Wanasiasa waliosingiziwa sana ni Kawawa, Lowassa na Ridhiwani pia wanasiasa waliosingizia sana ni Dr Slaa na Tundu Lissu!

Wakati tuliokuwa nao ni wachama kimoja ama vingi,situnasema tumewafuta walinzani keanu walituchelewesha ama miss umeniacha.?
 
Riziwani alikuwa na majengo ,mahotel ,kampuni za.mafuta ,mabasi daaah yote hayo alipewa na wanachi enzj za babake akiwa rais

Ila wakati babake anastaafu tu wakampokonya Kila kitu wanamuachia ubunge
Anamiliki kila kitu
 
Lowassa alisafishwa na mwanasheria mkuu wa Chadema mh Tundu Lisu mnamo mwaka 2015 pale viwanja vya jangwani.

Tundu Lisu ndiye aliyeandaa ile orodha ya mafisadi iliyosomwa na Dr Slaa pale Mwembe Yanga!
Sasa ivi yuko CCM japo alijinyea
 
Yaani huyu jamaa kila uchao anazidi kujishushia hadhi hapa jamvini kwa tungo zake zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 
Moja kwa moja kwenye pointi ni kwamba kama kuna wanasiasa waliosingiziwa sana kwa habari za uongo nchi hii basi ni Kawawa rip wakati wa chama kimoja na mzee Lowassa na Ridhiwani Kikwete wakati wa vyama vingi.

Na wanasiasa wanaoongoza kwa kuwasingizia wenzao habari za uzushi ni Dr Slaa na Tundu Lisu na hasa baada ya kusimama pale Mwembeyanga na kuwashushia tuhuma za kutunga tu wanasiasa zaidi ya 10.

Sikushangaa pale Rais mstaafu Kikwete aliposema Chadema ni kiwanda cha uwongo.

Maendeleo hayana vyama!
.
JamiiForums316873384.jpg
FB_IMG_1581491063368.jpg
 
Moja ya thread za kijinga sana kupata kujadiliwa JF.
Ukisingiziwa unakuwa umevunjiwa hadhi yako (defamation) na kwa sheria za nchi unayo nafasi kufungua shauri mahakamani ili aliyekusingizia awajibishwe na kukufidia.
Kwa nini walio singiziwa hawakwenda mahakamani hadi mtoto wao johnthebaptist aje awasafishe JF?
Mwizi ukimwita mwizi na kusema kaiba ng'ombe 10 wakati aliiba 4 hawezi shtaki kwani ukiambiwa udhibitishe utaishia ng'ombe wanne na hilo halimuondelei kosa la wizi wala wewe uliyetaja 10 halikuhukumu kwani bado yule ni mwizi ila ulikosea kiwango cha wizi wake!
Tundu Lissu alishamsafisha Mzee Lowassa na Msigwa alishamsafisha Mzee Kinana.
 
Moja kwa moja kwenye pointi ni kwamba kama kuna wanasiasa waliosingiziwa sana kwa habari za uongo nchi hii basi ni Kawawa rip wakati wa chama kimoja na mzee Lowassa na Ridhiwani Kikwete wakati wa vyama vingi
2025 ni mbali sana, mtuache tupumue. Afterall riz hafai kuwa rais sawa na imitation yake
 
Hujamkuta Kambona na Nyerere wewe...
Yani Kambona aliimbiwa hadi nyimbo za chekechea...
Idd Amin na Nyerere.. hadi leo kuna watu hawamjui Amin lakini wanamchukia..

Siasa za uongo na propaganda ni za dunia nzima toka vizazi
Kambona ha ha × 2
Kambona ameolewa
Wapi ha ha × 2
Wapi
Huko Ulaya

Ziliimbwa sana kwenye majeshi/mchakamchaka
Cold war ni propaganda tu kati pande mbili hasimu.
Wanaosema ubeberu mawazo ni yaleyale utopian idealism wakisahau hata ndani ya nyumba kuna ubeberu!
 
Miaka ya Mwinyi kila kitu alisingiziwa Mama Sitti Mwinyi na Cleopa Msuya hadi Yale ma Gari aina ya DCM tukadanganywa maana yake David Cleopa Msuya
Huyo ndo mwanaadamu akishapenda au kukichukia kitu hashindwi cha kufanya Umewahi kujiuliza kwann kifo cha mende kiwe maarufu kuliko mende mwenyewe akiwa hai ? Wajuzi wa mambo hebu tujadilini kwa Maarifa sio hisia
 
Na wanasiasa wanaoongoza kwa kuwasingizia wenzao habari za uzushi ni Dr Slaa na Tundu Lisu na hasa baada ya kusimama pale Mwembeyanga na kuwashushia tuhuma za kutunga tu wanasiasa zaidi ya 10.
umesahau baba lao mchungaji Msigwa,mpaka lilikiri hadharani kwamba ni liongo la kutupwa
 
Back
Top Bottom