Wanasiasa vijana CCM awamu hii mnatuangusha, hasa mawaziri. Mko kimya kama hampo!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,160
2,000
Kuna waoamini katika kitenda kwingi lakini kusema kidogo, Pamoja na hivyo lakini mbona hata kutenda kwenyewe hakupo wala kusema? Mnataka kusema kukaa kimya pekee ndio busara na hekima? Mmenaswa wapi Jamaa zangu ninyi?


Enzi za JK kulikua na wapiga siasa wengi ambao kwa sasa kimyaaa, huku kuna tatizo sio bure kabisa. Enzi hizo JPM alikua kimya sana lakini kwenye kazi alijulikana na sidhani kama kuna waziri anavunja rekodi yake na ndio kumempeleka alipo.

Tumezoea kwa mujibu wa somo la uongozi katika makundi hua kuna watu ambao huamsha makundi, kwenye siasa huongoza makundi na kua kama Identity za vyama. Kwa sasa CHADEMA yupo mpambanaji TUNDU LISSU,ACT yupo Zitto, CUF yupo Mtatiro. Hawa ndio walizibeba haswaa itikadi za vyama vtao. Sasa mimi nizungumzie upande wa Serikali ni kijana gani anayejibambanua tusema sasa huyu anatembelea viatu vya JPM enzi hizo?Ni nani?Labda Makonda japo nililenga zaidi upande wa mawaziri kijana.


Wapi Mwigulu Chemba, Kigwa, J Makamba, Wapi Luhaga Mpinga?
Labda kidogo Suleiman Jaffo.

Utenda wa Serikali upande wa baraza la mawaziri kwa sasa Mwajibikaji ni LUKUVI, MBARAWA na kidogo HUSSEIN MWINYI.

Amkeni bhana msiisubirie 2025 bado ni mbali.
 

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
8,362
2,000
Luhaga mpina yuko vizuri anachapa kazi za kuendeleza taifa na jimbo lake la kisesa
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
42,508
2,000
Hawana uhuru wa kufanya wanachotaka
kiongozi wao hatabiriki...wanaenda kwa kusitasita wanatazama upepo
 

South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,494
2,000
Akijitokeza yeyote anazimwa haraka mana huyu mzee anataka kushine pekeake
 

NorthJuu

JF-Expert Member
Mar 19, 2017
387
250
We uafikiri baada ya mtanange wa Nape na bastola kuna Waziri kijana wa C..C.... wala ....M atafunguka tena! Ilianza mtishia mtu bastola, ikafatia Bunduki (Machine Gun) kwa yule mwingine, itakayofata labda itakuwa AK-47 na Grunnete au Missile.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom