Wanasiasa wa CCM mbumbumbu wa ujasiriamali wa siasa

  • Thread starter kennedy lufulondama
  • Start date

K

kennedy lufulondama

New Member
Joined
Dec 8, 2012
Messages
2
Points
0
K

kennedy lufulondama

New Member
Joined Dec 8, 2012
2 0
WANASIASA WA CCM MBUMBUMBU WA UJASIRIAMALI WA SIASA.

Kama ilivyo katika biashara kuwa biashara bila ujasiriamali (ubunifu) hakuna biashara na vilevile siasa bila ujasiriamali hakuna siasa. Vilevile kama ilivyo katika biashara kuwa lengo lake kuu ni kutengeneza faida na katika siasa vivyo hivyo lengo lake ni faida tofauti kati ya hivyo viwili ni hali na jinsi faida inavyotengenezwa katika haya maeneo mawili yaani Biashara na siasa.
Hakika, nawasikitikia Wabunge wa Chama Tawala cha CCM kwa kushindwa kutambua kuwa siasa nayo kama ilivyo biashara ni eneo linalohitaji ujasiriamali ili kuweza kukua kama ilivyo kwa biashara.
Hali hii imekuwa ikitokea tangu Bunge la bajeti la mwaka 2011/2012 na 2012/2013 pale Wabunge wa Chama Tawala waliposhindwa kuwakilisha maslahi ya wapiga kura wao katika Bunge la bajeti wakati wa kujadili makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na madini. Pia hali ilijitokeza pale kiongozi mkuu wa kambi rasmi Bungeni, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Hai na Kiongozi mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mh. Freeman Aikael Mbowe alipomhoji Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda umuhimu wa kutungwa kwa sera ya Taifa ya matumizi na Mh. Pinda kutotilia maanani kuwepo kwa sera hii kama njia ya kuipa fursa serikali kuzuia matumizi yasiyo na tija yanayofanyika katika ofisi za umma, matumizi yanayopunguza bajeti ya maendeleo ya wananchi. Kama nilivyogusia hapo juu kuwa siasa kama ilivyo kwa biashara ni eneo linalohitaji taaluma ya ujasiriamali ili kujua aina ya faida na namna ya kutengeneza faida hiyo. Tofauti na biashara, katika siasa, faida ni imani ya wapiga kura kwa kiongozi wa Chama husika cha siasa na ujenzi wa imani hii ya wananchi kwa mwanasiasa wa Chama husika cha siasa ni shughuli kati ya posho za waheshimiwa wanasiasa wakiwemo wabunge na mawaziri na bajeti ya miradi ya maendeleo ya wananchi. Maana yake ni kwamba bajeti miradi ya maendeleo ya wananchi ambayo ndiyo chachu ya imani ya wapiga kura kwa mwanasiasa husika na Chama chake cha siasa hutegemea ukubwa wa posho (matumizi ya kawaida ya serikali) za wanasiasa hasa Wabunge na Mawaziri na wengineo walio katika muundo wa utawala.
Kama posho za waheshimiwa ni kubwa basi bajeti ya maendeleo ya wananchi inapunguzwa na posho hizo na kuwa ndogo na hivyo kushindwa kukithi matarajio halali ya wapiga kura walio wengi. Mfano bajeti katika miradi ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi mfano ujenzi wa madarasa, maktaba na maabara katika shule pamoja na huduma mbalimbali za ugani kwa wakulima na wafugaji pamoja na huduma za miundombinu ya uzalishaji mali. Na kama posho za waheshimiwa ni ndogo basi bajeti ya maendeleo ya wananchi inakuwa kubwa na kuweza kukithi matarajio ya wananchi wapiga kura walio wengi na hivyo faida ya mjasiriamali wa siasa ambayo ni imani ya wapiga kura walio wengi kwake inapanda juu kwani matarajio ya walio wengi ambayo ni maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu ya kiuchumi inakuwa bora. Wabunge na wanasiasa wa CCM wanashindwa kuielewa vizuri nadharia ya ujasiriamali katika siasa kwa kushindwa kujua faida katika siasa ni ipi na namna faida hii inavyotengenezwa kama nilivyofafanua hapo juu. Lakini kama ilivyo katika ujasiriamali wa biashara kuwa nadharia ya ujasiriamali huanza na uamuzi wa aina ya biashara na kiasi cha faida anayotaka kutengeneza mjasiriamali. Na mafanikio ya huyu mjasiriamali yanategemea uzuri wa maamuzi ya aina ya biashara na faida anayotaka kutengeneza mjasiriamali. Na maamuzi mabovu ya aina ya biashara na kiasi cha faida atakachofanya mjasiriamali awe wa biashara au siasa matokeo yake ni gharama za kimaamzi (opportunity cost). Na mjasiriamali bora awe wa siasa au wa biashara, kabla ya kufanya maamuzi ya aina ya biashara na kiasi cha faida anachotaka kutengeneza lazima ampatie vizuri nadharia ya kwanza ujasiriamali ambayo ni gharama za kimaamuzi na kwa kimombo wanadai (opportunity cost) kuwa kubwa. Nadharia ya gharama za kimaamuzi ndiyo mhimili wa ujasiriamali iwe ni katika biashara au siasa, kwani ndiyo hubeba Dira na Dhamira ya biashara au siasa, na nadharia hii inasisitiza nini mjasiriamali awe wa siasa au biashara atapata au kukosa kwa uamuzi wa kufanya au kuacha kufanya jambo Fulani kwa wateja au wapiga kura wake. Hapa ndipo pamekuwa pagumu kwa wanasiasa na chama cha mapinduzi. Ugumu wa hapa ni uamzi wa kuachana na posho kubwa hasa kwa wabunge na mawaziri na wote waliopo katika mfumo wa utawala. Wanasiasa hawa wamesahau kuwa matarajio ya wapiga kura wao ni maendeleo yanayohitaji mapesa mengi na ili bajeti ya miradi ya maendeleo iwe juu hakuna budi kuwa bajeti ya matumizi ya kawaida yaani posho na Mishahara ya Waheshimiwa yapungue kwa kiasi kikubwa. Katika hili makosa ya wanasiasa hawa wa CCM ni ya kimaamuzi (opportunity cost) ambayo ni kushindwa kujua kuwa ni nini watapata kwa kukumbatia posho kubwa kutoka kwa wapiga kura wao walio wengi wanaohitaji maendeleo na nini watapata kwa wapiga kura wao kwa kutokukumbatia posho kubwa pengine imani ya wapiga kura wao kwao kuongezeka . Hali hii iliwakumba wanasiasa hawa na kuwafanya washindwe kufanya maamuzi mazuri yanayolenga kuwawezesha wapiga kura wao kuwa na imani nao pale walipokataa pendekezo la kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Mh. Freeman Aikael Mbowe alipotaka kuwepo na sera ya Taifa ya matumizi “ THE NATIONAL EXPENDITURE POLICY” itakayoweka mwongozo wa jinsi rasilimali za umma zitakavyowatumikia watanzania katika kuwaondoa katika umasikini na kuwaletea maendeleo endelevu.Kimsingi, mantiki ya pendekezo la Mh. Freeman Aikeal Mbowe lilikuwa ni kuzuia matumizi ya fedha za umma katika matumizi ya serikali yasiyo na tija kwa walipa kodi mfano fedha za EPA na ununuzi wa Rada, ambayo hata hivyo rada hiyo ilishindwa kuziona ndege za uarabuni zilizotua katika ardhi ya Tanzania na kuchukua nyara za Taifa kama vile Twiga na Faru n.k. Mategemeo ya walio wengi katika hoja hii ya Mh. Freeman Mbowe ilikuwa ni serikali kulikubali pendekezo la Mh. Mbowe kwani lengo la hoja yake ilikuwa ni kuiwezesha serikali kuachana na matumizi yasiyo na tija kwa wananchi. Na kwa kuwa wanasiasa wa CCM walilikataa pendekezo hili lililolenga kuwaongozea imani ya wapiga kura wao kwao ni hakika walishindwa kujua biashara wanayofanya na kiasi cha faida walichotaka na kudhihirisha kuwa dhana ya wao kuwa mbumbumbu wa ujasiriamali wa siasa ni kweli. Vilevile hali ya wanasiasa hawa kutojua aina ya faida na kiasi cha faida na maamuzi yasiyo na gharama kwao ilijitokeza tena katika Bunge la bajeti mwaka 2011/2012 na 2012/2013 pale walipopiga kura nyingi za kupitisha bajeti ya serikali ambayo haikuwa na fedha za kutosha katika miradi ya elimu, maji, afya na miundombinu ya uchumi hasa katika kujenga miundombinu ya masoko kwa mazao ya wakulima wa pamba waliouza pamba yao kwa Tshs 600/= badala ya 1500/= za mwaka jana na kujikuta wanazomewa majimboni mwao. Yote hayo ni kutokujua ujasiriamali wa siasa kuwa ili imani ya wapiga kura kwao iwe juu ni lazima waamue kuitelekeza serikali na Chama chao kilichopoteza dira katika kuondoa kero za watanzania. Nikijiandaa kumalizia makala yangu, najisikia kuwa nisiye na fadhila kama sitawapongeza Wabunge wa CHADEMA walioipinga serikari katika bajeti yake ya tangu 2011/2012 na 2012/2013 kwani kijasiriamali, bajeti hiyo haikulenga kuwajengea imani ya wapiga kura wao kwao na kwa sababu makamanda hawa ni weledi katika ujasiriamali wa siasa ndiyo maana waliikataa kwa nguvu zote. HONGERENI MAKAMANDA. IMEANDIKWA NA: KENNEDY LUFULONDAMA MWANAHARAKATI WA MASUALA YA HIFADHI YA JAMII.
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
23,907
Points
2,000
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
23,907 2,000
Ulale mahala pema peponi mleta thread. raha ya milele umpe ee bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani. AMINA
 

Forum statistics

Threads 1,285,566
Members 494,675
Posts 30,866,928
Top