Wanasiasa wanaojaribu kutumia udini na ukabila wataingamiza nchi jamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa wanaojaribu kutumia udini na ukabila wataingamiza nchi jamani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ibange, Jun 12, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watanzania hatujawahi kuwa na udini na ndio maana Mwl alifanya kazi na waislamu vizuri na ukweli ji kwamba wazee wa kiislamu ndio waliompa urais. Hakukuwa na ukabila maana mwl ambaye ni mbara asingeweza kupewa urais na wazaramo. Jiulize, hivi hawa wazee hawakuwa na vijana wakawapa madaraka badala ya kumchukua mbara?

  Sasa akina Mukama wanavyojaribu kutumia ukabila na ukanda kwa maslahi ya muda mfupi hawajui wanaliangamiza taifa? CCM wanavyojaribu kutumia udini ili wabaki madarakani hawajui madhara yake? Kujenga ukabila, ukanda au udini kwa ajili ya maslahi ya muda mfupi ni rahisi ila kuondoa ukabila na udini itatuchukua karne kadhaa hasa katika mfumo wa vyama vingi. Kenya imeshindikana kuondoa ukabila kabisa, sisi Tz hatuoni? Watanzania wenzangu tuwe macho na mazezeta wa kisiasa ambao wanatafuta ugali wa leo ili Tz iangamie kwa karne nzima
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nakushauri rudi tena skuli ukasome uzuri sana historia ya Tanganyika na ukanda mzima wa Afrika mashariki wakti wa ukoloni na makovu na athari za ukoloni kwa nchi husika.

  Nitakupa kidogo sana hapa. Wakti wa Ukoloni wa waingereza, walitumia divide and rule katika kuzitawala nchi hizo. Kwa upande wa Kenya na Uganda kwa kuwa kulikuwa na makabila machache sana lakin raia wake takriban kwa asilimia kubwa walikuwa wakristo. Huko walitumia Ukabila. Na hicho mpaka leo kinawasibu sana. Ukabila kila pahala.

  Kwa Upande wa Tanganyika ambayo kwa wakti huo ilikuwa na makabila zaidi ya 70. hapo walitumia UDINI. kwa maana ya kuibeba dini moja dhidi ya nyingine. Ni hilo kovu si rahisi kufutika mpaka leo kama utaangalia katika ramani ya Dunia Tz inaitwa ni christian country. UDINI huo ni donda la kuwasibu kama hamkufuatilia historia.

  Siku zote waswahili wanasema aliyelala usimwamsha na ukimwamsha ...Sasa waislam nao wameamka. kazi kwenu.

  Ombi langu usimsingizie Mukama bali hilo ni kovu na athari za ukoloni wa waingereza.

   
 3. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nonesense, Wale wale wanaofikiri kwa kutumia matumbo!!
   
Loading...