Wanasiasa vijana wanatusaidia vipi kupambana na changamoto nchini

Makame

JF-Expert Member
Jan 3, 2008
512
60
Tanzania ina matatizo mengi. Miongoni mwao ni yale matatu ya ASILI kutoka kwa Baba wa taifa ambayo ni (1) Umaskini; (2) Ujinga na (3) Maradhi. Haya ymeendelea kuwepo kwa kuwa na yafuatayo:-

a) Kuendelea kuwepo kwa RUSHWA.
b) Kuendelea kukumbatia ujinga wa kuchakachua - vyeti vinachakachuliwa [Mpaka Waheshimiwa Mawaziri!]; Mafuta, Mitihani, mabenki nk!
c) Siasa kugeuzwa mtaji wa kuneemeka na sio kuwatumikia wananchi.
d) nk

Sidhani kama kauli za kujivuna kwa mfano 'ninajijenga mwenyewe' zitatusaidia na dhamira ya kupambana na maadui watatu wa Taifa letu. Tutimie jitihada kuweza kufikia malengo na sio kupotezeana muda.

Sasa swali langu, je wanasiasa hawa vijana wanatusaidia au tutaendelea na uozo tulioukuta kutoka kwa elder generation?
 
Te te teeh!..we acha kuchokoza ugomvi,watu walimsahau mpaka Shibuda.
 
Hakika hili ni tataizo jipya la Taifa,tizama vijana walio serikalini na vyama vya siasa baadhi wameanza kuonyesha dalili ndizo sizo zinazoleta maswali lukuki kuwa siasa zetu za kizazi hiki cha vijana wa sasa ni janga jipya tena hatari kuliko la mafisadi.
 
Hapa mkuu ndio wakati wa sie vijana kua makini sana na kauli ya baadhi ya viongozi vijana ya kutaka kutupotosha kwa kauli zenye utata mfano kauli za zitto juu ya kutuhumu uongozi wa juu Publically while kuna taratibu za kupresent matatizo yake ndani ya Chama kwa hyo tuwe makini sana juu ya hizi kauli mbali na hapo watataka kutuvuruga sie vijana lakn cha msingi tusimamie kile tunachokiamini
 
HAWA VIONGOZI WAKISHAFIKA HUKO MJENGONI AU WAKIKAMATA DHAMANA ZA KITAIFA WANASAHAU KWAMBA WANA UWAKILISHI WA VIJANA AMBAO NI WENGI KWENYE JAMII NA WANAENDELEZA UOZO.

DAWA

SIJUI MUARUBAINI WETU TANZANIA UKO WAPI

Wengine wanasingizia MUUNGANO
 
Tatizo la kuwa kijana iwe kwenye siasa au popote pale inakubidi kwanza ucheze na sheria zilizopo kabla hujaweza kuzibadilisha. Msitagemee vijana waingie na moja kwa moja waende kinyume kabisa na michezo ya wazee kwani hao wazee ndiyo wanao wapa nafasi kwa kuanzia.
 
Kwa maana nyengine Mheshimiwa Mwanafalsafa unatuambia kwamba

'If you cannot beat them ...... Join them'

Viongozi vijana wengi wanasumbuliwa na ulimbukeni na kudhani wao ni bora kuliko wengine wote kwa kuwa wapo kwenye uongozi wa vyama vya siasa.

Maneno ya majigambo yamekuwa mengi sana kiasi ya kutia shaka iwapo wanadhamira ya kutumikia watu au ni maslahi binafsi.

Viongozi vijana tungewategemea kuwa na maadili yanayompasa kiongozi kwa vile wana exposure kubwa zaidi, lakini kinyumechake wamekosa utashi na kukiuka maadili na miko kwa kile wanachokiita transparency kwenye demokrasia
 
Tanzania ina matatizo mengi. Miongoni mwao ni yale matatu ya ASILI kutoka kwa Baba wa taifa ambayo ni (1) Umaskini; (2) Ujinga na (3) Maradhi. Haya ymeendelea kuwepo kwa kuwa na yafuatayo:-

a) Kuendelea kuwepo kwa RUSHWA.
b) Kuendelea kukumbatia ujinga wa kuchakachua - vyeti vinachakachuliwa [Mpaka Waheshimiwa Mawaziri!]; Mafuta, Mitihani, mabenki nk!
c) Siasa kugeuzwa mtaji wa kuneemeka na sio kuwatumikia wananchi.
d) nk

Sidhani kama kauli za kujivuna kwa mfano 'ninajijenga mwenyewe' zitatusaidia na dhamira ya kupambana na maadui watatu wa Taifa letu. Tutimie jitihada kuweza kufikia malengo na sio kupotezeana muda.

Sasa swali langu, je wanasiasa hawa vijana wanatusaidia au tutaendelea na uozo tulioukuta kutoka kwa elder generation?

Mkuu nadhani jibu unalo tayari. Kama vijana wenyewe ndo akina Nape, January, Kawawa Girl etc ni pumba na utumbo mtupu wanachojua ni mipasho na maslahi ya chama na sio nchi, unategemea nini? Hii nchi ni kwishney, mpaka tuchinjane ndio tutashikishana adabu otherwise just forget it!!!
 
Kwa maana nyengine Mheshimiwa Mwanafalsafa unatuambia kwamba

'If you cannot beat them ...... Join them'

Hapana. Nasema it takes time. Vijana hao wanabidi waongezeke kwa idadi na kupata nyadhifa mbali mbali kabla ya kuleta mabadiliko.
 
Back
Top Bottom