Wanasiasa wasijikoshe kwa kumjengea sanamu Hayati Magufuli, badala yake wamuenzi kwa kuwa wazalendo na wachapakazi

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Binafsi naomba niwe tofauti kuhusu suala la Magufuli kujengewa sanamu pale sabasaba.

Magufuli sasa hayupo hivyo hakuna wa kumsemea leo nimejaribu kuvaa viatu vyake ,naamini kama angekuwa hai hasingeafiki swala hili ingewataka wale waliotenga pesa za sanamu wazielekeze kwenye miradi ya kiuchumi ya kuwakomboa wananchi.

Namkumbuka Magufuli vizuri alikuwa sio mtu wa kupenda sana kujikweza bila shaka angependa kuona hawa viongozi wetu waache kumuenzi kwa njia ya sanamu badala yake wawe wazalendo ,wachapakazi na watangulize maslahi ya Taifa sio matumbo yao binafsi.
 
Kama ni Sanamu Wanaotaka Kulijenga basi Wachange Hera Zao , Sio za Wavuja Jasho. Hata kila Mkoa wakichanga Hera zao Wajenge tu Hakuna shida, ila kutumia hera ya wavuja Jasho huku mahospitali yako Tahabani; No Thank you kwa Watanzania Wanyonge.
 
Si mlikuwa mnamtukana Magufuli?

Si mlisema mama anaupiga mwingi na sasa ufipa mnapumua?

Season ya nyumbu migration imeanza rasmi
 
Back
Top Bottom