Wanasiasa na mtaala wa elimu

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Wanasiasa wa Tanzania wamekuwa ndio chanzo cha kushuka kwa elimu ya Tanzania, matokeo mabovu ya darasa la saba, kidato cha nne na kile cha sita chanzo ni wanasiasa. Na kumbuka Mh. Joseph Mungai alipokuwa waziri wa elimu alibadilisha kabisa mtaala wa elimu kwa kuunganisha baadhi ya masomo na kuwa somo moja kwa shule za msingi na zile za sekondari, hivyo hivyo na kuondoa masomo ya biashara kwa shule za sekondari. Hali hii iliwachanganya walimu na wadau wa elimu, naye Mh. Magreth Sitta alipo teuliwa kuwa waziri wa elimu akarejesha mtaala wa zamani na kuvunja utaratibu wa Mh. Mungai, kama vile haitoshi Profesa Jumanne Maghembe naye alipoteuliwa kuwa waziri wa elimu yeye hakubadilisha bali akaboresha kwa kupunguza baadhi ya mada na kuongeza mada zingine ambazo hazikuwepo kabisa. Pamoja na yote wanafunzi na walimu wanashindwa washike lipi na wafuate lipi? Kinachofuata ni kuporomoka kwa taaluma ya elimu na kuweka visingizio walimu hawatoshi.


Kubadilishwa kwa mitaala mara kwa mara ni chanzo cha kushuka kwa kiwango cha taaaluma na ufaulu kwa wanafunzi kudorora kutokana na walimu kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu mitaala mipya.
Kitendo cha serikali kubadili mitaala mara kwa mara kina shusha elimu, mtaala unabadilishwa bila hata mwalimu kupewa semina, kuna walimu wengine ni wazamani, tangu walipo jifunza mbinu za ufundishaji wakiwa chuoni hawaja wahi kupata semina.

Baada ya kubadilishwa kwa mitaala mipya, walimu wanaletewa wa fundishe bila semina na mbinu na elimu ya ufundishaji, matokeo yake wanashindwa kumudu masomo, hivyo kuwaathiri wanafunzi. Kubadilishwa huku kwa mitaala kunawafanya wanafunzi wasielewe somo kutokana na kutokuwepo kwa msimamo thabiti, hali inayo wapa wakati mgumu wanafunzi kuelewa somo.

Ni muda muafaka sasa kwa serikali yetu kuangalia upya jinsi ya kuboresha mitindo ya mitaala hiyo ya elimu maana ina wachanganya wanafunzi na walimu.

Mitaala imegeuzwa kuwa biashara binafsi za watu, kwasababu kila waziri anapoingia madarakani anakuja na mbinu zake mpya, anabadilisha mitaala iliyopo na kuweka ya kwake, mawaziri na wizira ya elimu wamegeuka wafanyabiashara wa elimu. Mitaala inapoandaliwa iwe ni ya kudumu siyo ya muda mfupi, kama ina mapungufu ifanyiwe maboresho siyo kubadilishwa, na vilevile uandaaji wa mitaala ushirikishe walimu, wazazi na wadu wa elimu kwani wao ndio walio karibu na mazingira yanayowazunguka wanafunzi wa kitanzania.​
 
Lakini huoni kwamba mitaala inabidi ibadilishwe kulingana na nyakati ili wanafunz waweze kukabiliana na changamoto za nyakati husika?
 
Kama Waziri anaona kuna umuhimu wa kubadili mtaala,anyway siyo mbaya sana. Lakini wadau wa elimu mfano WALIMU washirikishwe kwenye mabadiliko hayo ili nao watoe maoni yao.
WALIMU WANA UMUHIMU. FIKIRIA WEWE UMETOKA WAPI!!!!!!!!
 
Ahsante kwa mada nzuri sana
Mungai na sera yake ya kufuta kilimo ndo 7bu ya nchi kutokuwa na wataalamu wa kilimo, cha kushangaza sera ya kilimo kwanza inaanzishwa lkn waliojiunga na koz izo ni walosoma HGK,HGL,EGM.HGE. wizara wanapewa viongoz wenye mtazamo wa kikuku wanaotumia nguvu nyingi kuimarisha paa wakat mcngi umejengwa kwa mchanga, unategemea apo patajengeka?
 
Back
Top Bottom