Wanasiasa na Mabaraza ya Maaskofu wekeni hili sawa

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
19,639
33,414
Wakuu,

Naomba leo niseme na mabaraza yote na kila umoja wa Kikristo hapa Tanzania. Lipo jambo ambalo limemea hapa Tanzania na pengine halipo kwingine na ni aibu kwa Ukristo ingawa tunaweza kuona ni dogo.

Wakristo kuna madhehebu mengi sana lakini pamoja na tofauti zetu kubwa yapo mambo mengi pia ambayo hatutofautiani kwa wengi wetu. Ni ngumu kuondoa hizi tofauti lakini tofauti zingine ni za kijinga mno! Hivi kwanini tumebariki kuonesha TUMSIFU YESU KRISTO na Bwana YESU ASIFIWE zitumike kutugawa?

Najua kila upande unaweza kufafanua mantiki ya salamu yao lakini ni ujinga kutumia salamu hizi kuonesha utofauti wa madhehebu. Tofauti za madhehebu zipo wazi hazihitaji salamu kutofautisha.

Wenzetu Waislamu pamoja na tofauti zao lakini si kwenye salamu ambayo haina mantiki kutofautiana zaidi ya kuonesha ipo roho chafu zaidi ya tofauti zetu.

Natoa mwito kwa umoja wa madhehebu yote utoe tamko kuwa viongozi wote na wanasiasa watumie salamu moja wapo inatosha na inawakilisha UKRISTO. Kama mtu akisikia TUMSIFU YESU Kristo bila Bwana YESU asifiwe akanuna huyo anamtindio wa ubongo

Lakini pia kwenye hadhara ambayo si ya kidini nafikiri hizi salamu hazihitajiki hata kama viongozi wa dini wapo. Wanasiasa rekebisheni mazoea ya hizi salamu kwenye maeneo ambayo si lazima. Kwanza salamu zenyewe zinatugawa tu maana dini si mbili tu hapa Tanzania.

Tuachieni hizi salamu makanisani na misikitini
 
Hivi hata wanasiasa wengine duniani lazima wasalimie Kikristo na Kiislamu? Haka katrend inabidi kakomeshwe. Salamu za dini zibakie kwenye ibada na waamini wakikutana.

Leo tunaanza na salamu huko mbele kuna mambo mengine ya kidini yataanza kuwekwa na wanasiasa.
 
Vipi na Ile kiongozi anazindua mradi au program fulani halafu msururu wa viongozi wa Dini wanaanza kufungua, unaweza kuta maaskofu hata 10 kutoka Makanisa mbalimbali na Shehe mmoja kutoka kwa Waislam

Haya mambo hayatakiwi kuwepo, Kama Ni kuombea Basi anatakiwa atoke mtu mmoja tu aombe maombi ambayo yapo neutral maana wote wanaamini Mungu

Mfano shuleni kwetu kipindi Cha mtihani alitoka mtu mmoja anaomba kwa niaba ya Dini zote kwa Sala ambayo sio ya Kikristo Wala Kiislam Bali ya kumuomba Mungu, Kama Haiwezekani Basi haya maombi yapigwe marufuku, Ni kupoteza muda
 
Tuangalie namna tunavyotumia mambo ya dini kwa ujumla. Ila hili la salamu linanikera sana.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom