Wanasiasa wameshindwa na wamechoka kuiongoza Tanzania,ni zamu ya wengine sasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa wameshindwa na wamechoka kuiongoza Tanzania,ni zamu ya wengine sasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Godwine, Feb 20, 2012.

 1. G

  Godwine JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Taifa limepoteza uelekea,limekufa kiuchumi,kitamaduni na kisiasa pia , wanasiasa wanatawala kila sehemu bila ya kujali ni za kitaaluma na si za kisiasa.Siasa imeleta utumwa na kusababisha wizi wa rasilimali za taifa unaofanywa na wageni, siasa imefanya watanzania kuwa watumwa katika taifa lao,


  Siasa inadidimiza kila sekta na kutaka yenyewe ndiyo iwe inaamua kila kitu, tumeiachia siasa itawale lakini inaendelea kuua watanzania. Ukosefu wa ajira na kunasababishwa na mipango mibaya ya wanasiasa.

  kukosekana kwa huduma mbovu za afya zinasababishwa na wanasiasa kwani wao wataenda kutibiwa India na ulaya,Siasa imefika wakati wa kuchukua maisha ya wanasiasa kwa mauaji ya wao kwa wao kwa kutumia sumu na ujambazi. wakimaliza kuuana wao watakuja kumalizia na kuleta vita kwa wananchi wa kawaida.

  Ni wakati wa kutafuta njia mbadala ya kuepuka matatizo yanayotaka kuletwa na siasa na wanasiasa katika taifa letu, na njia hii ya mabadiliko na kuwanyanganya wanasiasa Panga la kutukatia unayo wewe na sisi.


  Nini kifanyike kuokoa Taifa kutoka kwa wanasiasa? nani wa Aliongoze Taifa tukiwanyang-anya wanasiasa?
   
 2. k

  king11 JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Katiba inatambua wananchi ndi wenye nguvu na mamlaka .kama wameona wanasiasa wameshindwa njia ni moja kuwanyanganya madaraka na kuwapa watendaji
   
Loading...