Wanasiasa Vijana Wapewe Washauri wa Kisiasa nchini Tanzania

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,640
516
Heshima zenu wote wanabodi wa vyama vyote, Kwa kweli nianze kukiri kwamba uwezo na muelekeo wa vijana katika siasa za Tanzania umekuwa ukikinzana sana na taaluma na maadili ya siasa yenyewe nchini na kutofautiana na wazee.

Ikumbukwe kwamba majuzi tu, vijana wa CCM wamekuja na kauli za kutaka umri wa uraisi urudishwe nyuma, yaani wagombeaji wawe waliozaliwa baada ya uhuru.

Hili suala lilileta hisia mbalimbali katika jamii ya kitanzania kwa kuzingatia kwamba kijana aliyesema hayo maneno ni kiongozi wa ngazi ya juu kabisa katika serikali. Kabla ya hapo, mwenyekiti wa BAVICHA mkoa wa Tanga naye amekuwa akijinadi kuwania uraisi bila hata kufuata taratibu za chama chake.

Kwa kuongezea, naibu katibu mkuu wa CDM naye amekuwa bega kwa bega na kauli yake ya kutaka kuwa raisi bila kujali katiba wala kanuni za chama chake.

Hii ni mifano michache sana katika vyama vya siasa nchini ambavyo vijana wajiaona kupevuka kwa sababu kwa vipimo vyao wenyewe na wala vya vyama au wananchi. Hii inapelekea wanasiasa wanaobwatauka tu bila kufikiria kabisa, wapiga kelele na wachumia tumbo tu.

Hii ndo inayopelekea vijana kukosa uvumilivu na mbinu za kukabiliana na changamoto za kisiasa nchini na kupelekea kurubuniwa kiraisi sana.Najua wanaJFs wana mifano mingi ya vijana wa namna hii katika siasa za nchi yetu.

Kwa hiyo, ninatoa wazo kwamba mwanasiasa yeyote kijana apewa mshauri/ msimamizi wake katika siasa ambaye atamshauri na kumlea katika harakati za kisiasa ili kuwajengea uwezo wa kupambanua mambo katika uwezo na uzoefu mkubwa.

Njia hii hutumiwa sana na chama cha ANC cha Afrika ya Kusini, kwa kuchukulia mfano, Julius Malema alikuwa chini ya uangalizi wa Winnie Madikizela-Mandela.

Nawakilisha wanabodi.
 
Heshima zenu wote wanabodi wa vyama vyote, Kwa kweli nianze kukiri kwamba uwezo na muelekeo wa vijana katika siasa za Tanzania umekuwa ukikinzana sana na taaluma na maadili ya siasa yenyewe nchini na kutofautiana na wazee.

Njia hii hutumiwa sana na chama cha ANC cha Afrika ya Kusini, kwa kuchukulia mfano, Julius Malema alikuwa chini ya uangalizi wa Winnie Madikizela-Mandela.

Nawakilisha wanabodi.......


hao washauri watatakiwa wawe ni wazee
?kama ndivyo mimi mshauri wangu atakuwa mzee Wassira.
 
ondoa jina la zitto maana yeye anajua kila kitu..waliozaliwa kabla ya 1961 hawana akili kwa mujibu wake labda kama ni waganga wa kienyeji atawasikiliza
 
Ni wazo zuri. lakini nani atawathibitisha washauri? Bora tungesema kuwa kuwe na Institute ambayo vijana/wanasiasa wote watapitia kwa mujibu wa sheria. Ili kuwe na uniformity and acceptable standards of skills which can also be revised/assessed.
lakini tukisema wawe na uangalizi - wengine watakuwa chini ya waganga (lol)
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom