Wanasiasa na Biashara ya madawa ya kulevya

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,166
Viongozi wanne wa serikali ya Kenya (hawakutajwa majina) leo wamepigwa marufuku kuingia US kwa kuhusika ktk biashara ya madawa ya kulevya. Taarifa hii imetolewa na Balozi wa US nchini Kenya. Hili ni huko Kenya.

Hivi karibuni huko Mwanza, juhudi za wazi na za nguvu za kumurudisha kijana Masha ktk nafasi ya ubunge zilishindwa na sasa kuna fununu zinazunguka juu ya sababu ya kijana huyu kung’ang’aniwa kiasi hicho na hasa mkuu wa nchi (kama wananchi walivyoona). Wanadai kuna biashara halamu ya madawa inafanywa na marafiki hawa.

Ni fununu mbaya sana lakini ipo na bado Mwanza wanajiuliza sababu kubwa ya urafiki huo. Na kwa hili la leo huko Kenya linanipa taabu kwamba wanasiasa wetu wa kiafrika wapi hasa wanakwenda?
 
nahofia tu albino wetu waliopoteza maisha kama mikono ya wanasiasa haina damu zao
 
Cha ajabu hawa USA na nchi za Magharibi wanaifuatilia Kenya tu, Tanzania hata tufanye nini hawana time. Kenya wakifanya kitu kidogo wanastuka lakini Tz la!
 
Kulikuwepo ripoti zisizothibitishwa Mwanza kabla ya uchaguzi kuwa Ridhwani alijaribu kumhonga mgombea wa CHADEMA shilingi milioni 300 ili asigombee. Ukiunganisha dots unaona thread ya uhusiano wa Masha na Ridhwani.
 
Viongozi wanne wa serikali ya Kenya (hawakutajwa majina) leo wamepigwa marufuku kuingia US kwa kuhusika ktk biashara ya madawa ya kulevya. Taarifa hii imetolewa na Balozi wa US nchini Kenya. Hili ni huko Kenya.

Hivi karibuni huko Mwanza, juhudi za wazi na za nguvu za kumurudisha kijana Masha ktk nafasi ya ubunge zilishindwa na sasa kuna fununu zinazunguka juu ya sababu ya kijana huyu kung'ang'aniwa kiasi hicho na hasa mkuu wa nchi (kama wananchi walivyoona). Wanadai kuna biashara halamu ya madawa inafanywa na marafiki hawa.

Ni fununu mbaya sana lakini ipo na bado Mwanza wanajiuliza sababu kubwa ya urafiki huo. Na kwa hili la leo huko Kenya linanipa taabu kwamba wanasiasa wetu wa kiafrika wapi hasa wanakwenda?

Hapa JF iliwahi kuwepo sehemu ya kuweka nyepesi-nyepesi, naona inabidi irudishwe tena.
 
Kulikuwepo ripoti zisizothibitishwa Mwanza kabla ya uchaguzi kuwa Ridhwani alijaribu kumhonga mgombea wa CHADEMA shilingi milioni 300 ili asigombee. Ukiunganisha dots unaona thread ya uhusiano wa Masha na Ridhwani.

Majaribio kama hayo yalisika koote ambako vigogo wa CCM waliangushwa. Hiyo ndo sababu ya wananchi kuchachamaa ili kuwatia adabu pia wagombea ambao wangeweza kutamani kitita kama hicho.
 
Kulikuwepo ripoti zisizothibitishwa Mwanza kabla ya uchaguzi kuwa Ridhwani alijaribu kumhonga mgombea wa CHADEMA shilingi milioni 300 ili asigombee. Ukiunganisha dots unaona thread ya uhusiano wa Masha na Ridhwani.

1. Ridhiwani ni mwajiriwa wa IMMMA advocates eenh?
2. Masha ni mkurugenzi wa IMMMA advocates eenh?
3. IMMMA advocates ndiyo alikuwa baba wa Deep Green Finance eenh?
4. Deep Green Finance ilitajwa kwenye harakati za kuchakachua lile li-account letu la EPA eenh?
5. Mshiko uliotoka EPA ndio unasemekana ulimwingiza Muungwana kwenye li-state house letu eenh?

Kazi kweeeli kweli!
 
Back
Top Bottom