Wanasiasa na mangimeza wetu wamefilisika hivi kifikra?

Mbunge

Senior Member
Aug 7, 2008
104
10
SIKUBALIANI kabisa na uamuzi wa serikali kusimamisha tiba ya Babu Samunge. Kama ni kujaa mbona Muhimbili hospitali ya rufaa ya taifa imejaa wagonjwa hadi kwenye sebule au corridors na hata neti zinazotolewa bure kwingine hapo hospitalini hazipo. Yaani ghafla wizara ya Afya ambayo imeishindwa Muhimbili inajifanya itaweza ya Samunge kwa Babu?

Nyie viongozi msituchengue. Kama mmeshindwa kazi acheni. Angalia kiongozi wenu anachokifanya. Huyo kapanda nege kwenda nje. Haoni kama WAGONJWA WANAOKWENDA LOLIONDO NI KITU KWAKE. Muhimu kwake na wasaidizi wake na pengine mabibi zao ni kufaidi masurufu na raha za kukaa hoteli za nyota 10 huko nje.

Hali ya Loliondo ilikuwa ikijulikana kabla ya ruhusa kutolewa kwa ndege za kijeshi kufanya mazoezi leo. Bajeti ya kuchoma mafuta ya ndege hizo ingelitosha kufanya mambo makubwa tu pale kijijini lakini watu hawawazi, hawafikiri na hawatumii akili ndio sababu mambo yanakwenda kama vile mswahili asiyesoma kabisa na nyumba yake ya mwanamke anayejua tu kujipamba na kula na hawazi ya kesho!
Rudini kwa kiongozi wenu mkamwambie kwamba Wagonjwa kwa Babu wanasema kama uliachia wezi wakasomnba mabilioni ya serikali/wananchi basi sasa ipakue hazina nzima ili haraka haraka Samunge pajengewe kila kitu kinachohitajika kupokea wagonjwa kati ya laki moja na laki mbili na wakitaka kukaaa mwezi mzima wakae hapo bila wasiwasi. Na hela zilizokupuliwa TRA majuzi ziende kujenga barabara ya pande mbili kati ya Arusha na Samunge fumba na kufumbua. Na FFU wapumzishwe kupiga watu virungu kwa muda kwa kwenda kuwa wajenzi wa barabara hizo.

Kama nakumbuka vyema maadui wa Watanzania according to baba wa Taifa walikuwa umasikini, ujinga na maradhi. Niliamini zamani kwamba ujinga ulikuwa ni kwa wananchi tu. Lakini hakuna ujinga mbaya na wa hatari kama ujinga wa viongozi. Na leo tunayaona haya. Tumefika tulipo hapa si kwa sababu ya ujinga wa wananchi bali kwa sababu ya ujinga wa viongozi wizara ya afya na serikali kuu. Mwenyezi Mungu atuvue na wajinga hawa inshallah!

Hebu fikiria kama adui yetu ni maradhi na anatokea mtu anayeweza kuponya watu elfu kwa siku halafu wewe unaidharau tunu hii tukuite nani ? Mheshimiwa sana au Mjinga sana!

Mngelikuwa na akili wizara ya afya hata kama rais hayupo mngeliitisha kwanza baraza la mawaziri mjadili jambo hili nyeti na la kufa au kupona kwa wananchi na pengine mngelipata mawazo mazuri zaidi kuliko kutoa tu amri ya kumtaka babu asimame kutoa huduma.

Hakuna Mtanzania hata akiwa waziri au rais mwenye akili kuliko Watanzania wote au jamii fulani wakiwekwa pamoja hata kama Watanzania hao ni wagonjwa kule Samunge eti!

Dawa ya Matatizo yetu Tanzania haiwezi kupatikana nje au kwa safari za kila mara kwenda nje. Dawa kama ilivyo kwa Mchungaji Ambilikile imo humu humu ndani. Tuwaulize wenzetu kwa miaka hamsini waliyokaa madarakani nini Wazungu na wengine walichotufanyia zaidi ya kutupa pipi za kutulevya na kuwa mateja yao. Na chochote walichotufanyia ni sawa na kutupa samaki kila siku na hakuna hata safari wametupa nyavu za kuvulia na kama zilitolewa basi walioko madarakani wanajua walikozificha. Sisi hatujaziona.

Nauliza swali hivi kiongozi wetu hakuwa na utambuzi na ufahamu kwamba tiba ya Loliondo kwa Mchungaji Ambilikile kule Samunge ni kitu muhimu zaidi kwa wananchi wake kuliko safari zake za nje. Na kwamba yeye akiwepo au asipokuwepo madarakani matatizo ya dunia yataendelea kuwepo. Lakini yeye ana uwezo wa kupunguza sana matatizo ya wananchi wake kwa kufanya mambo sahihi kwa wakati wake.
Nimpe kaka yangu huyu ushauri. Robo ya masurufu yake na watu wake kwa ajili ya safari za nje zisizowasaidia wagonjwa wa Tanzania ingetosha kabisa kujenga mahema elfu kadhaa ya kisasa kule Samunge, Vyoo elfu moja na kutoa mtaji kwa wanakijiji wa Samunge kuanzisha huduma mbalimbali ambazo zingeliwasaidia wagonjwa na wasindikizaji wao pale kijijini saa ishirini nne kwa siku, mara saba kwa wiki na siku 30 au 31 kwa miezi kadhaa ijayo.

Anapenda sana utalii bwana huyu. Hivi kashindwa kuona nafasi ya kipekee iliyojitokeza Loliondo toauti na uuzwaji vitalu na uwindaji holela ambako hatujui fedha zake zinakwenda wapi?
Hii ni nafasi ya kufuta umaskini katika wilaya ya Ngorongoro chini ya kipindi cha mwaka mmoja lakini Mheshimiwa hajui au anaichezea au anaidharau au hajasoma kabisa kile kinachowezekana kufanyika kwa sababu kajikusanyia washauri na mangimeza ambao sio chochote wala lolote ila watu wa kumwitikia yes, yes, yes na kujifanya wanyenyekevu sana kwake.

Mbona wajenmeni tunalitumia jeshi vizuri sana kutuliza fujo hata pale pasipokuwa na fujo ila kwa sababu tu hao walioko juu hawataki maanadamnano fulani yafanyike.

Jeshi hilo hilo leo lingelitumika kuhakikisha kunakuwa na barabara za pande mbili japo za kokoto kati ya Karatu na Samunge hadi nyumbani kwa Mchungaji Samunge.

Jamani huu ni ubabaishaji wa 'diamond jubilee' na sio 'silver jubilee' wallahi tena. Yaani tumekuwa na viongozi mbumbumbu kiasi hiki kuwa nafasi ya kutengeneza mabilioni kutokana na utalii wa ndani inapojitokeza vivi hivi tena yenyewe kwa kujileta bado hawaioni. Wametumia mabilioni mangapi kututangaza kiujanja ujanja huko Marekani wakati mabilioni yakiingia mifukoni mwao na sasa wamejenga mahekalu ndani na nje ya nchi kwa fedha za walalhoi. Lakini kwa kuwa wanadhani hawajulikani wanachokifanya wanajidai ni watakatifu na wenye nia ya kweli kutuendeleza.
 
Back
Top Bottom