni watu kutoka Tanzania bara.
Wanasiasa hawa ninaowaongelea ni wale walioko au waliowahi kushika nafasi za umakamu wa raisi,waziri mkuu,mawaziri na hata nafasi ya ukatibu mkuu.Siku zote katika serikali ya muungano, majina yanayovuma miaka nenda,miaka rudi ni ya watu kutoka bara,mfano,majina kama,Sokoine,Mrema,Mwakyembe,Magufuli n.k lakini kamwe si watu kutoka Zanzibar licha ya wao nao kushika nyadhifa kama hizo.
Nadhani kwa mazingira hayo hayo ndio maana hata pia ni nadra kusikia mwanasiasa kutokan Zanzibar akituhumiwa kwa kashifa kubwa kubwa kama ufisadi,wizi,matumizi mabaya ya madaraka n.k.
Mimi nafikiri tatizo kwa hawa ndugu zetu wanapokuwa ndani ya serikali ya muungano wanakuwa na kitu kinachoitwa "inferiority complex" na pengine msingi wa hali hii ni serikali ya muungano kutazamwa zaidi kama ni serikali ya Tanzania bara na Zanzibar kuonekana kama haina nafasi,imetengwa au haihusiki sana.
Jamani hili ni tatizo ambalo linapaswa kuwekwa hadharani na pengine limo ndani ya zile "kero za muungano".
Ni mtazamo tu based on "circumstantial evidence".
Nawasilisha.