Wanasiasa wa CCM fanyeni utafiti kabla ya kuongea

WANASIASA WA CCM FANYENI UTAFITI KABLA YA KUONGEA.

Wakati wa uzinduzi wa bomba la mafuta huko Tanga, watanzania wamedanganywa na kuaminishwa kuwa bomba linalojengwa Tanga lenye urefu wa km 1445 ni refu kuliko yote duniani...!! Mbaya zaidi hata magazeti nayo yameandika hivyo hivyo bila hata kufanya utafiti na kuhoji, hii inathibitisha aina ya waandishi wa habari tulionao katika Taifa hili.
Naomba niweke kumbukumbu sawa baadhi ya mabomba ya mafuta marefu duniani:

1. Eastern Siberian to Pacific Ocean (ESPO) Oil pipeline lina urefu wa Km 4900.

2. International Crude Oil pipeline Edmonton Alberta kupitia Chicago lina urefu wa km 3787.2

3. Dar es salaam to Ndola Zambia pipeline lina urefu wa Km 1705.

Inakuwaje bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda to Tanga Tanzania lenye urefu wa Km 1445 liwe refu kuliko yote duniani? Jamani tutaendelea kudanganywa na Wanasiasa hadi lini? Watanzania siyo wajinga kwa kiasi hicho...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
PUSHING GRAVITY;
wide per INCH
Technolohy ya Bomba ; kama ukitumia techonology za ayo ya zamani; lingeenda umbali mrefu
 
Back
Top Bottom