Wanasiasa tujisahihishe ili tushinde uchaguzi ujao

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
6,509
2,000
Naomba kuchambua mbinu kuu atumiazo shetani kwa watu wake; “KUTOONA MAZURI” (Mathayo 13:14) “Kutazama mtatazama,lakini hamtaona” Chuki bila sababu au maamuzi mbele yaweza kumfanya mtu asione; Ukabila unaweza kumfanya mtu asione zuri kutoka kabila fulani, chuki ya chama kimoja yaweza isione uzuri ufanywao na chama kingine; (Yohane 1:46) “naye Nathanaeli akamwuliza Filipo,”Je,kitu chema chaweza kutoka Nazareti? Ubaguzi wa rangi unaweza kumfanya mtuasione jambo zuri kutoka watu wa rangi tofauti na yake, ingawa damu yao wote ni nyekundu; kutoona mazuri ni mbinu anayoitumia sana shetani,

Kuna bosi mmoja siku moja alikuwa anasikiliza malalamiko ya nawafanyakazi wake, ikiwa katika mjadala, akachukua karatasi nyeupe na kuweka alama nyeusi na kuwauliza nini, “mnaona nini? Wengi walijibu,”TUNAONA ALAMA NYEUSI TUPU BOSI; “Bosi akawajibu, “Mnaona alama nyeusi tu na hamuoni sehemu kubwa iliyo nyeupe? Chuki yao iliwafanya wasione kingine!

Mwenye chuki ukimpa glasi ikia na maji nusu; Atahoji kwanza kwanini “imejaa nusu”

UPINZANI SIYO KUPINGA KILA KITU; Tujifunze kuona mazuri, UTAWALA WA NYUMA; tulipiga kelele kuomba Viongozi wanakwamisha maendeleo “WATUMBULIWE” . Hakika hakuna Baba mwanaye amwombaye mkate akampa jiwe; Leo Rais wa jamhuri hasubiri kelele za Bunge; Anatumbua moja kwa moja, mnacholalamika ni nini? Mlichokiomba siku nyingi leo mmekisahau? Mbona mmekuwa na vigeu geu?

KUTOOKUONA MAZURI YA CHAMA TAWALA NI USHETANI;

Kila lifanywalo na chama Tawala ninyi mnapinga; ni lini mtasifia japo kidogo? U-mwamba si kujua kupinga tu, Hata kumsifu mpinzani wako ni u-mwamba pia; KOSOENI lakini msiache kusifu mazuri; ina maana mnapinga hata mambo muliyoyanadi wenyewe? Nini lengo lenu? Je; mnawapenda watanzania kweli? Kwanini mnakuwa wanafiki kiasi hichi? (Mathayo 13:13) “kwasababu hii nasema nao kwa mifano; kwakuwa wakitazama hawaoni,na wakisikia hawasikii,wala kuelewa”……(WAGALATIA 5:19-21) Basi matendo ya mwili ni dhahiri ndiyo haya, uasherati,uchafu,ufisadi, 20. Ibada ya sanamu,uchawi,uadui,ugomvi,wivu,hasira,fitina,faraka,uzushi……..21….Katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawaurithi ufalme wa Mungu.UFALME WA MUNGU KWA WAPINZANI NI KUIONA IKULU

NINI KIFANYIKE?

Mungu aliekeza ni namna gani watu wafanye ili wauone ufalme (kwa wapinzani-IKULU), Mungu anatusihi tujiepushe na hayo ili tufaidi mema ya nchi; (WAGALATIA 5:22) Lakini tunda la roho ni upendo,furaha,amani,uvumilivu,utu wema,fadhili na uaminifu.

WAPINZANI ni wakati sasa wa kubadili upepo wa siasa za chuki; kama mnaona kuna kunyanyaswa, Itisheni kikao cha amani na raisi, andaeni kongamano la amani, halafu mkaribisheni Raisi wa jamhuri, mwambieni kwa upole, sifieni mazuri yake, pongezeni mazuri yake! Ongeezeeni alipofikia; Hakikisheni siasa bora; Hakika Mungu atawainua; Mtapata kilicho chema; na mtachukua nchi mapema sana.

MIMI SINA CHAMA, LAKINI WAPINZA JARIBUNI KUJITAFAKARI NA SIASA BORA HUENDA MTATUVUTIA WENGI NIKIWEMO NA MIMI. KARIBUNI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom