Wanasiasa ni chui wawindaji na takukuru ni fisi wala mizoga!?!?

akajasembamba

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
256
250
TAKUKURU Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa au enzi zile ilikuwa Kikosi cha Kuzuia Rushwa. Chombo kinachoendeshwa kwa fedha lukuki za walipa kodi ili kipambane na Rushwa. Badala yake ninachokiona ni kuwa wanasubiri TUHUMA ziibuliwe Bungeni nk nk zizungumzwe weeeeeee na wanasiasa na wabunge, ndiyo na wao wanaenda ati Kuchunguza! Sijui ni ushahidi gani watakaoupata. Tuhuma za kina JAIRO, EPA, Meremeta,Twin Towers etc etc etc na hata huko Mikoani mpaka Madiwani katika Vikao vyao vya Halmashauri wamtuhumu Mtumishi fulani kwa kelele nyingi ndiyo TAKUKURU na wao wataitwa na Mkuu wa Mkoa au wa Wilaya au Mwenyekiti wa Halmashauri wachunguze!! Hivi tuhuma ambayo inakuwa imeshazungumzwa weeeee halafu chombo cha dola kinakuja baadae kuchunguza kitapata ushahidi gani? No wonder hawa jamaa wanabwagwa mahakamani kila siku! Kazi zao hazifanywi kama wachunguzi wanafanya kazi ya kusuburi tuhuma zilizoibuliwa na watu wengine, kazi ni kusubiri mishahara mwisho wa mwezi, wakifumbia macho rushwa na ubadhirifu wa aina zote mpaka Wanasiasa waibue tuhuma fulani nao ndiyo wanajifanya kwenda kuchunguza!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom