Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,383
- 38,653
Nilipoona Post hii ya Barbarosa nikaona limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa "wanasiasa" wa Jf wakiwa kwenye minyukano yao ya hoja kufikia jitmai la kuandika kuwa matendo, hoja, mitazamo, hisia ama chochote kile dhaifu ni alama ya mwanamke!Anaonyesha jinsi alivyo dhaifu, maneno kama hayo husema Wanawake pale wanapoachana na wapenzi wao, hivyo ni mambo ya kike tu!
Sisi sote tunafahamu kwamba mwanamke ni alama ya ushujaa, uvumilivu, uzazi, ulezi, na mwendelezo na ni mwanamke ndiye anayeifanya dunia kuwa hivi ilivyo hivi sasa. Iwe kwa Silka ama kwa hulka yake!
Kwenye siasa za Tanzania wanawake ndiyo wameifanya CCM kuendelea kuwa madarakani mpaka hivi sasa, halafu anakuja shabiki wa CCM anatoa maneno ya dharau dhidi ya wanawake, inasikitisha sana. wanawake ni viumbe adhimu sana lazima waheshimiwe!
Hivi kama wanawake ni dhaifu kama kada barbarosa anavyotaka kuonesha wangeweza kushinda shambani wakilima kwa majembe ya mikono mchana kutwa wakati wanaume zao wako vilabuni wakinywa Pombe. Wanawake hawa "dhaifu" wamewezaje kutembea zaidi ya kilomita kadhaa kufuata maji ama zahanati zilizo mbali na mahali wanapoishi?
Wanasiasa wa JF heshimuni wanawake kama hoja zimewaishia kaeni kimya!!