Wanasiasa nawaonya kwa mara ya kwanza. Hili Taifa ni mali ya watanzania na si mali yenu

Kuna watu wanajiona ni bora zaidi ya wengine wote bila kujua kuwa elimu yetu ndiyo tunu pekee ya kuongoza taifa letu.

Wanasiasa mnapojifanya hamuoni tatizo la ajira kwa vijana wetu mjiandae kuondolewa ofsini. Kama mnahisi kuwa mpo bora zaidi mnajidanganya.

Kununua magari yenu pesa zipo, kujenga nyumba zenu pesa zipo ila kununua vitabu pesa hakuna, kununua madawa hospital pesa hakuna, kuchonga madawati pesa hakuna. Endeleeni tu kuwa vipofu.
THE LOST, lost and gone in air.
CCM lazima wakuite wewe ni uchochezi...unachochea wananchi waichukia serikali yao...ambapo kwao ni kosa kisheria.
 
Wanasiasa mnapojifanya hamuoni tatizo la ajira kwa vijana wetu mjiandae kuondolewa ofsini. Kama mnahisi kuwa mpo bora zaidi mnajidanganya.

Kununua magari yenu pesa zipo, kujenga nyumba zenu pesa zipo ila kununua vitabu pesa hakuna, kununua madawa hospital pesa hakuna, kuchonga madawati pesa hakuna. Endeleeni tu kuwa vipofu.
Dawa ni kuwapunguza wale wanaojifungia Dodoma kwa kisingizio cha kutusemea kwa serikali, wakati serikali ina wawakilishi wake kila Mkoa, kila Wilaya, kodi zetu ndizo wanafanyia anasa badala ya fedha hiyo kwenda kwenye mambo ya msingi
 
Mkuu hakika haupo sawa kichwani! Wewe umeanza kunifatilia leo naona. Kwa taarifa yako nilimkosoa Magufuli akiwa hai na kamwe siwezi kumkosoa akiwa mfu. Kuwa na heshima, hata kama ningekuwa upande wa Magufuli bado hakunizuii kuwanyoshea kidole wanasiasa wa leo maana wote ni walewale wa mwendazake.
Very reasonable comment.
 
Hizi tawala zimekuwa za wazee kupeana ulaji ili waendelee kusinzia vizuri wakisubiri siku zao, ni muda mwafaka kwa vijana kushika hatamu....kuanzisha chama kitakachopitisha mgombea kijana (below 55) ambaye akiingia atateua watendaji na viongozi vijana.....wazee wabaki kwenye nafasi za ushauri....
 
Tanzania tunahitaji Raisi mwenye tafsiri sahihi kuhusu maisha!!je maisha yanahitaji nini zaidi?je ni hayo magari?majumba makubwa?au ni kitu gani????Maisha ni kuridhika ukiridhika utawatumikia watu vizuri!!!wizi,ufisadi na rushwa ni matokeo ya kutoridhika!!!Hamjachelewa fanyeni maamuzi sahihi!!wakati wenu ni sasa!!
 
Kura yenyee ni utaratibu tu Ila kurudi kwao ni kawaida. Then wanaimiza watu wawe wabunifuu vijana wafanye kazi na kuwa na udhubutu .🤓
Tuongeze ubunifu na uzalendo, na wanasema vijana wa siku hizi ni wavivu hawajitumi wajiajiri nchi ina fursa nyingi🤣
 
Kuna kikundi cha watu wachache wahuni ndiyo wanafaidi keki ya Taifa. Hawa wahuni hawafiki hata 5,000
Mahitaji yao yooteee yanatimizwa on time.

Wabunge wakimaliza tuu ubunge wanalipwa chao chap chap.

Akina sie kajamba nani sasa, utasaga makalio PSSSF/NSSF mpaka ukome.
 
Tanzania tunahitaji Raisi mwenye tafsiri sahihi kuhusu maisha!!je maisha yanahitaji nini zaidi?je ni hayo magari?majumba makubwa?au ni kitu gani????Maisha ni kuridhika ukiridhika utawatumikia watu vizuri!!!wizi,ufisadi na rushwa ni matokeo ya kutoridhika!!!Hamjachelewa fanyeni maamuzi sahihi!!wakati wenu ni sasa!!
Kiongozi aliyekuwa anaishi falsafa zake ni Nyerere tu, baasi.....waliofuatia na wateule wao ni upigaji kwenda mbele, hawana falsafa yoyote kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi na wananchi.
 
Kiongozi aliyekuwa anaishi falsafa zake ni Nyerere tu, baasi.....waliofuatia na wateule wao ni upigaji kwenda mbele, hawana falsafa yoyote kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi na wananchi.
Mkuu hata we ukipata channel utapiga tu
Dunia ya leo hakuna anayetaka kuwa nyuma

Ova
 
Mkuu hata we ukipata channel utapiga tu
Dunia ya leo hakuna anayetaka kuwa nyuma

Ova
Sasa unakuwaje kiongozi wa watu kama upo kwa ajili ya maslahi yako binafsi, usishirikishe kila mtu kwenye mawazo ya wizi na ubinafsi...
 
Sasa unakuwaje kiongozi wa watu kama upo kwa ajili ya maslahi yako binafsi, usishirikishe kila mtu kwenye mawazo ya wizi na ubinafsi...
Sawa....
Ngj upate channel lzm upige
Binafsi mm nikipata nafasi nawasha tu
Maslahi yangu kwanza mengine badaye
Sema nacheza kwa step

Ova
 
Back
Top Bottom