Wanasiasa Wababe Mwisho Ndio Huu? Wajuzi Tupeni Tafsiri

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,795
71,214

Huyu kiongozi alikuwa mbabe hakuna mfano. Tunaweza kumuweka katika category ya kina Hitler, lakini hukumu yake ilionyesha kabisa ubabe ulifikia mwisho.
Najua JF inayo hazina ya wajuzi wa lugha, tupeni tafsiri ya nini Saddam alikuwa anasema hapo
 

Huyu kiongozi alikuwa mbabe hakuna mfano. Tunaweza kumuweka katika category ya kina Hitler, lakini hukumu yake ilionyesha kabisa ubabe ulifikia mwisho.
Najua JF inayo hazina ya wajuzi wa lugha, tupeni tafsiri ya nini Saddam alikuwa anasema hapo
Libya raia wake wajinga, walimwona saddam kama mbabe sawa kabisa na wewe unavyomchukulia, but walibya wanajuta sasa hivi, wanasaka maiti yake wakaiombe msamaha ila haiwezekani tena. Wazungu washafanya yao wamewaachia mgofu na mashimo ya mabomu
 

Huyu kiongozi alikuwa mbabe hakuna mfano. Tunaweza kumuweka katika category ya kina Hitler, lakini hukumu yake ilionyesha kabisa ubabe ulifikia mwisho.
Najua JF inayo hazina ya wajuzi wa lugha, tupeni tafsiri ya nini Saddam alikuwa anasema hapo
Acheni ushabiki wa kimagharibi na hawa watu wabaya, soma kwa makini hii hotuba ya ghadaffi then ukimaliza fikiria walibywa wanavyoteseka sais, that is the price of democracy

QADAFFI ANAANZA HIVI:

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....

Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.

Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.

Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.

Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.

Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.

Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).

Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.

Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.

Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.

Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.

Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"

Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.

Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.

Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.

Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!

Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.

Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.

Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.

Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.

Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru.

-- Mu'uammar Qaddafi.
 
Libya raia wake wajinga, walimwona saddam kama mbabe sawa kabisa na wewe unavyomchukulia, but walibya wanajuta sasa hivi, wanasaka maiti yake wakaiombe msamaha ila haiwezekani tena. Wazungu washafanya yao wamewaachia mgofu na mashimo ya mabomu
Kwi kwi kwi! Jamani njooni msome post hii, huyu sio jiwe mwenyewe kweli? Tunaweza kuwa tumegundua ID yake.
Elli, Salary Slip, Retired, G Sam
 
kuwapulizia sumu wakurd , ambako wanazuoni wanaona hakuna tofauti na ubomoaji wa nyumba za kimara - mbezi , ndio kulinda malighafi za nchi zisichukuliwe na mabepari ?
Hakuna aliyepuliziwa sumu, ndugu yangu mzungu akikutaka atasema mambo mengi tu kukuhusu na ulimwengu utaaminishwa hivyo akati ni uongo
 
Back
Top Bottom