Wanasiasa wengi wa kizanzibari ndani ya serikali ya muungano wana "inferiority complex"?

Wale msiotaka kunielewa mtambue kuwa haya ni matokeo ya muundo mbovu wa muungano.

Wazanzibari wengi wanaamini serikali ya muungano ni serikali ya Tanzania bara na hivyo wao kujiona wako less concerned including mawaziri.

Ulitakiwa kueleza hivyo tu badala ya kuzunguka.
 
Habari wakuu,

Nimekuwa nikifuatilia sana wanasiasa kutokan zanzibar walioko katika serikali ya muungano na nimegundua wengi wao wanaonekana kuupooza sana kiutendaji kwani ni nadra sana kupata mwanasiasa "machachari" ndani ya serikali ya muungano.Siku zote wanasiasa wenye majina kutokana na uchapakazi wao ndani ya serikali ni watu kutoka Tanzania bara.

Wanasiasa hawa ninaowaongelea ni wale walioko au waliowahi kushika nafasi za umakamu wa raisi,waziri mkuu,mawaziri na hata nafasi ya ukatibu mkuu.Siku zote katika serikali ya muungano, majina yanayovuma miaka nenda,miaka rudi ni ya watu kutoka bara,mfano,majina kama,Sokoine,Mrema,Mwakyembe,Magufuli n.k lakini kamwe si watu kutoka Zanzibar licha ya wao nao kushika nyadhifa kama hizo.

Nadhani kwa mazingira hayo hayo ndio maana hata pia ni nadra kusikia mwanasiasa kutokan Zanzibar akituhumiwa kwa kashifa kubwa kubwa kama ufisadi,wizi,matumizi mabaya ya madaraka n.k.

Mimi nafikiri tatizo kwa hawa ndugu zetu wanapokuwa ndani ya serikali ya muungano wanakuwa na kitu kinachoitwa "inferiority complex" na pengine msingi wa hali hii ni serikali ya muungano kutazamwa zaidi kama ni serikali ya Tanzania bara na Zanzibar kuonekana kama haina nafasi,imetengwa au haihusiki sana.

Jamani hili ni tatizo ambalo linapaswa kuwekwa hadharani na pengine limo ndani ya zile "kero za muungano".

Ni mtazamo tu based on "circumstantial evidence".

Nawasilisha.

Asante kwa kuwakilisha, Je ulikua ukitaka kuwaona wakipiga kelele kwenye majukwaa ndo ujue wanafanya kazi ama unataka waonekane kwenye vyombo vya habari? Maana kunawengine utendaji wao ni wa showoff, lazima waandishi wawepo ndio anafanya jambo ili tu aonekane wakati unakuta ni kilaza kuliko maelezo.

Ushauri wangu kwako, 'circumstantial evidence' uliyoitoa hapa nadhani bado haina mashiko (invalid) hivyo basi fanya research zaidi.
 
Na jee hiyo mizigo unaweza kutupa jina la Mzanzibari? Tatizo lenu ni masifa.

Mizigo haiwezi kukosekana lakini tuambie ni mzanzibari gani anaekubalika kiutendaji kama hao mawaziri wa bara?

Mpaka sasa hili swali halijajibiwa na sioni mtu mwenye sifa hiyo kutoka Zanzibar.
 
Asante kwa kuwakilisha, Je ulikua ukitaka kuwaona wakipiga kelele kwenye majukwaa ndo ujue wanafanya kazi ama unataka waonekane kwenye vyombo vya habari? Maana kunawengine utendaji wao ni wa showoff, lazima waandishi wawepo ndio anafanya jambo ili tu aonekane wakati unakuta ni kilaza kuliko maelezo.

Ushauri wangu kwako, 'circumstantial evidence' uliyoitoa hapa nadhani bado haina mashiko (invalid) hivyo basi fanya research zaidi.
Wengine tumezoea kuwaona wakikata utepe tu!

Tunataka kuwaona wakiwa "active" kiutendaji kwani hii nchi ni yetu sote.
 
Mizigo haiwezi kukosekana lakini tuambie ni mzanzibari gani anaekubalika kiutendaji kama hao mawaziri wa bara?

Mpaka sasa hili swali halijajibiwa na sioni mtu mwenye sifa hiyo kutoka Zanzibar.

Kwanza sifa unazotaka zimekufikisheni wapi nyie Watanganyika? Halafu babaangu unataka Mzanzibari aje kukujengea nchi yako? Bado hujatosheka na mchango wao hata utake pia mawaziri wakufanyieni? Halafu jiulize ulitegemea Mzanzibari gani katika Baraza la Mawaziri aliyewekwa kwenye post ambayo ingehitaji masifa na makeke kuonekana kuwa wanatekeleza wajibu wao?
Kuna maswali mengi ambayo ungejiuliza basi ungehisi swali lako halihitajiki.
Kwanza ulitegemea Mzanzibari awekwe kwenye post ihusuyo Tanganyika?
Pili Jee kuna waziri Mzanzibari aliepewa wizara yenye changamoto?
Jee unapogeneralize Uzanzibari na utekelezaji wa majukumu, ulishasikia neno mizigo kwenye serikali yao Wazanzibari?
Kuna maswali mengi ambayo mwenye busara angejitosheleza na kujijibu badala ya kuleta mada hii hapa.
 
Back
Top Bottom