Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 58,978
- 103,352
Unaponishangaza ni hapo unaposema eti 2020 hakuna mtu atasimama kwenye Foleni ya uchaguzi.
Mkuu Kama dunia ingekua na watu wanaofikiri na kukata tamaa hivyo dunia bado ingekua kwenye shimo la Giza totoro.
Kumbuka Mgurugenzi ni binadam kama wengine.
Asipodhibitiwa na kupata machungu atajiinua na kuangalia maslahi yake badala ya sheria kwa kuumiza wengine ili familia yake ishibe.
Eye with eye!
Kwenye mpira Refa aliyezoea kubeba timu yake , akijua kuwa timu pinzani wanajua kupigania haki yao na mashabiki wake wanajulikana kuwa hawana uvumilivu wa kuhujumiwa ni lazima refa afuate kanuni kuokoa pumzi yake.
Usifikirie hao CCM wanaofurahiya wizi wa kura hawajui kua kuiba kura ni kinyume na Vitabu vya duni,sheria za nchi na hata maadli ya binadam waliostarabika. Wanajua sana Ila wanachoangalia ni maslahi.
Mfamo Spika alituambiwa TL Mbunge kwa Mwaka mmoja amelipwa zaidi ya mil. 200 tena akiwa kitandani.
Chama tawala wanajua utam wa kushika funguo za hazina. Wanajua utam wa kushika dola.
Wapinzani bado wanashangaa shangaa wakati wenzao wanapambana.
Kila unayemuona anapambana kufa na kupona kutetea ugali wake.
Ukimuona anayegawa fomu anapigania ugali .Mlinzi anapigania ugali wake, anayegombea hasa wa chama tawala anataka agawiwe ugali wake kwa namna yoyote. Kama utakua na mgombea wa upinzani ambaye anasubiri apewe haki Mezani atapata makombo.
Usione watu wanahujumu wapinzani ni feza babu .
Wajipange kukabiliana na uovu wa kuhujumu zoezi la uchaguzi kwa namna yoyote mana wao ndio wanaotafuta nafasi za ubunge zenye maslahi na familia zao.
Kama mtu unapeleka mke wako kliniki Marekani halafu unalala kama ndezi uibiwe kura na vibaka halafu unabaki kulia badala ya kumliza mwizi ,utakua hujui umuhimu wa nafasi unayoitafuta.
Mtu unarudisha form peke yako barabarani halafu eti wanatokea vibaka wanakupora na wewe unabaki ukigaragara Chini kama mwehu badala ya kutafuta vijana wa kukusindikiza tena wakiwa na viberiti ili akijitokeza kibaka mporaji wa form basi anavuna anachopanda kama vibaka wengine.
Kila mtu alinde anachokitafuta kama ana uhakika wa kukipata.
Ni wazi kuwa Chama Kikongwe wamekua kama kundi la wapigaji wanaojipanga muda wote kufa na kupona ili tu washike nafasi za kuweza kuwapatia fedha za walipa kodi kwa UDI na uvumba. Hawa hawaangalii ubinadam wala sheria wanachojali ni kugawana nafasi za kupata hizo pesa.
Wakiachwa wanageuka kuwa kama wahalifu alimradi wapate nafsi hizo za ubunge ambazo zina maslahi makubwa.
Ww unaongea nadharia za kutokukubali hujuma, mimi nakuambia uhalisia. Kwa taarifa yako sina uoga hata chembe, nazungumzia jamii inayopaswa kuungana kuzuia hujuma. Jamii ni kama imeridhika, na wapinzani wenyewe wamechangia huu ukondoo kuingia kwenye jamii. Siwezi kwenda kupanga mstari na kuhatarisha usalama wangu kisha ninayemchagua anakwenda kuungana na waliohatarisha usalama wangu. Jamii itakapoamka na kuona inaumia itachukua hatua japo kwa machungu. Kwa sasa hapa jamii forums ndio uwanja wangu wa mapambano na ushahidi wa hiyo vita ni kilio cha huyu mleta uzi.