Wanasiasa, Wasomi,Viongozi wa Dini.Wamekula, wamevimbiwa, wamelewa,wanabeua na kutoa gesi tumboni.

Guru Master

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
224
591
Kwa hali iliyopo sasa inasikitisha sana. Watizame wanasiasa. hawa ambao walipita nchi nzima wakijinadi na kuomba kura zetu. wakipiga na magoti na kunyenyekea sana. wamepewa madaraka. wamekula chakula cha watanzania. na kwa ulinzi tuliowapatia wanalindwa wale kwa raha na amani kabisa. wamekula sana. mpaka wamevimbiwa. sikiliza matamshi yao.utagundua ni matamshi ya waliovimbiwa. sikiliza wanavyotoa gesi na kuchafua hali ya hewa. hawajali. wamevimbiwa sana na wamebaki kubeua. wengine wamelala kabisa. hushtuka mara moja moja wanapojigeuza upande wa pili. lakini wamelala. unawasikia? unamsikia january makamba? unamsikia mwigulu nchemba aliyekuwa akipenda kujitanabaisha kuwa ni mzalendo kwa kuvaa tai na skafu za tanzania? hakujua kuwa uzalendo upo moyoni si usoni. amelala.

kuna waliolala kwa kulewa shibe, kuna wanaobeua, kuna wanaotoa gesi tumboni haya yote yanatokana na kushiba. wameshiba chakula tulichowalisha. wameshusha na neti. mbu wanapiga kelele nje ya net tu. wamelala usingizi mzuri wa pono mpaka mwaka 2020 wataamka tena na kuanza kutatua matatizo yetu halisi.

nenda kwa wasomi. wasomi wamechukua vyeti vyao. wakasambaza chini ili wapate kukaa vizuri sehemu safi. wamekalia elimu yao. wakasambaza miguu chini halafu wakawekewa sinia la chakula. wamekula sana. wamekula. wamekula mpaka matumbo yakajaa. wakajilaza chali. matumbo yao yakiangalia juu. elimu yao ikiwa chini ya makalio yao. nao wengine wamepitiwa na usingizi. wanakoroma, wanabeua, wanatoa gesi huko tumboni. taifa linaangamia. hawasemi kitu maana njaa mwana malegeza na shibe mwana malevya. wamelewa. wanapotaka kuongea wanamung'unya maneno. hayasikiki sawa sawa. wanageukia upande wa pili wanaendelea kukoroma.

viongozi wa dini. wameweka vitabu vyao chini juu yake wakaweka masinia makubwa ya vyakula. wamekaa wakila na kumtukuza mungu wao. wakala na kula. wakaimba nyimbo za kumshukuru "mungu wao" kwa kuwaletea chakula. wakala tena na tena. wakashiba, wakavimbiwa. wakaweka vitabu vyao chini ya vichwa vyao kama mito wakalala. wakawa wakiota ndoto mbalimbali na kila waliposhtuka walimtukuza "mungu wao" halafu wakageukia upande mwingine. wakalala.

haya yamekuwa ni maisha ya kila siku ya matabaka haya matatu katika maisha ya watanzania hawa maskini. ambao miaka na miaka hawaweza pata mtetezi wa kweli. na pia akiwepo hawajaweza mtambua mtetezi wa kweli. wanaishi maisha ya kubeti kwa wanasiasa, viongozi wa dini na wasomi. wanaishi kwa kucheza hizo karata tatu. za viongozi wa dini,wanasiasa na wasomi.

Mungu ni wakati wa kuangalia watu wako hawa. ambao siku zote wamekuwa ngazi za makundi hayo matatu. na ijulikane leo kuwa upo wewe ambaye upo. sikia kilio cha maskini sisi. tusamehe yote tuliyokukosea ili utuondolee adhabu hizi tuzipatazo.
 
tehe..tehe... umewapiga tukio! haipiti wiki mbili wataibuka na matamshi kisha watalala tena!
kinachowaponza kama hao wawili ni kuwa bado wanezing'ang'ania zile kambi zao za mtoto wa mfalme na matokeo yake hawaimbi nyimbo zinazofanana na mfalme aliyepo kwa kuwa wameamua kuchezesha mzani ambao kama nyama inavyopimwa na mawe ya mzani na kutokubaliana nao wanashindwa kupima majukumu yao kwa kuwa mawe yao ambayo ni mioyo yao imeshindwa kwenda na kasi iliyopo.
wamekuwa ni watu wa mazoea wameshindwa kujua kuwa siasa ni sayansi hivyo uwe tayari kubadilika.
 
2019 watakuja na mbwembwe nyingi nawatapata kura apo ndo utaelewa watanzania wanaakili ndogo elfu 20 inamsahaulisha mtu matatizo aliyopata miaka mitano.
 
Tena wengine wanatuambia tuvumilie magumu neema inakuja. Kweli mwenye shibe akili huwa ziko likizo eti neema inakuja , neema ipi hiyo bado miezi 35 tufike 2020.
 
Pole sana ,na bado 2020 wakija na paketi ya chumvi na sukari utawapa ULAJI tena,watakuja na maelezo ati wapinzani ndiyo waliowazuia,hivyo msichague wa pinzani.

Watakuja na maneno unaona hata Lissu tulikataa asichaguliwe TLS maana angeenda kutuvuruga kabisa.

Kaka yangu kwa sasa mwanangu akiniambia ati anaenda kufanya PhD nitamwomba akalime maana hicho cheti kwa sasa ni LAANA kubwa kwa TAIFA letu.
 
Wanajijali matumbo yao na familia zao, kujinufaisha kila kona, huku talalila nyingi kujifanya wako nasi, bure kabisa...
 
Viongozi wa dini nao wamelewa kbs kwel kwel... Mwingine juzi kasema Neema ipo njiani inakuja.. Mwingine kawakana waislam wenzie..... Nimeamini kwenye chakula kuna upofu mkubwa
 
Ndugu mtoa mada hii naomba uandae uzi mwingine kuhusu hawa viongozi wanaotudanganya na kutuadaa kila kukicha kwamba tuliombee taifa amani wakati wao wanajitoa ufaham na kuendelea kuminya haki za wengine " kwa maoni yangu amani ni tunda la haki "
 
Pole sana ,na bado 2020 wakija na paketi ya chumvi na sukari utawapa ULAJI tena,watakuja na maelezo ati wapinzani ndiyo waliowazuia,hivyo msichague wa pinzani.

Watakuja na maneno unaona hata Lissu tulikataa asichaguliwe TLS maana angeenda kutuvuruga kabisa.

Kaka yangu kwa sasa mwanangu akiniambia ati anaenda kufanya PhD nitamwomba akalime maana hicho cheti kwa sasa ni LAANA kubwa kwa TAIFA letu.
PHD ni laana kwa taifa! Teh teh teh .......najaribu kuwazia ile ya mawembe na yule jamaa was morogoro aliyelia kama yuko kwenye kitubio!....nimekosa Mimi,nimekosa sana!.....
 
Good observation,ila kuna kundi la ovyo kabisa umelisahau,maana kazi yao kuwalamba miguu wana si hasa.nao ni...."wanaha- bari"
 
PHD ni laana kwa taifa! Teh teh teh .......najaribu kuwazia ile ya mawembe na yule jamaa was morogoro aliyelia kama yuko kwenye kitubio!....nimekosa Mimi,nimekosa sana!.....

Umeona eh!
 
Yani mara nyingi sana huwa najiuliza hivi tulimkosea nini Mungu? Jee tulijichongea sanamu za shaba tukaanza kuziabudu?? Sijui ni lini tutafika Canaan, i see tutafia jangwani. Mungu atusaidie sana
 
mkuu uliyoasema sasa tunaona madhara yake. ndugai anaonekana kavimbiwa sana.. anatoa gesi tu kwa sasa..hali inachafuka kila anapokaa... aisee.
 
Badala ya kutuhangaisha na gesi ya songosongo matumbo yao yaliyofura stinking gas yangetosha

Wanaj.MBA kama nini
 
Ustadh mkuu wa jiji la makamba huwa hakosi magogoni kwenye mialiko,inasemekana anakesha kwenye maofisi ya umma kuliko anavyokaa misikitini,kama kuna ajira wampe
 
Back
Top Bottom