Wanasiasa, wasomi sasa wapongeza uteuzi wa Rais Kikwete

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Posted Date::11/14/2007
Wanasiasa, wasomi sasa wapongeza uteuzi wa Rais Kikwete
Na Waandishi Wetu, Dodoma
Mwananchi

BAADHI ya wanasiasa na wasomi wameunga mkono uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuunda na kuteua wajumbe Kamati ya kupitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini wakiwemo wajumbe kutoka kambi ya upinzani.

Mbunge wa Karatu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Willibrod Slaa, aliunga hatua ya Rais Kikwete ya kuunda kamati hiyo kwa kuwa ametekeleza haraka ahadi aliyoitoa hivi karbuni

Hata hivyo, alisema ana wasiwasi wa utekelezaji wa ripoti ya kamati akisema kuwa kamati hiyo inayoongozwa na Jaji Mark Bomani si ya kwanza kuundwa na serikalinchini kushughulikia mambo yanayogusa maslahi ya umma. Hii ni tume ya nne, lakini hakuna utekelezaji, alisema Dk Slaa.

Alisema kuundwa kwa kamati hiyo hakumaanishi kwamba tuhuma mbalimbali, zikiwamo za ufisadi walizozitoa dhidi ya vigogo kumi na moja wa serikali zimefutika.

Suala la madini, ni sehemu ndogo sana katika yote tuliyoyaeleza. Sasa kinachotakiwa Rais asiishie hapo tu, ashughulikie tuhuma zetu pia, alisema Dk Slaa.

Mbunge wa Longido (CCM), Michael Lekule Laizer alisema amefurahishwa na hatua hiyo ya Rais Kikwete kwani itasaidia tuhuma zote zilizotolewa katika madini kupata ukweli wake, badala ya watu kuachwa wakiendelea kupiga kelele kila siku.

?Nadhani serikali imeanza kutambua vilio vya wananchi. Hilo ni muhimu kwani litaondoa manung'uniko. Na nimefurahishwa na muundo wa kamati ambayo itakuwa ni muungano wa wajumbe kutoka vyama vyote, alisema Laizer.

Naye Mbunge wa Iramba Mashariki (CCM), Mgana Msindai alisema anaunga mkono kamati hiyo kwa kuwa italisaidia Bunge kujua mambo yaliyomo kwenye mkataba wa uchimbaji madini katika Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, ulioko Kahama, mkoani Shinyanga.

Pia naunga mkono kamati kuwa na wajumbe kutoka upinzani, itaondoa utata kwa wabunge na pia ni haki kwa wapinzani kuteuliwa katika kamati, alisema Msindai.

Naye Mwenyekiti wa Chama caha Tanzania Labour (TLP), alisema hatua ya rais kumteua, Zitto Kabwe imeonyesha kuwadhalilisha wabunge kutokana na hatua yao ya kumsimamisha mbunge huyo kuhudhuria vikao hivyo.

Mrema alisema Kikwete ameonyesha ujasiri mkubwa ambao wabunge wa CCM walishindwa kuufanya, hivyo wameumbuka kwa kitendo walichokifanya.

Hii ni aibu kubwa kwa Bunge letu, mtu mnayemsimamisha ndiye anakuwa kinara katika kamati ya uchunguzi, Kikwete anastahili pongezi kwani ameweza kutetea maslahi ya taifa bila kuangalia tofauti za vyama,?? alisema Mrema na kuongeza kuwa katika maslahi ya Taifa lazima kusimama kwa pamoja na kuacha tofauti zilizopo.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa hatua ya kuunda tume hiyo inaweza kuzuia ufisadi unaoendelea katika sekta ya madini ambao alidai kuwa ni watu wachache tu wanaofaidika huku Watanzania wengi wakiwa katika hali mbaya.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila alishauri Tume hiyo kupewa uwezo zaidi badala ya jukumu la kutoa mapendekezo pekee.

Alisema kumekuwa na Tume nyingi zilishowahi kuundwa nchini kwa kutumia pesa nyingi ambazo ni kodi za wananchi, lakini matokeo yake yanakuwa ni kiini macho kutokana na ripoti zake kufungiwa kwenye makabati.

Hata hivyo, Mchungaji Mtikila aliitaka kamati hiyo kufanya kazi yake kwa uwazi mkubwa na kutoruhusu kuingiliwa katika maamuzi yake ili kuhakikisha mafisadi wote waliohusika kuwekwa hadharani.

Wakati huo huo, taasisi ya Utafiti na Tathmini ya rasilimali ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (IRA) imeipongeza kamati hiyo ikisema kuwa imeundwa wakati muafaka na kuwahusisha watu muhimu.

Mmoja wa wakurugenzi wa IRA ambaye hakutaka jina lake kutajwa gazetini alisema kamati hiyo imetoa sura mbili kwa serikali.

Alisema sura ya kwanza ni serikali kutokuwa makini na kufanya mambo kwa msukumo wa wanasiasa na ya pili ni dhamira ya dhati ya rais kushughulikia tatizo la mikataba ya madini.

Hata hivyo alisema katika sura yoyote ambayo mtu angependa kuipokea, kuundwa kwa kamati hiyo ni changamoto kwa wanasiasa hasa wapinzani ambao sasa wanatakiwa kujipanga ili waje na agenda mpya.

"Hapa maana yake amemaliza mjadala wa madini, wapinzani wanatakiwa kujipanga upya kwa kutafuta agenda mpya," alisema.

Katika hatua nyingne, Mbunge wa Tarime (Chadema), Chacha Wangwe, aliipinga kamati hiyo Zitto, kujitoa kwenye kamati hiyo.

Alisema anapinga suala hilo kwa madai kwamba, kuundwa kwa kamati hiyo kumelenga kudhoofisha hoja ya msingi ya wapinzani ya kutaka sheria ya madini ifutwe kabla ya kwenda katika hatua ya pili ya kujadili mikataba.

Kizingiti kikubwa ni sheria, ndio haijakaa vizuri. Hivyo, kilichotakiwa ni sheria kufutwa kwanza halafu ndio tuzungumze mikataba mipya, alisema Wangwe.

Alisema mbali na hilo, ana wasiwasi kamati iliyoundwa na Rais Kikwete haitakuwa na tofauti na kamati zilizopita, kama vile ya Brigedia Mang??enya, Jenerali Mboma na Dk Kipokola ambazo alisema hazikubadilisha lolote, badala yake baadhi ya makampuni ya uchimbaji madini, yameendelea kupora madini ya Watanzania.

Wangwe alisema wasiwasi wake unatiwa nguvu na baadhi ya watu walioteuliwa katika kamati hiyo ambao alisema ni walewale waliohusika kutengeneza sera mbovu, mawakili wa serikali na wachumi wanaoishauri vibaya serikali. Ndio hao hao wamerudishwa kuishauri tena serikali katika suala la madini, ni ushauri gani watautoa?, alihoji Wangwe.

Juzi Rais Jakaya Kikwete aliunda kamati ya kupitia upya mikataba ya uchimbaji madini na kuteua wajumbe kumi akiwamo Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Kamati hiyo inayoongozwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mstaafu, Jaji Mark Bomani, Wajumbe wengine ni Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini, Salome Makange, Kamishina wa Sera Wizara ya Fedha, Mugisha Kamugisha, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Makazi Wizara ya Ardhi, Edward Kihundwa na Mbunge wa Kyela (CCM) na Dk. Harrison Mwakyembe.

Wengine ni Mbunge wa Msalala (CCM),Ezekiel Maige, Peter Machunde kutoka Soko la Hisa, Dar es Salaam (DSE), Mkaguzi wa Mahesabu kutoka Kampuni ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Mahesabu, Price Water Coopers, David Tarimo ambaye ni mtaalam wa masuala ya kodi na Mkurugenzi wa Madai na Sheria za Kimataifa, Wizara ya Katiba na Sheria, Maria Kejo.

Habari hii imendikwa na Muhibu Said, Kizitto Noya na Tausi Mbowe
 
Katika 'state craft' mara nyingi tume huundwa kutuliza mambo na siyo kuibua mambo. Wajumbe wa Tume huteuliwa kwa uangalifu sana kwa kuzingatia pamoja na mambo mengine 'deni walilonalo' kwa mamlaka iliyowateua na matarajio yao ya baadaye katika kujijenga ama kikazi ama kisiasa. Itatokea wajumbe wawili wa tatu ambao wataingizwa ili tume ipate 'sura ya kuwa neutral'. That makes good PR. Kwa hiyo kijana wetu Zitto inabidi awe makini. akiona mambo yanaenda visivyo ajitoe mapema...he has nothing to lose. Lilipotajwa jina la mwenyekiti wa tume...tiyari nilishakuwa na wasiwasi! Hadi za rejea nazo like a research questionaire huandaliwa katika namna ambayo italeta majibu ya aina fulani.....na ikileta majibu tofauti mtu anaambiwa 'ilikuwa nje ya terms of reference'

The beef lies in the Terms of reference and the extent to which members of the commission can have unlimited access to vital documents na wahusika muhimu. Mtego ulioko hapa ni kwamba mjumbe atakula kiapo cha utii na kutotoboa siri/habari nyeti (thanks to stalin!) ambazo zinaweza zika athiri 'maslahi ya taifa'.

Je tume itatoa maamuzi yake katika mfumo upi? - mapendekezo..kwa nani? ambaye analazimika katika muda gani kuyafanyia kazi? ni vipi tume itapata taarifa motomoto hasa kwa watu walio chini ya maafisa wakuu wanaotuhumiwa, kama maofisa hao wakuu bado wamekalia viti vyao? kwanini wasiende 'likizo' ili kutoa mwanya wa taarifa 'kutiririka' bila woga?
 
BAADHI ya wanasiasa na wasomi wameunga mkono uamuzi wa Rais Jakaya Kikwete kuunda na kuteua wajumbe Kamati ya kupitia upya mikataba ya uchimbaji wa madini wakiwemo wajumbe kutoka kambi ya upinzani.

Mbunge wa Karatu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Willibrod Slaa, aliunga hatua ya Rais Kikwete ya kuunda kamati hiyo kwa kuwa ametekeleza haraka ahadi aliyoitoa hivi karbuni. (FULL STOP!)


Hongera Mkuu Slaaa,

Hii ndio tunaita siasa na ustaarabu, aliyeyaanzisha ya ufisadi anaposema haya, sisi wananchi wafuasi ni kujibu AMINA!
 
Mkuu unachosema ni sawa sawa kabisa, lazima tuwe na utaratibu wa kusimama na kupiga makofi kwa zuri lolote linalofanywa na viongozi badala ya kulaumu tu.

Sasa tusubiri tuone hii kamati itapewa mandate ipi na kama itakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli ambayo yatainufaisha Tanzania kupitia rasilimali zake.
 
Sasa tusubiri tuone hii kamati itapewa mandate ipi na kama itakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli ambayo yatainufaisha Tanzania kupitia rasilimali zake.


Mkuu Bubu,

Heshima mbele, this is very strong stuff, sitegemei kuwa Zitto atakubali kuburuzwa tu ndani ya hiyo kamati, Ndesamburo, alipojitoa kwenye ile kesi ya Manji, pale pale kesi iliisha kabla haijaenda mbali kwetu sisi wananchi, kwa hiyo serikali ikaishia kuchekesha sana kwenye ile ishu,

Sasa here comes this, Zitto akijitoa tu tutajua kuwa haina kitu, na hapo ndipo kiama cha mawe kitakapomuangukia Muungwana, subira yavuta heri, ingawa sio all the time!
 
Unachosema ni kweli kabisa Mkuu. Zitto yuko makini sana na kamwe hatakuwa tayari kuburuzwa ili kuja na ripoti ambayo itakuwa haina jipya ila kuendeleza rasilimali zetu kuwafaidisha wageni tu na sio Watanzania.

Najua wakuu kwenye kamati hiyo ambao wamemzidi umri na madarasa watataka kumburuza, lakini wakifanya hivyo watakuwa wamefanya makosa ya hali ya juu.
 
Nampinga Wangwe anaposema zitoo ajitoe kwa sasa. huwezi kuwa predict wajumbe wengine kwamba watamburuza Zitto mapema. shurti aingie humo, aone ushupavu au udhaifu wao. tunamuaminia hatakubali ujinga, labda kama thamani yake imeshuka.
 
November 2007 tulisifia Mkuu kuongeza wasomi serikalini mwake......... je wamemsaidia kwa chochote au wamemuangusha?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom