Wanasiasa mnatumaliza: Watoto wa walala hoi sasa kukiona katika shule za st kayumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanasiasa mnatumaliza: Watoto wa walala hoi sasa kukiona katika shule za st kayumba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jan 29, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Kwakuwa watoto wao wanakwenda hizo St nini sijui na Academy gani sijui hili kwa Waziri hawoni shida kulitamka kwenye majukiwaa na kugeuka kuwa sera. Hawa ni wengi na wakishindwa kumudu elimu hii watamudu elimu ya mtaani, tunajua watajifunza nini? Na watatumiaje elimu hiyo? Kwa Waziri mchango huo ukizingatia viposho vya bungeni na vikao kadhaa n.k. haoni kama ni kitu ambacho yuko mtu atashindwa, upofu wa ajabu kabia. Sijui kama serikali inaona pengo inalolitengeneza? Mahesabu yake hayasomeki kabisa maana hata Health insurance sio ghali hivyo, na sina uhakika hiyo capital grant kama ipo bado. Ninatishwa na pengo la elimu linalojengeka katika nchi hii:

  Tamko hilo lilitolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Philipo Mulugo alipokuwa akizungumza na wakuu wa shule za msingi na sekondari jijini Dar es Salaam.

  "Lakini michango hii yote ihakikishwe inatolewa kwa risiti ili nitakapokuja kutembelea, ama mzazi akitaka kujua matumizi, aonyeshwe kihalali na sio kuchukua fedha hizo na kuzitumia mnavyojua,” alionya naibu waziri huyo.

  Alitaja michango inayoruhusiwa na viwango vyake kwenye mabano kuwa ni tahadhari (Sh5,000), taaluma (Sh15,000), vitambulisho (Sh5,000), nembo ya shule (Sh2,000) na madawati (Sh15,000) . Alisema fedha hizo zinapaswa kutolewa kabla wanafunzi hawajaanza masomo.

  Waziri abariki michango shule za msingi
   
 2. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 586
  Trophy Points: 280
  juzi mdogo wangu ananipigia simu nimtumie ada ya mtihani wa 4m 4, nimejiuliza mengi, serikali mwaka jana walifuta ada zote za mitihani ya taifa kwa shule za serikali, imekuaje zimerudi kimya kimya? aisee zis kantri iz krezi kwakweli.
   
Loading...